Friday, March 25, 2011

Fanyika tawi lizaalo katika mzabibu.

Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Kaeni ndani yangu nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu, kadalika nanyi msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi neno lolote. Mtu asipokaa ..................................
Yohana 15:1-8

Thursday, March 24, 2011

Utukufu na Heshima ni kwa Bwana Mungu tu

Baba Ninakushukuru kwa wema na fadhili zako nasema asante kwa kunipenda kwa pendo la kipekee pendo la agape, uhimidiwe maana unastahili, utukuzwe kwa maana unastahili upewe sifa kwa maana unastahili unastahili! unastahili! unastahili! Bwana wangu. Nakupenda sana sana Bwana asante kunipenda asante kwa kunibariki asante kwa kila kilicho katika maisha yangu. Bila wewe mimi siwezi ni kwa uweza wako na nguvu zako mimi niko hivi nilivyo leo hii asante sana Bwana wangu. Mkono wako ni mkuu sana umenitangulia katika kila jambo ndani ya maisha yangu asante sana Bwana nakupenda sana Mungu wangu. Sina Mungu mwingine ila ni wewe sina Bwana mwingine ila ni wewe na sina kiongozi mwingine katika maisha yangu ila ni wewe tu Bwana ni wewe tu Mungu wangu ni wewe peke yako ndio tegemeo langu ngome yangu na uzima. Uhimidiwe Mungu wangu uhimidiwe Mfalme wangu uhimidiwe ewe uliye kimbilio langu, utukufu na heshima ni kwako Bwana wangu na Mungu wangu. Amen Amen Amen

