Je waifahamu Living Water Centre Ministry iliyopo Kawe Dar Es Salaam.
Kutana na watumishi wa Mungu wapakwa mafuta wa Bwana ambao Roho Mtakatifu anawatumia kweli kweli. Kwa habari zaidi mafundisho sahihi ya neno la Mungu maombi na maombezi basi fika kanisani LWC upate kubarikiwa, kufunguliwa na upate kuijua kweli na hiyo kweli ikuweke huru.
Ibada ya Jumapili: 12/09/2010 -: Maisha ya Kuongozwa na Roho Mtakatifu
Fuatilia Mfululizo wa somo hili kwenye Website ya Kanisa.
...Ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwa kutupa Waamini sisi tulio mwamini, Kiongozi ambaye wakati wote nia yake ni kutufikisha katika burudiko la kweli. Sisi tukiwa kama binadamu, tumeumbiwa kuongozwa na utawala fulani katika maisha yetu. Katika hali yoyote, binadamu lazima aongozwe na utawala mmoja kati ya Utawala wa Giza uliotawaliwa na Dhambi na Mauti, au Utawala wa Nuru, uliotawaliwa na Uzima wa Milele na Bududiko la kweli katika Kristo Yesu. Utawala wa Nuru, ni utawala wa Roho Mtakatifu ndani ya Maisha ya Mwamini. Utawala wa Roho Mtakatifu, wakati wote ni utawala wa faida, ni utawala uliojaa Upendo usio kifani, na gharama yake hailinganishwi na kitu chochote, kiwe Fedha, Dhahabu n.k. Ni utawala wenye ukamilifu katika kila idara ..
Fuatilia Somo letu la jumapili iliopita, lenye kichwa cha Somo "Maisha ya kuongozwa na Roho Mtakatifu" kama lilivyoletwa kwetu na Mtumishi wa Mungu Mama Lilian Ndegi.