Thursday, September 30, 2010

WAMEJAA TUMAINI NA WANAAMANI NO.2

Watoto wa Mungu hawa ni wa Moshi na ninao wengine wa Kinondoni Hananasifu - DSM na LWC Kawe DSM more pictures to come stay tune mwenye kutaka kuwasaidiaaa anakaribishwa tuwasiliane kwa njia ya e-mail tuone jinsi ya kuwawezesha hawa viongozi, watumishi wa kesho. Barikiwa


















Watoto waliojaa matumaini. Huyu mmoja kama hajashiba vile?
Na mwingine anaona kama yeye hatapewa daftari vile anasubiri kwa haaamu
Mungu ni mwema sana jamani aliposema atakuwa baba wa Yatima analidhihirisha
neno lake sasa. Wakirudi nyumbani wanakung'uta tu miguu wanalala kitumbo ndiii.
Tuzidi kuwapenda na kuwasaidia.

Wednesday, September 29, 2010

JE WAJUAA? NO2.

Biblia inasema hiviii,
"Maskini hutumia maombi, Bali tajiri hujibu kwa ukali.''
Jibu  :  Maneno ya vinywa vyetu yatiwe munyu.

MWALIKO! MWALIKO! NO.7

KANISA LA LIVING WATER CENTRE MAKUTI KAWE WANAKUKARIBISHA KWENYE IBADA YA MJINI KILA IJUMAA INAYOFANYIKIA KATIKA JENGO LA HAIDERY PLAZA GOROFA TA PILI ''UKUMBI WA ONION'' KUANZIA SAA KUMI KAMILI JIONI.
KWA WALE WAFANYAKAZI WA MJINI POSTA NA MAENEO YA JIRANI AU KAMA UMEBAHATIKA KUWEPO JIONI MAENEO YA POSTA UNAKARIBISHWA KWENYE IBADA HII UJE UPATE KUPOKEA CHAKULA CHA KIROHO KUTOKA KWA WATUMISHI WA MUNGU WAPAKWA MAFUTA WA BWANA APOSTLE ONESMO NDEGI PAMOJA NA MAMA LILIAN NDEGI.
KWA NINI UKAE KWENYE FOLENI KWA MUDA MREFUUUU NI BORA UPATE NENO AMBALO LITAKUSAIDIA WAKATI UKISUBIRI FOLENI IPUNGUE UENDE NYUMBANI KWA URAHISI NA KWA HARAKA UKIWA UMEJAA FURAHA NA AMANI TELE.
WOTE MNAKARIBISHWA NA BWANA AKUBARIKI SANA SANA

Daily Grace by Joseph Prince











The Lord Is Able And Most Willing
Matthew 8:3
3Then Jesus put out His hand and touched him, saying, “I am willing; be cleansed.” Immediately his leprosy was cleansed.

When you see someone receiving a miraculous healing or financial breakthrough, do you ask, “What about me, Lord?” I believe that the leper who came to Jesus must have asked the same question.

He must have heard or seen from a distance, since he was not permitted to be in public places by the law, how Jesus had healed the sick. So he had no doubt that Jesus could heal him, but he was not sure if Jesus would. He said to Jesus, “Lord, if You are willing, You can make me clean.” (Matthew 8:2) He was confident of the power of God, but not the love of God for him.

Like the leper, maybe you don’t have a problem believing that God can give you your miracle, since He is Almighty God. But you are wondering if He will do it for you. My friend, let Jesus’ actions and answer to the leper settle this question once and for all. He stretched forth His hand, touched the leper and said, “I am willing; be cleansed.” And immediately, the leper was healed.

I want you to notice that Jesus touched the leper. He could have healed him from a distance with just a spoken word. He had healed others this way as in the case of the centurion’s servant and the Syro-Phoenician woman’s daughter. So why did He touch the leper?

Jesus knew that for so many years, the leper had been cut off from his family and society, so he must have been feeling dehumanized. I believe that Jesus touched him to make him feel human again, to make him feel loved and accepted again. His touch was His love language to the leper.

Can you see God’s heart of love here? Can you see how much He loved the leper? That is how much He loves you! The day that you come to know God’s heart of love and believe that He wants you blessed more than you want to be blessed is the day that you receive your miracle!

Beloved, catch a glimpse of God’s heart of love, and you will believe that He is not only able, but also willing to make you whole!

Tuesday, September 28, 2010

JE WAJUA? NO. 1

Biblia imetuambia hiviii.
"YEYE ARUDISHAYE MABAYA BADALA YA MEMA, MABAYA HAYATAONDOKA NYUMBANI MWAKE."

Hivyo ndugu usishangae kuona nyumbani mwako mambo yanaenda kombo kila wakati hebu jihoji kuhusiana na hili jaribu kutengeneza ulipokosea na Mungu wangu aliye hai atakuweka huru tena.
JIBU:    USHINDE UBAYA KWA WEMA.

WAMEJAA TUMAINI NA WANAAMANI

Bwana Yesu akasema "WAACHENI WATOTO WAGODO WAJE KWANGU MSIWAZUIE KWA MAANA WATOTO KAMA HAWA UFALME WA MBINGUNI NI WAO" Yesu alikuwa na maana gani? (tafakari)

Bado wamejaa tumaini wanaamani ya kweli kutoka ndani ya moyo ingawa
ni watoto yatima na baadhi wamepoteza wazazi wao either wote 2 au mmoja.
tuzidi kuonyesha upendo kwao na kwa watoto wengine tusiwasahau katika maombi yetu.

Monday, September 27, 2010

DAILY GRACE BY JOSEPH PRINCE











Which Righteous Man Do You Want To Be?
Genesis 24:1
1Now Abraham was old, well advanced in age; and the Lord had blessed Abraham in all things.

The Bible says that Abraham was righteous. But do you know that his nephew Lot was righteous too? (2 Peter 2:7–8) Yet, both men lived very different lives. Although they both lived under God’s grace some 400 years before the law was given, Abraham was very blessed, whereas Lot lost a lot!

Both men had large herds and flocks. When their herdsmen started quarrelling over space, Abraham took the initiative to make peace. He even let Lot pick the lands that he wanted. Both men were righteous, but one was more gracious than the other.

Lot picked the well-watered plain of Jordan, where the cities of Sodom and Gomorrah were. He dwelt there and pitched his tent as far as Sodom. Eventually, he lived in Sodom. Now, Sodom and Gomorrah in the Bible represent a sinful lifestyle. Some Christians think, “Since I am righteous by faith and under God’s grace, I can live a sinful lifestyle.”

Well, let’s learn from Lot. He first saw Sodom, then his feet walked toward it and finally he went into it. I like what a great man of God said: “Sin will take you farther than you want to go, keep you longer than you want to stay and cost you more than you want to pay.” What did Lot end up paying?

He was captured when four kings plundered Sodom and Gomorrah. And even after Abraham rescued him with the help of God, he did not learn his lesson. He went back to Sodom. Some Christians live from one bail-out to another. God delivers them from, say, debt, and they go right back to borrowing money or gambling! Sodom and Gomorrah were eventually destroyed. Lot escaped with only the clothes on his back and even lost his wife in the process.

