Wanafuraha ya ajabu hawana mawazo wanaamani haijalishi hali ngumu kiasi gani ya maisha wanapitia burudani lazima iwepo. Tuweni kama watoto wadogo jamani hata biblia yetu inatuambia.
HATA IMEKUWA MTU AKIWA NDANI YA KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA, YA KALE YAMEPITA TAZAMA YAMEKUWA MAPYA!!2KOR. 5:17
Haya wapendwa ahadi ni deni vivazi hivi hapanaaaa vya kanisani (hebu piga picha umekaa mbele na kivazi hizi inakuwaje jamani) mkao utakavyokuwa unahangaika haya mara Roho Mtakatifu anakushukia si ndio kazi itakuwa kweli kweli kwa maana itabaidi wamama wawe na kazi ya ziada ya kukufunika kila wakati. Tujiangalie na vivazi vya kuendea kanisani.


Ukiacha hayo makofia kwa maana mengine ni makubwaa hata ukikaa mbele mwenzio unakuwa unamziba otherwise kwa kanisani nguo hizi ni bomba sana bila hiyana mtoto wa kiafrica unatoka chicha.
