BWANA WA MAJESHI ASEMA HIVII,
Itatokea halafu ya kwamba watakuja mataifa na wenyeji wa miji mingi, wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! twendeni zetu kwa haraka tuombe fadhili za Bwana, na kumtafuta Bwana wa Majeshi, Mimi nami nitakwenda. Naam, watu wa kabila nyingi na mtaifa hodari yatakuja Yerusalem, kumtafuta Bwana wa Majeshi, na kuomba fadhili za Bwana. Bwana wa Majeshi asema hivii, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi, naam wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi kwa maana tumesikia ya kwamba Mungu yu pamoja nanyi.
Je haya maono ya Nabii Zekaria yametimia? Kwani ukiangalia kwa sasa watu wengi wanakimbilia Israel. Watumishi wa Mungu mbalimbali wanaandaa safari za watu kwenda kuona na kuomba fadhili Israel. Mataifa hodari nayo yanaitetea Israel kwa maana wamejua kuwa Mungu yupo pamoja na wana wa Israel, je ni kwamba unabii alioutoa mtumishi wa Mungu Nabii Zekaria unatimia? Tutafakari njia zetu tugeuke tutafute uso wa Bwana kwani nyakati za mwisho zimekaribia. Mpendwa fanya hima usibaki nyuma tafuta sana kuuona mkono wa Mungu ndani ya maisha yako. Mimi na nyumba yangu hatukubali kubaki nyuma wewe jeee?