Beloved, you are the righteousness of God in Christ. When you truly understand what Jesus did to make you the righteousness of God, it will cause you to fall out of love with sin and fall in love with God. Then, it will not be hard to have a heart for God, as Abraham did, and like Abraham, be blessed in all things!

MWALIKO MWALIKO NO. 6 (SAFARI YA KUTEMBELEA NCHI YA ISRAEL)

Living Water Center Makuti Kawe inawakaribisha wale wote wanaopenda kwenda kutembelea nchi ya Israel mwakani wakati wa pasaka. Safari itakuwa ni ya siku tisa(9) siku mbili za safari siku saba za kutembelea nchi Teule ya Bwana. Gharama ni $ 2700 hii ni nauli ya kutokea Dar es Salaam kwenda Israel na kurudi na gharama za kuishi kule kwa muda wote wa siku saba. Wote mnakaribishwa.

Bendera ya Israel

Sehemu Teule Israel

Uwapo kwenye maombi usisahau kuiombea nchi hii ya Israel kwani Bwana Mungu asema hivii...
"yeyote atakayeibariki Israel atabarikiwa na atakayeilaani atalaaniwa" (tafakari)

Sunday, September 26, 2010

ROHO MTAKATIFU ALIVYOCHUKUA NAFASI KATIKA MKUTANO WA WAMAMA LWC - MAKUTI KAWE



JANA (25/9/2010) ILIKUWA NI SIKU YA MKUTANO WA WAMAMA KANISANI LIVING WATER CENTRE MAKUTI KAWE. MKUTANO ULIKUWA MZURI SANA NA BWANA ALIWATUMIA WATUMISHI WA BWANA WALIOSIMAMA KUTOA NENO KWANI ROHO MTAKATIFU ALISHUKA NA NGUVU ZAKE NA UTUKUFU WA MUNGU UKATAWALA. TUMSHUKURU MUNGU SANA KWA KUWA  NI MWAMINIFU NA MTIIFU NDANI YA MAISHA YETU.

MWALIKO NO. 5 INVITATION

Don’t miss a special service that will
CHANGE YOUR LIFE!
The Brooklyn Tabernacle Choir sings with all their hearts &
Pastor Jim Cymbala speaks on
How to Kill the Weeds of Worry
All at 3 PM this Sunday... (26/09/2010)
DON’T MISS IT!

Daily Grace Inspirations By Joseph Prince



Let The Lord Be Your Defense
Psalm 94:22
22But the Lord has been my defense, and my God the rock of my refuge.

Imagine being a poor widow, a stranger in the land and holding one of the lowliest jobs in society. That was Ruth’s situation, so it would have been easy for her to feel vulnerable and defenseless. But because she trusted the Lord (Ruth 1:16), He placed her under Boaz’s protection.

Boaz, the owner of the field she worked in, commanded his young men saying, “Let her glean even among the sheaves, and do not reproach her.” (Ruth 2:15) What he was saying to his men was this: “She might be a gleaner, but because I care for her, treat her with respect and make sure she is not put to shame.”

Boaz is a picture of our Lord Jesus. If you are feeling vulnerable and defenseless right now, imagine Jesus commanding His angels, “Watch over this one who belongs to Me. Make sure he is treated with respect and not put to shame because he is someone I love and someone whom I died for.”

God’s Word tells us that if God is for us, who can be against us? (Romans 8:31) No one who has set himself against us can prevail because when God is for us, His protection is upon us. That is why I have never answered any of the poison email messages which I have received in the course of my ministry.

My attitude is this: Jesus is my defense. If He does not defend me, it means that there are things in my life that are not to be defended, and I would be glad to find out about them now rather than later. On the other hand, because I take the Lord as my defense, and He defends me, what can those who are against me do to me?

When you defend yourself, you have only your two hands and your own human resources. But when you let Jesus take up your defense, He defends you with His nail-pierced hands and His legions of angels! The results will be amazing.

Beloved, the Lord is your defense and refuge. Trust Him to defend and protect you!

Friday, September 24, 2010

KUHUSIANA NA EMMANUEL TV

NAJUA BAADHI YA WATANZANIA WENZANGU MNAPENDA SANA KUSIKILIZA MAFUNDISHO YA MTUMISHI WA MUNGU T. B. JOSHUA NA KITUO CHAKE CHA TELEVISION CHA EMMANUEL MNAKIPENDA SANA LAKINI SOMA HII UONE SHETANI  ANAVYOWEZA KUPENYA SEHEMU ZILE WATU WENYE KIU NAZO

Naomba uwahabarishe wadau ,Kuna matapeli wameingia nchini Tanzania ( Dar es Salaam) wanadai wao ni representatives wa T.B. Joshua wa SCOAN na Emmanueli TV. SCOAN wamekanusha kutuma representative nchini, hivyo kuweni makini. Matapeli wa aina hii wameenea duniani ambao hujipatia mali kwa jina la T.B.Joshua na Emmanuel TV.
Kwa habari zaidi angalieni Emmanuel TV au someni kwenye mtandao www.emmanueltv.com.
Asanteni na tuwe makini na hawa matapeli
(kwa hisani ya Michuzi)

TUELIMISHANE

Kusema kweli mimi wakati mwingine nashindwa kuelewa hapa naomba msaada wenu jamani kujua tofauti ya hawa wenye kazi hii na wale tunaokwenda kwa ajili ya mambo mengine mengine (wale tunaopenda kuvunja kazi zao na mipango yao katika jina la Yesu) yaani waganga wa kienyeji. Je hawa si wale wale jamani au ni sawa na hospitali kwa daktari unakwenda basi na hawa ndio jambo moja. Nina maswali mengi mno naamini na nyie ndugu mnayo tusaidiane kuelimishana pia tusisahau kuiombea nchi yetu tuwapo kwenye maombi jamani.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Blandina Nyoni akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa tiba za asili Dkt. Ahmad Darusi kuhusu namna ya kutumia Dawa aliyoitengeneza yenye uwezo wa kuwasaidia wagonjwa wa UKIMWI wakati wa sherehe za uzinduzi wa Usajili wa waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.
Katibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Bi. Blandina Nyoni akituma fomu za usajili wa waganga wa tiba za asili na tiba mbadala kwa njia ya mtandao katika mikoa yote ya Tanzania leo jijini Dar es salaam fomu ambazo zitapatikana kwenye ofisi za Halimashauri kote nchini kwa ajili ya usajili. Wanaoshudia Kulia ni Mganga mkuu wa serikali Dkt. Deo Mutasiwa na Msajili wa Tiba za Asili na Tiba Mbadala Dkt. Paul Muhani (Kushoto).

 Baadhi ya wataalam wa Tiba za asili wakiwa na dawa mbalimbali za asili walizozitengeneza tayari kwa maonyesho leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Usajili wa waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.

