HATA IMEKUWA MTU AKIWA NDANI YA KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA, YA KALE YAMEPITA TAZAMA YAMEKUWA MAPYA!!2KOR. 5:17
Tuesday, November 9, 2010
MAVAZI YA VIJANA WA LEO
Sijui ni kwanini vijana wetu wanapenda kuvaa style hii na sijui ni nani aliyeanzisha na kwa sababu gani kwani inamfanya kijana aonekana kuwa ni kijana mhuni hata kama hana tabia za kihuni. Juzi nilikutana na kijana mdogo kweli kweli wa miaka kama tisa kumi, alikuwa amesuka nywele zake mwenyewe na yeye kavaa style hii sema ya kwake ilikuwa imeshuka zaidi yuko na mama yake. Nikamwangalia nikajaribu kuchunguza nijue ameishikilia na nini hiyo suruali kwani ilikuwa inaonekana kama inadondoka vile lakini wapi alikuwa kama anapata shida kutembea maana anajaribu kuibalance nadhani isidondoke au ndio miondoko yenyewe kwa kweli sikupata jibu, lakini mwenyewe alikuwa anajiona yuko sawa na mama naye alikuwa anaona ni jambo jema tu. Nikatamani ni mwambie ndugu mwambie mtoto avae vizuri sema nikaona hayo maneno ningepewa hapo ningelazwa hospitali kwani wa dada black american kwa kuongea mhuu mzaramo haoni ndani. Nilichofanya ni maombi tu ya kimya kimya sina zaidi. Tuzidi kuwaombea watoto wetu wote awe msichana awe mvulana wote wanahitaji maombi ya haswa bila kuzembea.
picha kwa hisani ya issa michuzi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment