Ni jambo jema kumshukuru Mungu kila wakati kila saa kila siku katika maisha yetu na kumwinua kwa matendo yake makuu anayotutendea siku hadi siku. Si jambo la hekima/ busara kusubiri Mungu akufanikishe katika jambo fulani au akunusuru kwenye hatari ndio UMSHUKURU, bali tunatakiwa kumshukuru KILA WAKATI hata kwa pumzi tunayovuta kwani vyote vya toka kwake. Tumshukuru hata kwa kuwepo hadi siku hii ya leo kwani ni wengi walitamani kuiona siku hii ya leo lakini hawakuiona (wamekufa) na wengine ni wagonjwa wamelazwa mahospitalini wanaumwa walitamani wangekuwa wazima wenye afya lakini si hivyo kwao (wako vitandani hawajiwezi) lakini wewe na mimi leo hii ni wazima wa afya tuna nguvu, tunatembea, tunachakula je tumekumbuka kumshukuru Mungu wetu? Kusema kweli tunawiwa kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Hata kama tunapitia mambo magumu kiasi gani bado tumshukuru kwani ni kusudi lake wakati mwingine kupatwa na hayo ili aweze kutuvusha kutoka hapo tulipo kwenda sehemu nyingine ktkt ulimwengu wa Roho. Huwezi kujua labda anataka kuona imani yako ni kubwa kiasi gani je unamwamini kwa kiwango kipi? (Japo Biblia inatuambia kuwa Mungu hamjaribu mtu bali mtu hujaribiwa na tamaa zake mwenyewe). Pia wakati mwingine Mungu anataka umtegemee yeye yawezekana umekuwa ukitegemea akili zako zaidi kuliko kumtegemea Mungu. Hivyo basi;
TUWE WATU WA SHUKRANI MBELE ZA BWANA KILA WAKATI. KWANI MUNGU ANAJUA MWISHO WETU TANGU MWANZO. Uwe na wakati mzuri na ubarikiwe.