(Hii ni kwa hisani ya blog ya Isaa Michuzi)

KUHUSU VAZI LA KWENDEA KANISANI

KUMBE LIPO JAMBO KATIKA VAZI LA KANISANI
Nimekutana na mtumishi mmoja wa Bwana dada mtanashati ambaye aliwahi kushiriki Miss Tanzania miaka ya nyuma na kwa sasa ameokoka na Bwana anamtumia tukawa tunazungumza kuhusiana na VAZI LA KWENDEA KANISANI (hii ni kutokana na post zangu za nyuma) akasema yeye ameipata hii kutoka kwa mtumishi wa Mungu mmoja ambaye alimwambia kuwa si kwamba makanisa wanakataza uvaaji wa mabinti au wamama kuvaa vimini kanisani (na makanisa mengine hata suruali kwa wanawake wanakataza) tatizo linakuwa ni kwa hao Baba zetu na kaka zetu ambao tamaa ya mwili bado kufishwa kwani wakiona wadada wamevaa namna hiyo na akiwa ibadani basi mambo ya ibada yanaishia hapo hapo inakuwa tena umempeleka sehemu nyingine kabisa na hata neno kusikiliza inakuwa ngumu. Kwa hiyo inakuwa uwepo wake ibadani siku hiyo ni ya bure hapokei kitu kabisa.
Na huyo mtumishi wa Bwana pia akatoa mfano wa akina mama/dada wengine wanaokaa viti vya mbele kabisa wengine wanajisahau sana unakuta anakaa vibaya hivyo pia inampa wakati mgumu mtumishi wa Bwana wakati yuko mbele anatoa Neno la Mungu kwani kukwambia kaa vizuri anashindwa na yeye ni mwanaume rijali basi inabidi aweke macho pembeni ili kuweza kutokuvutiwa na kuchungulia kwani anasema wao pia ni binadamu na shetani anatafuta kila njia ya kuweza kuwaangusha. "Kumwingiza mtumishi wa Mungu majaribuni ni laana kubwa tena kubwa sana."
Hivyo basi cha msingi wanachoona kinafaa kufanya ni kuwaambia wamama na wadada wavae nguo ndefu na magauni mapana au wasivae suruali kama sheria ya kanisa ili kuepusha kuwapoteza au kuwakwaza au hata kuwaingiza majaribuni baadhi ya wababa na wakaka na hata baadhi ya watumishi wawapo kwenye uwepo wa Mungu (kanisani)

Nadhani nitakuwa nimeleweka kama sivyo, namsihi Roho Mtakatifu aliye mwalimu mkuu akueleweshe.
Vazi la kanisani linatakiwa kuwa hivi wapendwa. (Haswa kwa wale wakaaji wa mbele kabisa)

Helen & Mama miezi kadhaa iliyopita Brooklyn Tabernacle tukitoka kanisani.

Mtoto wa Kifai (Matechi's la familia)
yeye hutoka hivi kwenda kanisani.

FRIENDSHIP

Friendship is not about who you have known the longest..........
but about who came and never left your side..
Four things you can't recover:
The stone.........after the throw. The word..........after it's said.
The occasion........after it's missed. The time.........after it's gone.


Knock, Knock I knocked at heaven's door this morning. God asked me...'My child, what can I do for you?' And I said, 'Father, please protect and bless the person reading this message.' God smiled and answered....'Request granted'.

Thursday, September 23, 2010

Huduma ya Living Water Centre Ministry

Je waifahamu Living Water Centre Ministry iliyopo Kawe Dar Es Salaam.
Kutana na watumishi wa Mungu wapakwa mafuta wa Bwana ambao Roho Mtakatifu anawatumia kweli kweli. Kwa habari zaidi mafundisho sahihi ya neno la Mungu maombi na maombezi basi fika kanisani LWC upate kubarikiwa, kufunguliwa na upate kuijua kweli na hiyo kweli ikuweke huru.

Mtumishi wa Mungu Aunty Peace akiombea
















Maombezi yakifanyika kanisani LWC


Maombezi yakiendelea kanisani LWC - Makuti Kawe

Karibu katika huduma ya Living Water Centre:

RATIBA NA MATUKIO MUHIMU YA LIVING WATER CENTRE MINISTRY
Tarehe: 26/09/2010
Muda kuanzia: Saa Tatu na Nusu Asubuhi
Tukio : Ibada ya Neno na Kusifu
Mahali : Kanisani, Living Water Centre - Kawe

Tarehe: Kila siku za Alhamisi
Muda kuanzia: Saa Nne Usiku
Tukio : Mkesha Maalum kwa Mabinti - Na. Mchungaji Paschal.
Mahali : Kanisani, LWC-Makuti, Kawe


Tarehe: Kila siku za Ijumaa
Muda kuanzia: Saa Nne Usiku
Tukio : Mkesha Maalum kwa Vijana wa Kiume- Na. Mchungaji Paschal.
Mahali : Kanisani, LWC-Makuti, Kawe


Tarehe: Kila siku za Ijumaa
Muda kuanzia: Saa Saba Mchana (1:00pm)
Tukio : Ibada ya Mjini Dar Es Salaam, kwa Wafanyakazi na Wenyeji wote.
Mahali : Kanisani, LWC-Makuti, Kawe


Tarehe: Kila siku za Jumanne
Muda kuanzia: Saa Nne Asubuhi hadi Saa Sita na Nusu (10:00am - 12:30pm)
Tukio : Darasa la kuukulia wokovu, Maombezi na ushauri wa Mtu mmoja mmoja hadi saa 11.Jioni.
Mahali : Kanisani, LWC-Makuti, Kawe


Tarehe: Kila siku za Jumatano hadi Ijumaa
Muda kuanzia: Saa Tisa Alasiri hadi Kumi na Mbili jioni (3:00pm - 6pm)
Tukio : Mazoezi ya Timu ya Kusifu na Kuabudu
Mahali : Kanisani, LWC-Makuti, Kawe


Tarehe: Kila siku ya Ijumaa ya Mwisho wa Mwezi
Muda kuanzia: Saa Nne Usiku (10:00pm - asubuhi)
Tukio : Mkesha wa Vijana Wote
Mahali : Kanisani, LWC-Makuti, Kawe



WOTE MNAKARIBISHWA USIKOSE!!!

NENO KUTOKA KWA MAMA LILIAN NDEGI

LIVING WATER CENTRE - MAKUTI KAWE


Ibada ya Jumapili: 12/09/2010 -: Maisha ya Kuongozwa na Roho Mtakatifu
Fuatilia Mfululizo wa somo hili kwenye Website ya Kanisa.

...Ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa kutupa Waamini sisi tulio mwamini, Kiongozi ambaye wakati wote nia yake ni kutufikisha katika burudiko la kweli. Sisi tukiwa kama binadamu, tumeumbiwa kuongozwa na utawala fulani katika maisha yetu. Katika hali yoyote, binadamu lazima aongozwe na utawala mmoja kati ya Utawala wa Giza uliotawaliwa na Dhambi na Mauti, au Utawala wa Nuru, uliotawaliwa na Uzima wa Milele na Bududiko la kweli katika Kristo Yesu. Utawala wa Nuru, ni utawala wa Roho Mtakatifu ndani ya Maisha ya Mwamini. Utawala wa Roho Mtakatifu, wakati wote ni utawala wa faida, ni utawala uliojaa Upendo usio kifani, na gharama yake hailinganishwi na kitu chochote, kiwe Fedha, Dhahabu n.k. Ni utawala wenye ukamilifu katika kila idara ..
Fuatilia Somo letu la jumapili iliopita, lenye kichwa cha Somo "Maisha ya kuongozwa na Roho Mtakatifu" kama lilivyoletwa kwetu na Mtumishi wa Mungu Mama Lilian Ndegi.

