Friday, January 21, 2011

KUBALI KUWA MLAWI

The Brooklyn Tabernacle Choir is currently accepting applications for membership. If you are interested, and are a member or in the process of becoming one, please apply online at:www.brooklyntabernacle.org/choirapp


The Brooklyn Tabernacle Music Staff

Haya kwa wale wenye karama ya kuimba au kama unajijua unayo sauti kama chiriku au hata ya kumtoa nyoka pangoni jiunge basi kuwa member wa Brooklyn Tabernacle Choir ukamwimbie Bwana maana kwenye sifa Mungu huwapo kwani yeye anapenda nyimbo za sifa na shukrani kuliko kitu kiwayo chote naye hushuka nakuja kuweka makao hivyo hima jiandikishe tumwimbie Bwana Sifa (kubali kuwa Mlawi) Soma 2 M/ Nyakati 5: 11-14

BWANA YESU ANAKUMBIA NINI LEO HII

Mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwone haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.