Wednesday, September 8, 2010

BACK TO SCHOOL PRAYER

BWANA APEWE SIFA WAPENDWA. Jana tarehe 7/9 tulikuwa na maombi ya kuwaombea watoto wetu wanaorudi mashuleni / vyuoni hata wazazi pia wanaosoma nao walipata kibali mbele za bwana na Mtumishi wa Mungu akawaombea. Maombi yalianzia umri 0 - wanaochukua PHD wote walikuwepo pale Brooklyn Tabernacle Church  (Brooklyn- New York). Namshukuru Mungu sana kwani na mimi nilipata kibali cha kuwepo  kwa ajili ya kuwaombea watoto wangu walioko TZ ambao nao siku ya leo ndio walikuwa wanafungua shule na ndio mwaka mwingine wa masomo kwao wameingia darasa jipya pia na watoto wa dada yangu walioko huku USA. Kusema kweli sisi wana wa Mungu (wazazi) tunahitaji sana kuwaweka watoto wetu mikononi mwa Mungu kwani huko mashuleni wanakumbana na vikwazo mbalimbali na sisi kama wazazi hatuwezi kwenda nao shule ili tuweze kuwasaidia hapa ni mtoto peke yake na Mungu wake. Mtoto anakutana na watoto wengine ambao wamelelewa katika mazingira tofauti na ya nyumbani kwao, wenye tabia tofauti na ambao wenye kumjua Mungu na ambao hata hawajawahi kusikia kitu kama hicho. Hivyo bila msaada wa Mungu kwa kweli sisi wenyewe wazazi hatuwezi, hatuna uwezo wa kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja lakini yupo mwenye uwezo huo na zaidi. Kwa kweli watoto wetu wa karne hii wametuzidi sana maujanja wazazi wana mambo mengi na makubwa kuliko hata ya bibi zao ambao wameishi miaka mingi na kukumbana na mambo mengi. Utakuta mtoto wa shule ya msingi hata kwa mganga wa kienyeji anakwenda (anafuata nini? zaidi sana ni kuwaloga wenzao ktk masomo na kuwaloga hao wanaowaita mabuzi upo!) na wengine wanakwenda huko kwa waganga hadi wamekuwa wachawi yaani wanajua  na kufanya mambo mengi ambayo sisi wazazi wao hata hatukufikiria  wala hatufikirii kuyafanya au hata kutaka kuyajua. Je ni nani atakayeweza kuwaoko watoto wetu na kuwaponya na mkono wa yule adui shetani kama sisi wazazi hatutawasimamia jamani na kuwaombea na kuomba muongozo wa Roho Mtakatifu katika kuwalea na kuwakabidhi kwake. Tutafakari jambo hili wapendwa tuone umuhimu wa kuwaombea watoto wetu sana haijalishi ni mdogo kiumri kwa kiasi gani bado shetani anaweza kumtumia vile vile. Usijidangaye kuwa mtoto bado ni mdogo hajui hili wala lile lakini shetani anaona kuwa hicho ndicho chombo kizuri anachoweza kukitumia ili kukufadhaisha na kukutumia wewe kuwa mtumwa wake kama apendavyo. Mfano unakuwa na mtoto ambaye anasumbuliwa na magonjwa mara kwa mara kila leo wewe uko hospitali unasali sana mama / baba wa watu lakini bado tatizo liko pale pale kumbe bado mtoto wako haujamkabidhi mikono mwa Bwana na kumwombea kila atokapo na aingiapo. Unapomwacha nyumbani na mtu mwigine hujui ana maroho gani kwani sisi wanadamu hatuwezi kuona kwa kuangalia sura bali Mungu yeye ndiye aonaye mioyo yetu wanadamu na kujua ni yupi aliye mwema na aliye mwovu. Hivyo hata wale tunaowaacha wawe waangalizi wa watoto wetu tunatakiwa kuwaombea na kuomba Roho Mtakatifu awaongoze katika kumjua Mungu kama bado hawajamjua kama tayari katika kuwa wa kweli na wawazi mbele za Bwana kwani wao ndio wanaokaa na watoto wetu kwa muda mwingi wanaweza kupandikiza kitu kisichofaa kwa watoto wetu bila sisi kugundua tunabaki kuwakandamiza watoto kwa kuwaona wanatabia zisizofaa. Biblia inatuambia kuwa "Lakini katika mambo hayo yote tutashinda na zaidi ya kushinda kwake yeye aliyetupenda"Warumi 8:37 Hivyo basi cha msingi ni tuyaache yote madhabahuni tusijitwike mizigo ambayo hatuwezi kuibeba Bwana Yesu anatuambia kuwa tumpatie mizigo yetu iliyo mizito na yeye atupe wa kwake ambao ni mwepesi kwa nini ulemewe na yupo aliyejitolea kukusaidia? Mkabidhi Roho Mtakatifu mambo yako yote na ukubali akutumie nawe upate kuona furaha ya kweli kuwa ndani ya Kristo naye atakupasha hata mambo yajayo ndani ya maisha yako na ya watoto wako. Yoh.16:13. pia Tunaambiwaaaa "Onjeni mwone ya kuwa Bwana yuu Mwema"

SHUKRANI

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa wale wote walioniandikia e-mail kunitia MOYO na hata kuleta maombi yao kwangu nawashukuru sana. Kusema kweli  MAOMBI YOTE nitayafanyia kazi na naamini Mungu wangu ninayemtumainia atawajibu kila mtu hitaji la MOYO wake, wenye magonjwa hakika mtaponywa na hakuna kulemewa tena na mizigo. Wengi mmeomba nisipublish maombi yenu nami naahidi kutokufanya hivyo (yote mliyoandika ni siri), japo kwa wale ambao watakubali kutoa ushuhuda wanakaribishwa kwa sababu unapotoa ushuhuda unamwaibisha shetani na vile vile unamfungua na mwingine ambaye alikuwa anatatizo kama lako naye anapata kufunguliwa katika vifungo mbalimbali walivyofungwa. (majina hayatatajwa hivyo usiwe na hofu). Nitakuwa natoa mistari ya Biblia ya kusoma kila siku vile vile kwa wale tunaowasiliana kwa njia ya e-mail nitakupatia kulingana na hitaji lako.

Tusikate tamaa kwani tumaini la Bwana lipo na hakuna lisilowezekana na lisilo na jawabu chini ya jua hili yote yawezekana kwake yeye yule aaminie. HAKIKA UTASHINDA KWANI HAKUNA JARIBU LISILOKUWA NA MLANGO WA KUTOKEA. BARIKIWA  SANA NA BWANA.