RATIBA NA MATUKIO MUHIMU YA LIVING WATER CENTRE MINISTRY
Tarehe: 26/09/2010
Muda kuanzia: Saa Tatu na Nusu Asubuhi
Tukio : Ibada ya Neno na Kusifu
Mahali : Kanisani, Living Water Centre - Kawe >>ratiba zaidi >>
Pia, muda si mrefu tutapatikana katika Facebook na Twitter

Wednesday, September 22, 2010

MWALIKO NO. 4 "MARRIAGE COUPLES"

The Brooklyn Tabernacle Marriage Ministry invites all Married Couples for

CHIP INGRAM’S DVD STUDY ON COMMUNICATION

Special Speaker: Pastor Alex Burgos 
 Thursday, September 23 @ 7pm
 180 Livingston Street, Hall 1A
Refreshments will be served at 6:30pm  (Owkay here we go sisi tupendao kula oopss am jocking Wamarekani hapa ndio nimewavulia kofia du kama sisi tunasema 'wakati wote ni wakati wa chai' wao husema wakati wote ni wakati wa kula haijalishi unatembea, uko njiani uko kwenye gari, kazini we twende namshukuru Mungu kanisani wanasema noooo big noooooo!! "food is not allowed" otherwise aha watu wangekuja na sufuria kanisani Mungu pembeni tuanze kula halafu ndio Neno la Mungu lifuate  (nkiki tupu, mweee, haiombe!!")
RSVP appreciated to marriageministry@brooklyntabernacle.org

Daily Grace Inpirations From Joseph Prince Ministries "KARIBU UPATE CHAKULA CHA ROHO"



Speak God’s Word And Activate His Angels Psalm 103:20
20Bless the Lord, you His angels, who excel in strength, who do His word, heeding the voice of His word.

Notice that the verse says that angels are “heeding the voice of His word”. Now, who gives voice to God’s Word? We do! Each time we speak God’s Word, we give voice to His Word. And when angels hear His Word given voice, they respond!

The Bible says that at the end of Daniel’s three weeks of fasting and praying for an answer from God, the angel Gabriel appeared to Daniel and said to him, “I have come because of your words.” (Daniel 10:12)

So when angels hear you saying, “Thank You, Father, no evil shall befall me nor shall any plague come near my dwelling,” (Psalm 91:10) they will come to your aid because you are giving voice to God’s Word. Even if you cannot quote the verse perfectly, they can still come to your rescue.

This was what happened to a lady in the United States. While walking home after an evening church service, she was attacked from behind by a man and dragged toward a dark corner in an alley. In that frantic state, she remembered only one word from that evening’s sermon. So she shouted, “Feathers! Feathers!” Her attacker released her and fled!

Feathers? What did she mean? She was actually referring to Psalm 91:4 — “He shall cover you with His feathers, and under His wings you shall take refuge”. In that state of panic, she remembered only one word — “feathers”, and it was enough to cause her attacker to flee. You see, it is not your ability to quote an entire verse perfectly that releases God’s power, but faith in His Word and His love for you. And one word from Him is enough to send your enemies scurrying away.

However, if you know God’s Word by heart but refuse to proclaim it, the power of His Word cannot be released. The Bible does not say that angels heed His Word. No, it says that “His angels, who excel in strength, who do His word, heeding the voice of His word”. So beloved, give voice to God’s Word and see His angels respond. His angels are activated for your benefit when you speak His Word!
Mama Matechi upoooo. Naamini nitakuwa nimeukonga Moyo wako Mambo ya Joseph Prince yamo ndani ya blog sasa furahia mama yangu. Mungu akujaze maisha marefu.

MWALIKO NO 3. YOU ARE INVITATED

The Brooklyn Tabernacle.
 Family Ministries Presents:
Academic Excellence Helping Your Child Succeed in School
What every parent should know!

This seminar will provide information and re-sources designed to assist families in becom-ing proactive in their child’s education.
It will offer suggestions and practical informa-tion parents can use to more effectively:
Collaborate with School Officials to improve their child’s education.

Topic: Are You a Team Player?
The School/Parent Team
Incorporate techniques used by teachers to enhance their child’s learning experience.

Topic: The Teacher’s Learning Secrets
Know their child’s personality type in order to help them succeed in school.

Topic: Personality Types in Children
cbad 

Registration Required

Locations:
Fulton Street Lobby – after 9:00am, 12:00pm, and 3:00pm services

Resource Table - 180 Livingston Street

Email: Familyministries@brooklyntabernacle.org

Phone: 718-290-2013

All Seats Free
For more information call Family Ministries. 718-290-2070

Date:
Friday September 24, 2010
Time:
6:30pm—9:30pm
Location:
180 Livingston Street
For more information call Family Ministries. 718-290-2070

Monday, September 20, 2010

NENO

Sheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa; Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, kwa maana ninayo sikuzote. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo, Ninao ufahamu kuliko wazee kwa kuwa nimeyashika mausia yako. Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya ili nitii NENO lako. Sikujiepusha na hukumu zako kwa maana wewe mwenyewe umenifundisha. Mausia yako ni matamu sana kwangu, kupita asali kinywani mwangu. Kwa mausia yako najipatia ufahamu. Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
Oh, how i love your law! i mediatate o it all the day long, Your commands make me wiser than my enemies for they are ever with me. I have more insight than all my teachers for i meditate on your statutes. I have more understanding than the elders for i obey your precepts. I have kept my feet from every evil path so that i might obey your word. I have not departed from your laws for you yourself have taught me. How sweet are your words to my taste; sweeter than honey to my mouth. I gain understanding from your precepts therefore, i hate every wrong path.
Zidi kubarikiwa

Wednesday, September 15, 2010

MSEMO MSEMO NO. 3

Baadhi ya watu husemaaa"Kuokoka ni ushamba, ukiokoka ina maana unayo matatizo, umefulia hauna jipya" je hii ni kweli?
Laiti watu wa namna hii wangemjua Mungu wangejua furaha na uzuri wa kuokoka wasingesema hivyo. Bibilia inasema Dunia na vyote vijazavyo ni mali ya Bwana Dhahabu fedha nk ni mali yake Baba yetu sasa je iweje mtuite tuliofulia? sisi walokole tumejaa amani, tuna furaka ya kweli kutoka ndani ya moyo. Maisha yetu yana msimamo na mafanikio yetu yanaanzia ndani kwenda nje, tumebarikiwa ktk kila nyaja. Sisi ni watoto wa mfalme tangu lini prince au princess akawa amepauka / amefulia? jamani lazima alivyonavyo baba na sisi pia tunavyo na chochote tukitakacho twakipata tukimwomba baba anatupa bila hiyana na vingine hata tusipoomba anatupatia yeye mwenyewe kadri apendavyo. Njoo uonje uzuri wa kuokoka hakika hautajuta.

