neno la uzima |
Nahumu 1:2-9
Bwana ni Mungu mwenye Wivu, naye hujilipiza kisasi. Bwana hujilipiza kisasi naye ni mwingi wa hasira; Bwana hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya Hasira.
Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi wala hatamwesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe, Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake. Yeye huikemea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote.
Mstari 5 unasema hivi, Milima hutetemeka mbele zake, navyo vilima huyeyuka, nayo dunia huinuka mbele ya uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake. Ni nani awezeye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye. Bwana ni mwema ni ngome siku ya taabu, naye huwajua hao wamkimbiliao. Lakini kwa gharika ifurikayo atapakomesha kabisa mahali pake, na kuwafuatilia adui zake hata gizani.
Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa mateso hayatainuka mara ya pili.