Monday, November 8, 2010

NENO LA UZIMA (TUTAFAKARI NJIA ZETU)

BWANA WA MAJESHI ASEMA HIVI,

Zitafakarini njia zenu. Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo, mnakula lakini hamshibi, mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji, mnajivika nguo lakini hapana aonae moto; na yeye apatae mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka toboka.

Uzao niliobarikiwa na Bwana. No 2


Huyu ndiye Joe first born wangu siku ya visiting day mwezi uliopita 23 hapa akiteta na mama. Lazima mausia yawepo niliongea weeeee mpaka basi. Asante Mungu kwa kunikuzia kijana.


 Aliyevaa black tshirt ndiye no 2 kijana Tee anakwambia peace akiwa na sisteri wao Nicole. Hilo pozi la Nicole kama model vile itabidi nimwandikishe kwa Tyra Banks kwenye American next top model.

Junior, Tee na Nicole
Jua lilikuwa limewachomaa wanagu masikini wakawa weusi na naona walikuwa na njaa hao hakuna aliyekuwa anaongea na mwenzake hapa.

Junior kamdomo kanameremeta ungefuta mdomo mwanangu ungetoka chicha mzee wa mapozi

Asante kwa wote mliofika kumwoka kijana Joe mbarikiwe na Bwana.

NENO LA UZIMA

BWANA WA MAJESHI ASEMA HIVII..

YA KWAMBA FANYENI HUKUMU ZA KWELI, KILA MTU NA AMWONEE NDUGU YAKE REHEMA NA HURUMA; TEMA MSIMDHULUMU MJANE , WALA YATIMA ,WALA MGENI, WALA MASIKINI, WALA MTU AWAYE YOTE MIONGONI MWENU ASIWAZE MABAYA JUU YA NDUGU YAKE MOYONI MWAKE.
LAKINI HAO WALIKATAA KUSIKILIZA WAKAGEUZA BEGA LAO, WAKAZIBA MASIKIO YAO ILI WASISIKIE. NAAM WALIFANYA MIOYO YAO KUWA KAMA JIWE  GUMU, WASIJE WAKAISIKIA SHERIA NA MANENO YA BWANA WA MAJESHI, ALIYOYAPELEKA KWA ROHO YAKE KWA MKONO WA MANABII WA KWANZA , KWA SABABU HIYO GHADHABU KUU IKATOKA KWA BWANA WA MAJESHI
IKAWA KWA SABABU ALILIA, WAO WASITAKE KUSIKILIZA, BASI, WAO NAO WATALIA, WALA MIMI SITASIKILIZA, ASEMA BWANA WA MAJESHI