MWALIKO ! MWALIKO! NO. 2

Brooklyn Terbanacle Tuesday Prayer is very powerful kindly passby when you have time.
Unakaribishwa sana kwenye maombi ya kila Jumanne katika kanisa la Brookyn Terbanacle. Watu wanaokolewa, wanapata uponyaji na faraja kubwa katika maombi ya kila jumanne kanisani Brookyn. Hivyo mtumishi wa Mungu mpakwa mafuta wa Bwana anakualika wewe na mwingine kuhudhuria siku hii ya maombi usikose.
Pata muda wa kuongea na Mungu wako kwa njia ya maombi. KARIBU SANA

Tuesday, September 14, 2010

MWALIKO! MWALIKO! MWALIKO!

KANISA LA LIVING WATER - GONGO LA MBOTO LINAWAKARIBISHA WATU WOTE KWENYE IBADA YA JUMAPILI KANISANI GONGO LA MBOTO KUANZIA SAA TATU KAMILI ASUBUHI HADI SAA NANE MCHANA; KUTANA NA MTUMISHI WA MUNGU MPAKWA MAFUTA WA BWANA AMBAYE AMEKUBALI KUTUMIKA NA ROHO WA MUNGU ANAMTUMIA UKAPATE KUBARIKIWA NA KUFUNGULIWA MCHUNGAJI MARY MAGOLO
PIA
KANISA LA LIVING WATER CENTER MAKUTI -KAWE LINAKUKARIBISHA KWENYE IBADA YA JUMAPILI HII KUANZIA SAA TATU ASUBUHI HADI SAA NANE MCHANA KUTANA NA WATUMISHI WA MUNGU WENYE UPAKO WA KWELI NA WAPAKWA MAFUTA WA BWANA APOSTLE ONESMO NDEGI NA MWALIMU LILIAN NDEGI UKAPATE KUIJUA KWELI NA HIYO KWELI IKUWEKE HURU.
WOTE MNAKARIBISHWA SANA.
PATA KUIJUA NGUVU YA NENO NDANI YA MAISHA YAKO !!!!

Monday, September 13, 2010

MAOMBI YALIYOAMBATANA NA SHUKRANI

Muombapo aminini yamekuwa nayo yatatendeka. Tunapopeleka maombi yetu (haja zetu) mbele za Bwana Biblia inasema tuamini kuwa tayari maombi hayo tuliyoomba yameshajibiwa nayo yatakuwa hivyo. Baada ya hapo ni shukrani mbele za Mungu. Kumshukuru Mungu kwa maombi tuliyopeleka mbele zake ni jambo la msingi kwani linafanya hata yale ambayo hatukumwomba Baba kwa kinywa chetu yafunguliwe. Si vyema kila wakati kuomba maombi ya kupeleka haja zetu kwa Mungu. Tunatakiwa wakati mwingine tuingie kwenye maombi ya kusifu na kushukuru tu kwani yana nguvu kweli kweli mpendwa ukijua siri yake. Tukitangaza matendo makuu ya bwana na jinsi alivyo mwema na jinsi alivyomwaminifu, alivyo mkuu na ya kwamba hakuna Mungu mwingine ila yeye peke yake. Ingia kwenye maombi haya mpendwa bila kupeleka haja zako kwake nawe uone jinsi anavyoweza kukutendea mambo makubwa ambayo hata hukudhania.
MAOMBI YA SHUKRANI YANA NGUVU. Barikiwa.

Sunday, September 12, 2010

TUMSHUKURU MUNGU

Ni jambo jema kumshukuru Mungu kila wakati kila saa kila siku katika maisha yetu na kumwinua kwa matendo yake makuu anayotutendea siku hadi siku. Si jambo la hekima/ busara kusubiri Mungu akufanikishe katika jambo fulani au akunusuru kwenye hatari ndio UMSHUKURU, bali tunatakiwa kumshukuru KILA WAKATI hata kwa pumzi tunayovuta kwani vyote vya toka kwake. Tumshukuru hata kwa kuwepo hadi siku hii ya leo kwani ni wengi walitamani kuiona siku hii ya leo lakini hawakuiona (wamekufa) na wengine ni wagonjwa wamelazwa mahospitalini wanaumwa walitamani wangekuwa wazima wenye afya lakini si hivyo kwao (wako vitandani hawajiwezi) lakini wewe na mimi leo hii ni wazima wa afya tuna nguvu, tunatembea, tunachakula je tumekumbuka kumshukuru Mungu wetu? Kusema kweli tunawiwa kumshukuru Mungu kwa kila jambo.  Hata kama tunapitia mambo magumu kiasi gani bado tumshukuru kwani ni kusudi lake wakati mwingine kupatwa na hayo ili aweze kutuvusha kutoka hapo tulipo kwenda sehemu nyingine ktkt ulimwengu wa Roho. Huwezi kujua labda anataka kuona imani yako ni kubwa kiasi gani je unamwamini kwa kiwango kipi? (Japo Biblia inatuambia kuwa Mungu hamjaribu mtu bali mtu hujaribiwa na tamaa zake mwenyewe). Pia wakati mwingine Mungu anataka umtegemee yeye yawezekana umekuwa ukitegemea akili zako zaidi kuliko kumtegemea Mungu. Hivyo basi;
TUWE WATU WA SHUKRANI MBELE ZA BWANA KILA WAKATI. KWANI MUNGU ANAJUA MWISHO WETU TANGU MWANZO. Uwe na wakati mzuri na ubarikiwe.

Friday, September 10, 2010

MSEMO! MSEMO ! MSEMO NO. 2

(Kwa nini Wanuna? / Raha jipe mwenyewe)
(KWA YESU HAKUNA KUNUNA KUNA RAHA YA AJABU HEBU MKARIBISHE KWENYE MAISHA YAKO UONJE RAHA YAKE. WAKATI WOTE NI FURAHA, AMANI UPENDO KICHEKO KAZI YETU NI KUUNGANA NA MASERAFI NA MAKERUBI, WAZEE 24 NA WENYE UHAI WANNE TUNASIFU NA KUIMBA MTAKATIFU! MTAKATIFU! MTAKATIFU HAKUNA KUCHOKA HAKUNA KULALA TUMEJAA NGUVU TUNA AMANI TUNAYE BABA MWENYE UWEZA WOTE kwa nini tununeeeeeeeee tunacheza tu tunarusha taji tunadaka tunaima tunainuka usiku na mchana kazi yetu moja kusiffuuuuu wajua siri ya kusifuuu. YESU NI BWANA

MSEMO, MSEMO, MSEMOOOOO NO:1

(Waswahili wanasema Mpende Akupendaye Asiyekupenda Achana Naye) Lakini Biblia inasemaaaa MPENDE AKUPENDAYE, MPENDE ASIYEKUPENDA MPENDE, ADUI YAKO TENA KAMA UNAVYOJIPENDA WEWE. Mpendwa umeikubali hiiiiiiiii
JAMANI KWA YESU KUNA RAHAAAAAAAAAAAAA; TUDUMISHE UPENDO

