Wednesday, September 15, 2010

MSEMO MSEMO NO. 3

Baadhi ya watu husemaaa"Kuokoka ni ushamba, ukiokoka ina maana unayo matatizo, umefulia hauna jipya" je hii ni kweli?
Laiti watu wa namna hii wangemjua Mungu wangejua furaha na uzuri wa kuokoka wasingesema hivyo. Bibilia inasema Dunia na vyote vijazavyo ni mali ya Bwana Dhahabu fedha nk ni mali yake Baba yetu sasa je iweje mtuite tuliofulia? sisi walokole tumejaa amani, tuna furaka ya kweli kutoka ndani ya moyo. Maisha yetu yana msimamo na mafanikio yetu yanaanzia ndani kwenda nje, tumebarikiwa ktk kila nyaja. Sisi ni watoto wa mfalme tangu lini prince au princess akawa amepauka / amefulia? jamani lazima alivyonavyo baba na sisi pia tunavyo na chochote tukitakacho twakipata tukimwomba baba anatupa bila hiyana na vingine hata tusipoomba anatupatia yeye mwenyewe kadri apendavyo. Njoo uonje uzuri wa kuokoka hakika hautajuta.

MWALIKO ! MWALIKO! NO. 2

Brooklyn Terbanacle Tuesday Prayer is very powerful kindly passby when you have time.
Unakaribishwa sana kwenye maombi ya kila Jumanne katika kanisa la Brookyn Terbanacle. Watu wanaokolewa, wanapata uponyaji na faraja kubwa katika maombi ya kila jumanne kanisani Brookyn. Hivyo mtumishi wa Mungu mpakwa mafuta wa Bwana anakualika wewe na mwingine kuhudhuria siku hii ya maombi usikose.
Pata muda wa kuongea na Mungu wako kwa njia ya maombi. KARIBU SANA