Namshukuru Mungu sana kwa kunipa mafunuo ya kuanzisha hii Blog kwani toka nianzishe nimeona jinsi Mungu anavyotenda ndani ya maisha yangu na pia kunipa kibali mbele za watu kwani nimefanikiwa kukutana na watu kupitia blog hii ambao hapo kabla nilikuwa siwafahamu na kujua kuwa bado kuna watu wana kiu ya kumjua Mungu sana na wengi wako kwenye vifungo.
Nimepata email kadha wa kadha za watu kuomba maombi nami nimefanya hivyo kwa uweza wa Roho mtakatifu na usaidizi wake. Lakini hivi karibuni nimepata maombi ya kipekee kutoka katika nchi moja huko Africa. Huyu ni mtumishi wa Mungu ambaye analo kanisa lake lenye watu thelathini, yeye badala ya kuomba maombi aliomba asaidiwe Biblia kwa ajili yake yenye Maandishi makubwa ili aweze kuwafundisha vizuri waumini wake, kwani anasema kutokana na umri alio nao kwa maana ni mtu mzima macho yake hayaoni vizuri. Nami kwa msaada wa Mungu naamini ni kwa kibali chake kumwelekeza huyu mtumishi kwangu hivyo imenipasa kufanya hivyo na zaidi. Namshukuru Mungu kwa hili kwani siku zote nilikuwa namwomba Mungu anitumie mimi kama chombo chake sasa naamini kuwa nimefanyika chombo kwa Bwana kwa watu kupata neno lake ambalo ni muhimu katika maisha yetu sisi sote na naamini litawafungua wengi katika vifungo.
Namshukuru Mungu kwa ajili ya hili kwani naamini hizi Biblia zitawaokoa wengi ambao watalisikia neno akiwahubiria huyu mtumishi nami nitakuwa nimeishi andiko katika Yohana 15:1-2
Bwana Yesu Apewe Sifa sana sana sana. Tuzidi kupendana na Amani ya Kristo itawale mioyoni mwetu. Amen amen.