MISEMO

NDUGU ZANGU WAPENZI KATIKA BWANA NAWASALIMU HABARI ZETU, BWANA APEWE SIFA. NILIWAAHIDI KUWA NITAWAPA MISEMO,JE WAJUAAAA? (mambo ambayo hukuwahi kusikia hapo kwanza au ndio mara ya kwanza kusikia kuhusu Biblia) VIONJO NA MANJONJO MENGINE KIBAO KUTOKA KWENYE BIBLIA YETU. NENO LA MUNGU LINAUTOSHELEVU WOTE HAKUNA KITU KIMEACHWA BWANA TENA KATIKA ULIMWENGU WETU HUU TUNAOISHI LINAFANYA KAZI. KARIBU MTUMIE NA MWENZIO

UPENDO WA KWELI

Bwana Yesu Apewe Sifa! Namshukuru Mungu sana kwa wema na fadhili zake anazonitendea siku hadi siku, nimeuona wema, uweza na upendo wake kwangu kila iitwapo leo. Nalitukuza jina lake na kumwinua maana hakika anastahili kuinuliwa, kupewa sifa na hata kusujudiwa. Tumwamini maana yeye ni mwaminifu na ahadi zake ni kweli. Soma Warumi 4:20-21
Upendo wa KINDUGU (UPENDO WA AGAPE) Jamani tuwe na pendo/ penzi la kweli sisi tulio waaminio. Tupendane sisi kwa sisi kama Mungu alivyotupenda hata akamtoa MWANA WAKE WA PEKEE YESU AFE msalabani kwa ajili ya dhambi zangu mimi na wewe. Soma Warumi 5:8 Mungu ametupenda upeo jamani haijalishi umefanya dhambi kiasi gani, haijalishi umemkosea mara ngapi, haijalishi kama umeokoka ukakengeuka ukarudi nyuma , haijalishi umeokoka au haujaokoka bado ANAKUPENDA tena kupitiliza UPEO!! (anasema nawanyeshea mvua wema na waovu) Mbona na sisi tusipendane? Kwa maana tumeshaunganishwa na kuwa wandugu kupitia mwana wake Yesu Kristo. Tena tunaitwa watoto wa Mungu? soma Warumi 8:16 tumebeba sura na mfano wake yeye aliyetuumba, je tabia zake tunazo au tumeziacha wapi wapendwa kwa maana tabia ya Mungu ni ya Upendo na anataka TUPENDANE na amri Kuu Yesu aliyotuachia ni UPENDO. Kwanini tusipendane basi, tusiwe wamoja tusilie nao waliao na tucheke na wachekao? kwa nini tuwe wanafiki? kwa nini hatufurahishwi na mwenzetu akipata mafanikio au hata anapobarikiwa? Kwa nini uwe na upendo na mtu kwa vile unapata kitu fulani kutoka kwake kama hakuna basi huna time naye? Wivu wa nini? wakati sisi wote ni wana wa Mfalme tena Mfalme wa Wafalme.
Nasema hivii Wivu hauna nafasi tena katika jina la Yesu, Upendo wa kinafki naukataa katika jina la Yesu, Roho ya korosho ndio naifunga na kazi zake zote ktk Jina la Yesu, husuda naifunga nakuitupa kuzimu katika jina la Yesu Kristo aliye hai. Nakataa Roho zote hizo zinazofanya wana wa Mungu  tusipendane. Nafunga mipango yote na hila alizopanga mwovu shetani kwa ajili ya wana wa Mungu wasiwe na Upendo. Naambukiza Upendo wa kweli wa AGAPE utokao kwa Baba na Bwana wetu Yesu Kristo. Amen Amen.
Biblia inasema kuwa Mungu alitupenda upeo yaani alitupenda kupitiliza hakuna ukomo ktk penzi lake kwani yeye ni Mungu wa Upendo hata tunapokuwa kwenye upendo huu tunaweza kubomoa na kuangusha kuta zilizotuzingira. Kwenye UPENDO basi amani, furaha, ujasiri, neema lazima vipo na sehemu hiyo ujue kuwa Utukufu wa Mungu upo, Yesu yupo na Roho Mt yupo na yule mshitaki wetu shetani hana nafasi mahali hapa kabisaaaa.
Kama wewe unasema kuwa umeokoka na hauna Upendo basi ujue unajidanganya bado haujaokoka kwani hata Bibilia inakukataa kuwa wewe si wa Mungu Soma 1Yohana 4:8; 1Yohana 4: 16b. Ndugu yetu Petro anasema kuwa "Tuwe na juhudi nyingi ktk KUPENDANA kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi" Soma 1Petro 4:8 ina maana kwamba ukiwa na upendo wa kweli hutaweza kumbagua mwenzako kwa kuangalia sura, mavazi, fedha, mali nk wala kumdharau bali utampenda kama jinsi alivyo hutakuwa na kijicho pembe kwa mafanikio yake ya Kiroho na ya kimwili pia, bali utafurahi naye na kuhuzunika naye pale apatwapo na msiba (siyo kifo msiba lina maana mbili)
"KILA AMCHUKIAYE NDUGU YAKE NI MWUAJI, na mnajua kuwa KILA MWUAJI HANA UZIMA WA MILELE. TUSIPENDE KWA NENO, WALA ULIMI BALI KWA TENDO NA KWELI" Haya si maneno yangu bali yatoka kwenye Bibilia. Kwenye upendo jamani Hofu haina nafasi Paul anasema hivii "KATIKA PENDO HAKUNA HOFU, LAKINI PENDO LILILOKAMILI HULITUPILIA NJE HOFU, KWA MAANA HOFU INA ADHABU, NA MWENYE HOFU HAKUKAMILISHWA KATIKA PENDO" haya kama una hofu ikatae haraka sana ktk JINA LA YESU. Upendo utokao kumoyo wapendwa ambayo ndiyo tabia ya baba yetu. (kama mataifa wanaweza kumpenda mtu jinsi alivyo iweje sisi tuliopata neema ya uokovu tushindwe???? ( NANUKUU WIMBO WA DUDU BAYA "Nakupenda tu vile ulivyo nakupenda tu PUA KAMA ANDAZI NAKUPENDA TU ) sisi je haitupasi kuwa na UPENDO WA KWELI!!!!! kwenye Upendo pia kuna Umoja wapendwa na kwenye Umoja kuna nguvu ya ajabu ambayo Mungu anaiachilia, na yeye mwenyewe hushuka watu wakiwa na umoja na wakishikana SOMA 2M/Nyakati 5:13-14 "quote walipokuwa kama mmoja " (sehemu nyingine Mungu pia anaogopa Umoja jamani ndio maana hata wanadamu walipodhamiria kwa umoja kutaka kujenga Mnara wa Babel aliwatawanya kwa kuwapa lugha tofauti sababu ya nini NGUVU ILIPYOPO KWENYE UMOJA na umoja wa kweli hutoka kwenye "UPENDO WA KWELI. Tupendane sisi kwa sisi, upendo wa Agape, Upendo ambao Yesu alituachia kama AMRI KUU YA KUPENDANA. Kwani tukipendana tutashikana, tutashirikiana tutakuwa mamoja na kunena lugha moja na kumpenda Mungu kwa kulisoma NENO lake na kutenda huu ndio UPENDO autakao kwetu. UPENDO! UPENDO! UPENDO nitaendelea siku nyingine huu ni utangulizi somo lipo kuuubwa!bado hata sijaanza subiri uhondo misemo ya kwenye biblia na mistari ya kukufundisha.
SOMA 1Yohana wa Kwanza, wa Pili na Tatu Yote Kwa habari ya Upendo. Kuhusu ujenzi wa mnara (Babeli) soma Mwanzo 11:1-9

