BABA NINALITUKUZA JINA LAKO NASEMA ASANTE SANA BWANA KWA KUWEZA KUTULINDA NA KUTUPA AMANI, ASANTE KWA ULINZI WAKO, BARAKA ZAKO NA UPENDO USIO NA KIPIMO, ASANTE KWA KUTUPA TUMAINI NA FURAHA KWA MWAKA ULIOPITA NAKUSHUKURU BWANA KWA KUTUVUSHA SALAMA NA SISI KUWEZA KUUONA TENA MWAKA 2011 ANZA NASI TENA KWA UPYA BWANA KATIKA MWAKA HUU NA KARNE HII MPYA JEHOVA ENDELEA KUTUTIA NGUVU, TUPE AMANI, FURAHA, UTU WEMA, FADHILI ZAKO, BUBUJIKO LA ROHO WAKO MTAKATIFU, NA UPENDO WA KWELI UUMBIKE NDANI YA MAISHA YETU, TUNDA LA ROHO MTAKATIFU LIZIDI KUUMBIKA NDANI YETU, TUPE ROHO YA UNYENYEKEVU NA MOYO ULIOPONDEKA, NA UWEPO WAKO BWANA USITUONDOKEE, BARIKI KAZI ZA MIKONO YETU, BARIKI WATOTO WETU NDOA ZETU, FAMILIA ZETU, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA HATA MAJIRANI ZETU WOTE KWA MWAKA HUU MPYA NA KARNE NYINGINE BWANA, BARIKI KUINGIA KWETU NA KUTOKA KWETU, TUNASIHI KIBALI MBELE YAKO BWANA NA KWA WANADAMU PIA, TUNAOMBA KIBALI CHAKO POPOTE TUINGIAPO NA TUNAPOKANYAGA BWANA ONEKANIKA WEWE BWANA KILA TUINGIAPO, MANENO YA VINYWA VYETU JEHOVA YATAWALIWE NA WEWE TUWE NI WATU WA KUBARIKI KWA MWAKA HUU NA SIO WA KULAANI TUWE NI WATU WA KUTIA MOYO NA KUWALETA WATU KWAKO EE BWANA, ROHO MTAKATIFU FANYA MAKAO KATIKA VILINDI VYA MIOYO YETU. TEMBEA NASI TUSHIKE MKONO UTUONGOZE WEWE KWA MWAKA HUU WOTE NA HATA MILELE NA MILELE NINAOMBA HAYA KUPITIA JINA LA MWANAO MPENDWA YESU KRISTO ALIYE BWANA NA MWOKOZI KATIKA MAISHA YETU. AMEN AMEN AMEN
HERI YA MWAKA MPYA WENYE BARAKA TELE NA AMANI YA BWANA IWATAWALE KATIKA MAISHA YENU NA FAMILIA ZENU KWA UJUMLA
MZIDISHIWE BARAKA NA BWANA YESU KRISTO ALIYE HAI
HAPPY NEW YEARRRRRRRRRRRR.