BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO NALITUKUZA JINA LAKO NA NINAKUSHUKURU KWA WEMA NA FADHILI ZAKO UNAZONITENDEA NDANI YA MAISHA YANGU SIKU HADI SIKU. ASANTE KWA UPENDO WAKO, ASANTE KWA REHEMA ZAKO, ASANTE KWA KUNIPA TUMAINI SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU, ASANTE KWA ULINZI WAKO NA BARAKA ZAKO UNAZONIPA SIKU HADI SIKU. LIHIMIDIWE JINA LAKO.
NAKUSHUKURU MUNGU WANGU KWA AJILI YA BABA HUYU, MAMA HUYU, KIJANA HUYU, BINTI HUYU NA WALE WOTE WATAKAOFUNGUA MAOMBI HAYA KWA MAANA MUNGU UMEZIDI KUWAPENDA KWA JINSI YA TOFAUTI. ENDELEA BWANA KUONYESHA UWEZA WAKO NA PENZI LAKO NDANI YA MAISHA YAO. WASAMEHE MAKOSA YAO BWANA NA UWAREHEMU NA KUWAHURUMIA, DAMU YA YESU KRISTO ULIYOMWAGIKA PALE MSALABANI KWA AJILI YA ONDOLEO LA DHAMBI IWATAKASE DHAMBI ZAO NA KUWASAFISHA NA KUWAWEKA HURU. USIWAACHE MFALME WANGU WA AMANI BALI WAZINGIRE KWA WIGO WAKO NA UTUKUFU WAKO UWAFUNIKE. ROHO MTAKATIFU WAFUNIKE KWA WIGO WA MOTO WAKO UTAWALE NYUMBA ZAO, FAMILIA ZAO, WATOTO WAO, NDOA ZAO NA HATA KAZI ZA MIKONO YAO. USIWANYIME BARAKA ZAKO KILA IITWAPO LEO BWANA WANGU TEMBEA NAO KATIKA MAISHA YAO YA KILA SIKU KILA WAINGIAPO NA WATOKAPO WAKAPATE KIBALI MACHONI PAKO NA KWA WANADAMU PIA EE MWOKOZI WANGU. WAPE ILE HAJA YA MIOYO YAO BWANA KWANI WANAKUTUMAINIA WEWE TU KWA MAANA WEWE NDIWE NGAO YAO, NGOME YAO NA MSAADA KATIKA MAISHA YAO NA BILA WEWE BWANA HAWEZI KUFANYA JAMBO LOLOTE KWANI WEWE NDIO TEGEMEO LAO KUU.
WAKINGE NA KILA NGUVU ZA GIZA NA MAJARIBU YALETWAYO NA YULE MWOVU. WAOKOE KATIKA VISHAWISHI, KILA ROHO ZITAKAZOINUKA JUU YAO SIKU HII YA LEO NA ZISHINDWE KATIKA JINA LA YESU, NAKATAA ROHO YA HOFU NDANI YA MAISHA YAO KATIKA JINA LA YESU, NAKATAA MAGONJWA, NAKATAA ROHO YA UCHUNGU, HASIRA, CHUKI , KUKATA TAMAA KATIKA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARET ALIYE HAI. KIFUNGO KIWAYO CHOTE WALICHOFUNGWA NDANI YA MAISHA YAO NINAKIFUNGUA SASA KATIKA JINA LA YESU, NINAWAKOMBOA KATIKA ULIMWENGU WA KIROHO NA KUWARUDISHA POPOTE WALIPOFUNGWA KATIKA JINA LA YESU. SHETANI HANA MAMLAKA NAO, NGUVU ZA GIZA HAZINA MAMLAKA NAO, WACHAWI HAWANA MAMLAKA NAO, MAJINI HAYANA MAMLAKA NAO KUANZIA SASA, KUANZIA LEO KATIKA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI.
NAWAPA AMANI YA KRISTO, UPENDO, FURAHA, TUMAINI, AFYA NJEMA NA KILA HALI YA UWEZA WA MUNGU KATIKA MAISHA YAO YA KILA SIKU KUANZIA SASA. UWEPO WAKO BWANA USIWAPUNGUKIE BALI UZIDI KUWAFUNIKA NA KUWAONGOZA KILA WAKANYAGAPO WAPAMILIKI MUNGU WANGU. ROHO YA UNYENYEKEVU IUMBIKE NDANI YA MAISHA YAO, TUNDA LA ROHO MTAKATIFU LIUMBIKE NDANI YAO BWANA. ROHO MTAKATIFU TAWALA MAISHA YAO, ONEKANIKA BWANA NDANI YA MAISHA YAO. USIWAACHE JEHOVA BALI UZIDI KUWATUMIA KAMA CHOMBO CHAKO KITEULE. FANYA JAMBO JIPYA NDANI YA MAISHA YAO SASA BWANA, ANZA NAO KWA UPYA LEO TENA BWANA.
NAKUSHUKURU MUNGU WANGU, NASEMA ASANTE ROHO MTAKATIFU KWA MAANA MAOMBI HAYA YAMEKUBALIKA MBELE ZAKO NA YAMEKUWA MANUKATO KATIKA KITI CHAKO CHA ENZI EE MUNGU WANGU.
KATIKA JINA LA MWANAO MPENDWA YESU KRISTO NINAOMBA NA KUSHUKURU.
AMENI! AMENI! AMENI!
KATIKA JINA LA MWANAO MPENDWA YESU KRISTO NINAOMBA NA KUSHUKURU.
AMENI! AMENI! AMENI!