Wednesday, September 8, 2010

BACK TO SCHOOL PRAYER

BWANA APEWE SIFA WAPENDWA. Jana tarehe 7/9 tulikuwa na maombi ya kuwaombea watoto wetu wanaorudi mashuleni / vyuoni hata wazazi pia wanaosoma nao walipata kibali mbele za bwana na Mtumishi wa Mungu akawaombea. Maombi yalianzia umri 0 - wanaochukua PHD wote walikuwepo pale Brooklyn Tabernacle Church  (Brooklyn- New York). Namshukuru Mungu sana kwani na mimi nilipata kibali cha kuwepo  kwa ajili ya kuwaombea watoto wangu walioko TZ ambao nao siku ya leo ndio walikuwa wanafungua shule na ndio mwaka mwingine wa masomo kwao wameingia darasa jipya pia na watoto wa dada yangu walioko huku USA. Kusema kweli sisi wana wa Mungu (wazazi) tunahitaji sana kuwaweka watoto wetu mikononi mwa Mungu kwani huko mashuleni wanakumbana na vikwazo mbalimbali na sisi kama wazazi hatuwezi kwenda nao shule ili tuweze kuwasaidia hapa ni mtoto peke yake na Mungu wake. Mtoto anakutana na watoto wengine ambao wamelelewa katika mazingira tofauti na ya nyumbani kwao, wenye tabia tofauti na ambao wenye kumjua Mungu na ambao hata hawajawahi kusikia kitu kama hicho. Hivyo bila msaada wa Mungu kwa kweli sisi wenyewe wazazi hatuwezi, hatuna uwezo wa kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja lakini yupo mwenye uwezo huo na zaidi. Kwa kweli watoto wetu wa karne hii wametuzidi sana maujanja wazazi wana mambo mengi na makubwa kuliko hata ya bibi zao ambao wameishi miaka mingi na kukumbana na mambo mengi. Utakuta mtoto wa shule ya msingi hata kwa mganga wa kienyeji anakwenda (anafuata nini? zaidi sana ni kuwaloga wenzao ktk masomo na kuwaloga hao wanaowaita mabuzi upo!) na wengine wanakwenda huko kwa waganga hadi wamekuwa wachawi yaani wanajua  na kufanya mambo mengi ambayo sisi wazazi wao hata hatukufikiria  wala hatufikirii kuyafanya au hata kutaka kuyajua. Je ni nani atakayeweza kuwaoko watoto wetu na kuwaponya na mkono wa yule adui shetani kama sisi wazazi hatutawasimamia jamani na kuwaombea na kuomba muongozo wa Roho Mtakatifu katika kuwalea na kuwakabidhi kwake. Tutafakari jambo hili wapendwa tuone umuhimu wa kuwaombea watoto wetu sana haijalishi ni mdogo kiumri kwa kiasi gani bado shetani anaweza kumtumia vile vile. Usijidangaye kuwa mtoto bado ni mdogo hajui hili wala lile lakini shetani anaona kuwa hicho ndicho chombo kizuri anachoweza kukitumia ili kukufadhaisha na kukutumia wewe kuwa mtumwa wake kama apendavyo. Mfano unakuwa na mtoto ambaye anasumbuliwa na magonjwa mara kwa mara kila leo wewe uko hospitali unasali sana mama / baba wa watu lakini bado tatizo liko pale pale kumbe bado mtoto wako haujamkabidhi mikono mwa Bwana na kumwombea kila atokapo na aingiapo. Unapomwacha nyumbani na mtu mwigine hujui ana maroho gani kwani sisi wanadamu hatuwezi kuona kwa kuangalia sura bali Mungu yeye ndiye aonaye mioyo yetu wanadamu na kujua ni yupi aliye mwema na aliye mwovu. Hivyo hata wale tunaowaacha wawe waangalizi wa watoto wetu tunatakiwa kuwaombea na kuomba Roho Mtakatifu awaongoze katika kumjua Mungu kama bado hawajamjua kama tayari katika kuwa wa kweli na wawazi mbele za Bwana kwani wao ndio wanaokaa na watoto wetu kwa muda mwingi wanaweza kupandikiza kitu kisichofaa kwa watoto wetu bila sisi kugundua tunabaki kuwakandamiza watoto kwa kuwaona wanatabia zisizofaa. Biblia inatuambia kuwa "Lakini katika mambo hayo yote tutashinda na zaidi ya kushinda kwake yeye aliyetupenda"Warumi 8:37 Hivyo basi cha msingi ni tuyaache yote madhabahuni tusijitwike mizigo ambayo hatuwezi kuibeba Bwana Yesu anatuambia kuwa tumpatie mizigo yetu iliyo mizito na yeye atupe wa kwake ambao ni mwepesi kwa nini ulemewe na yupo aliyejitolea kukusaidia? Mkabidhi Roho Mtakatifu mambo yako yote na ukubali akutumie nawe upate kuona furaha ya kweli kuwa ndani ya Kristo naye atakupasha hata mambo yajayo ndani ya maisha yako na ya watoto wako. Yoh.16:13. pia Tunaambiwaaaa "Onjeni mwone ya kuwa Bwana yuu Mwema"

SHUKRANI

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wale wote walioniandikia e-mail kunitia MOYO na hata kuleta maombi yao kwangu nawashukuru sana. Kusema kweli  MAOMBI YOTE nitayafanyia kazi na naamini Mungu wangu ninayemtumainia atawajibu kila mtu hitaji la MOYO wake, wenye magonjwa hakika mtaponywa na hakuna kulemewa tena na mizigo. Wengi mmeomba nisipublish maombi yenu nami naahidi kutokufanya hivyo (yote mliyoandika ni siri), japo kwa wale ambao watakubali kutoa ushuhuda wanakaribishwa kwa sababu unapotoa ushuhuda unamwaibisha shetani na vile vile unamfungua na mwingine ambaye alikuwa anatatizo kama lako naye anapata kufunguliwa katika vifungo mbalimbali walivyofungwa. (majina hayatatajwa hivyo usiwe na hofu). Nitakuwa natoa mistari ya Biblia ya kusoma kila siku vile vile kwa wale tunaowasiliana kwa njia ya e-mail nitakupatia kulingana na hitaji lako.

Tusikate tamaa kwani tumaini la Bwana lipo na hakuna lisilowezekana na lisilo na jawabu chini ya jua hili yote yawezekana kwake yeye yule aaminie. HAKIKA UTASHINDA KWANI HAKUNA JARIBU LISILOKUWA NA MLANGO WA KUTOKEA. BARIKIWA  SANA NA BWANA.

