Monday, September 13, 2010

MAOMBI YALIYOAMBATANA NA SHUKRANI

Muombapo aminini yamekuwa nayo yatatendeka. Tunapopeleka maombi yetu (haja zetu) mbele za Bwana Biblia inasema tuamini kuwa tayari maombi hayo tuliyoomba yameshajibiwa nayo yatakuwa hivyo. Baada ya hapo ni shukrani mbele za Mungu. Kumshukuru Mungu kwa maombi tuliyopeleka mbele zake ni jambo la msingi kwani linafanya hata yale ambayo hatukumwomba Baba kwa kinywa chetu yafunguliwe. Si vyema kila wakati kuomba maombi ya kupeleka haja zetu kwa Mungu. Tunatakiwa wakati mwingine tuingie kwenye maombi ya kusifu na kushukuru tu kwani yana nguvu kweli kweli mpendwa ukijua siri yake. Tukitangaza matendo makuu ya bwana na jinsi alivyo mwema na jinsi alivyomwaminifu, alivyo mkuu na ya kwamba hakuna Mungu mwingine ila yeye peke yake. Ingia kwenye maombi haya mpendwa bila kupeleka haja zako kwake nawe uone jinsi anavyoweza kukutendea mambo makubwa ambayo hata hukudhania.
MAOMBI YA SHUKRANI YANA NGUVU. Barikiwa.