Saturday, September 4, 2010

MAPINDUZI YA BINTI WA LEO

Hiki ni kizazi kinachopitia mambo mengi katika ulimwengu huu wa sasa. Misukosuko katika kila kona ya maisha ni kama wamesahaulika na hawana msaada kabisa, hawana Imani na mtu yeyote wamekosa tumaini. Wengine hata wameanza kuzeeka kabla hata ya muda wao kwa sababu ya mizigo mizito waliyobeba uchungu, hofu, mawazo wanaona kama dunia yote ni giza, wameshapatwa na misukosuko mingi kuliko hata sisi wazazi wao tulioishi miaka mingi zaidi yao. Je sisi wazazi tunasemaje kuhusu mabinti zetu? tunakaa na kuongea nao kweli au ndio tunawarushia maneno mabaya kila siku? Tujue kuwa sisi wazazi ndio tunaowapa watoto wetu baraka au laana. Je ulishawahi kama mzazi kumbariki mwanao? au binti yako akishavunja ungo tu basi mnaanza mashindano na kuanza kuwawazia mawazo (mambo) mabaya. Ulishachukua muda ukaongea naye ukajua kuwa ni yapi yanayomsibu awapo nyumbani wakati wewe haupo, awapo shuleni, awapo njiani kwenda sehemu yeyote? Umewahi kujua Binti yako anawaza nini katika akili yake. Umewahi kumpa nafasi ya kusema jambo ukalisikiliza na kulipa kipaumbele. Maana jamani dunia ya leo si kama ya miaka ile sisi wengine tulivyolelewa, ambapo binti / kijana/ mtoto analelewa na Bibi na Babu, Shangazi na Mjomba, Jirani na hata mpita njia tu. Dunia ya sasa watoto wanajilea wenyewe na sisi wazazi wao tupo. Wanadamu tumekuwa wabaya kuliko hata simba jike mwenye watoto na halafu ana njaa. Hakuna baba, wala mama, wala kijana, si mjomba si shangazi kila mtu amekuwa simba jike. Je umeshafikiria mtoto wako anaishije? vikwazo gani anavyokumbana navyo. Tuamke jamani wazazi wenzangu kwa akili zetu wenyewe hatuwezi,  kwa mali tulizonazo bado na fedha bado si cho chote hatuwezi kulea watoto wetu vyema katika ulimwengu huu wa sasa tunahitaji msaada wa mwenye uweza na nguvu kutushinda sisi wanadamu na ni Mungu pekee ndio jibu na kimbilio letu ambaye anao uweza wa kutuwezesha kuwalinda na kuwalea watoto wetu.
TUBADILIKE WAZAZI WENZANGU.
Binti usivunjike moyo bado tumaini lipo bado nafasi unayo kwa yote uliyopitia bado liko penzi la kweli bado unaweza kuanza mwanzo mpya wenye mafanikio. Haijalishi wewe ni mfanyakazi wa ndani , haijalishi wewe ni yatima, haijalishi wewe umekimbia nyumbani nasema tena tumaini bado lipo. UNAHITAJI MAOMBI EWE BINTI EWE MZAZI, USHAURI n.k karibu sana nipo tayari kukuombea usiwe na wasiwasi kwa muda wote masaa 24 tuma maombi yako kwenye e-mail yangu nipo na wamama wengine waliojaa nguvu watakuombea pia.
USIKATE TAMAA BADO TUMAINI LIPO KARIBU SANA NA MUNGU WANGU AZIDI KUKUTIA MOYO NA KUKUBARIKI.

Friday, September 3, 2010

VAZI LIPI LAFAA HASA KWENDEA KANISANI? TUELIMISHANE

Wapendwa jamani hili ni jambo ambalo linawasumbua sana watu wengi na wengine hata wanadiriki kutokwenda kanisani siku nyingine sababu kubwa sina nguo ya kuvaa. Naomba tusaidiane tuelimishana kuhusu hili kwa sababu mimi ninaamini kuwa Mungu wetu haangalii mavazi  umbo, utajiri wala chohote kiwayo chote ila yeye anaangalia MOYO wako. 1Samweli 16:7

Sasa je ni vyema kwa waumini kumnyooshea kidole mtu aliyevaa nguo fupi au suruali au jeans akaenda nayo kanisani? (naongelea kwa mwanamke) Mfano kama nimeokoka nikivaa jeans kanisani au nguo fupi na (kijana wa kiume) akavaa suruali chini ya makalio inamaanisha kuwa mimi sijaokoka? Unawezaje basi kutambua kuwa mimi nimeokoka au la kwa kuangalia mavazi yangu? Au kama hata sijaokoka mimi ni muumini wa kawaida napenda kwenda kanisani napenda kujifunza kuhusu neno la Mungu je utanitenga na kuanza kunisengenya kuniangalia jicho pembe kuwa mimi sifai kuingia kanisani kwa kungalia uvaaji wangu? Je Yesu alikuja kutafuta walio watakatifu tu au wenye dhambi? Si vyema mimi nije kama nilivyo ili niweze kupata badiliko la kweli? Je si Roho Mtakatifu pia aamuaye ndani ya mioyo yetu namna ya kuwa Mtakatifu nadhani akiwa ndani yako atakuonyesha jinsi ya kuvaa au mwasemaje wapendwa?
Naomba tusaidiane kuchangia hii mada ili tujifunze na tuelimishane kusudi tupate kupona. Pia kama unazo picha za kuonyesha vazi la kwendea kanisani tafadhali naomba unipostie ili tubadilike. Barikiwa na Bwana

MAOMBI YANGU KWAKO SIKU HII YA LEO

Bwana Mungu wetu Mfalme wa Amani, ninakutukuza ninakupa heshima na utukufu. Asante kwa kuwa mwema kwetu na uaminifu wako ndani ya maisha yetu.Asante kwa kutupa kibali katika siku hii nzuri na njema ya leo. Wabariki wana wako baba panda kitu kipya ndani ya maisha yao siku hii ya leo. Bariki kazi za mikono yao, wabariki kila waingiapo na watokapo, chochote watakachofanya au kugusa kwa siku hii ya leo kiwe kimebarikiwa. Waepushe na kila hila za yule mwovu na kazi zake, waondolee magonjwa, hofu, huzuni, kukosa amani, uchungu. Wape furaha ya kweli, amani itokayo kwako, tabasamu la kweli kutoka ndani ya mioyo yao, panda ujasiri wako ndani yao. Roho Mtakatifu wape hekima itokayo kwako, maarifa  na ufahamu wako. Linda familia, watoto na ndoa zao. Nashukuru baba kwa maana maombi haya yamepata kibali machoni pako katika jina la mwanao mpendwa Yesu Kristo. Amen, Amen, Amen.

I SAID MY PRAYER FOR YOU TODAY

I said my prayer for you today and i know God must have heard; I felt the answer in my heart although he spoke not a word. I didn't ask for wealth or fame ( i knew you wouldn't mind) I asked for priceless treasures rare of a more lasting kind. I prayed that he'd be near to you and protects you at the start of each new day.
To grant you health and blessings fair and friends to share your way. I asked for happiness for you in all things great and small, but that you'd know his LOVING, CARE.
I PRAYED THE MOST OF ALL. HAVE A BLESSED DAY.