Thursday, March 3, 2011

TUMIA MAMLAKA ULIYOPEWA NA MUNGU

Mungu ametupa mamlaka ya kipekee sisi wanadamu katika ulimwengu huu sema tu ni kwamba tunashindwa kutumia hiyo mamlaka. Ukisoma katika Mwanzo 1:27-30 Biblia inasema Mungu akamuumba mwanadamu kwa mfano wake na pia akampa mamlaka ya kutawala samaki wa baharini na ndege wa  angani na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu nchi, vyote hivi mwanadamu alipewa kuvitawala na Mungu. Swali la kujiuuliza ni kwamba je inakuwaje mwanadamu wa leo anakuwa hana uwezo wa kuvitawala vitu hivyo?
Tunaweza kuona kuwa baada ya anguko la Adam mwanadamu amekuwa akishindwa kuvitwala viumbe vyote na vyote vilivyomo duniani na hii imekuwa ni kifungo kikubwa kwa wanadamu hadi leo hii kwa maana toka Adamu afukuzwe katika bustani ya Eden watu wamekuwa wakihangaika huku na kule bila kujua nini cha kufanya sababu shetani amekamata fahamu zetu ili tusiweze kukumbuka na kutumia mamlaka hii tuliyopewa na Bwana. Lakini Mungu kwa upendo wake na huruma zake na kwa Neema yake ya pekee alimtoa mwana wake Yesu Kristo ili kutupatanisha naye kutuwezesha kutumia ile mamlaka ya kutawala dunia kama ilivyokuwa kusudi lake hapo awali la kumuumba mwanadamu.
Jambo la msingi na la kipekee ni  kupokewa Neema hii tuliyopewa bure ya kumkubali Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi ndani ya maisha yatu ili tuweze kutumia tena yale mamlaka. Ukisoma ktk kitabu cha TITO 2:11-12 utaona kuwa Biblia inatuambia kuwa Neema ya Mungu imefunuliwa kwetu nayo inatufundisha kuukataa ubaya .... hii Neema iliyofunuliwa ndio wokovu wenyewe ambao unatuwezesha sisi wanadamu kukiri kuwa Yesu ni Bwana, kwani yeye alifanyika chombo cha kuweza kutubebea ile laana aliyoipata Adam baada ya anguko. Soma Isaya 53:4-5 .... kwa kupigwa kwake sisi tumpona. Hivyo basi Bwana wetu Yesu ameturejeshea ujasiri na nguvu na uweza wa kutumia ile mamlaka ambayo tunatakiwa kuwa nayo kwani kwa kuliita jina lake tu magonjwa, pepo, na nguvu zote za giza zinakimbia. Hakutakuwa tena na maonevu yaletwayo na yule mwovu shetani katika maisha yetu hofu, kuyumba katika kipato, biashara, ndoa, watoto hata katika ulimwengu wa kiroho kwani utakuwa tayari unajua ni jinsi gani unaweza kupigana vita na ukaweza kuvishinda hakuna kitakachoweza kukudhuru kwani uweza unao mikononi mwako tayari ni jinsi gani tu unaweza kutumia na ni silaha zipi utumie ili uweze kushinda.
Ukisoma tena katika Zaburi ya 91:13 utaona pia Mungu amekupa uweza na mamlaka ya kumwangamiza adui. Anasema hivi : Utawakanya simba na nyoka, mwana simba na joka utawaseta kwa miguu. Kwa hiyo kilichobaki ni wewe kujitambua na kujikubali kuwa uweza na mamlaka unayo kwamba kusudi la Bwana Mungu kukuumba ni ili utawale dunia. Jione kama vile mtoto mchanga anavyomwamini mama yake kuwa akimbeba hatamwangusha na wewe pia mpendwa unatakiwa kumwamini Mungu kuwa hakika hatakuacha mamlaka aliyokupa ni sahihi na hawezi kukuangusha kwani anajua kuwa ukitumia na kufuata kanuni zake lazima utakuwa imara na mshindi siku zote za maisha yako vyote vilivyo katika ulimwengu huu vitatiishwa chini ya miguu yako.
Ukiwa kama mwana wa Mungu umeokoka na unampenda Yesu jua kwamba wewe pia unauwezo na mamlaka ya kuumba na kubomoa pia. Ukisoma katika Zaburi 8:5-6 Biblia inasema kuwa sisi wanadamu tumefanywa kidogo chini ya Mungu kwa maana ya kuwa baada ya Mungu ni sisi wanadamu tunafuata na vile vile bado Biblia inasisitiza jinsi gani tumepewa mamlaka ya kuweza kutawala viumbe vyote. Bwana Mungu ametupa kibali mbele zake kwani katika ufalme wa Mungu wewe na mimi ni Waziri Mkuu vyooote viko mikononi mwako na mwangu unachotakiwa kuitumia tu mamlaka hiyo. Ukiangalia hata ktk hali ya kibinadamu mfano wa nchi yetu Waziri Mkuu ni mtu mkubwa sana katika serikali na anayo mamlaka juu ya vyombo vya dola vyote na anasauti katika serikali na katika nchi na pia anao mawaziri chini yake wa kuweza kumsaidia sasa basi kama jinsi alivyo Waziri Mkuu na Mawaziri wake ndivyo na wewe pia ulivyo katika ufalme wa Mungu ni Waziri mkuu unayo mamlaka unayo sauti unao Mawaziri chini yako ambao ni Malaika kwa ajili ya kukusaidia. Je unawatumiaje hao Malaika (mawaziri wako) katika ulimwengu wa kiroho kukusaidia? ni juu yako sasa ewe Waziri Mkuu, Mungu amekupa mamlaka tayari yeye ni Mfalme anasubiri umpe ripoti tu kuwa umefanya nini na unatazamia  kufanya nini katika maisha yako kwa familia yako, kwa watoto wako, kwa jamaa zako, kwa majirani zako, kwenye biashara, kwenye kazi nk. Hivyo basi tumia mamlaka hiyo sasa bila hofu fungua moyo wako chukua mamlaka uliyopewa kama Waziri Mkuu fanya maamuzi sahihi vaa ujasiri hakika utauona mkono wa Bwana katika maisha yako.  Bwana wetu Yesu Kristo anakwambia pia katika Mathayo 16:19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lolote utakalofunga duniani litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalofungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni; sasa rafiki, ndugu yangu unataka upewe nini tena Yesu mwenyewe anasema amekupa ufunguo kwa maana nyingine amekupa mamlaka ya kufungua na kufunga yale uyatakayo; mfano kama mtu ana chumba chenye dhahabu tele na fedha anakuambia chukua funguo hii chochote ukitakacho humo ndani ya chumba uchukue kama ni fedha kama na dhahabu na yeyote anayetaka wewe ndio unayo mamlaka ya kumfungulia mlango kuingia kuchukua au la; mfano mwingine ni kuwa umepewa ufunguo ambao unauwezo wa kuwafungulia wafungwa walioko gerezani au au kuendelea kuwafungia humu. Hiyo ndio mamlaka uliyopewa na bwana. Itumie mpendwa kamata hizo funguo kwa kujiamini kuwa ni zako fungua mlango uingie fungua mlango upate baraka za Bwana alizokusudia uwe nazo. Usikate tamaa usivunjike moyo Yesu ni yeye yule jana leo na hata milele hatokuacha kamwe ameahidi kutenda atatenda amekupa mamlaka sasa itumie, itumie, itumie.
Kama bado haujaokoka basi rafiki mkubali Yesu kuwa ni Bwana na Mwokozi katika maisha yako leo mpokee Yesu  kwa kumaanisha ili mamlaka hii iwe dhahiri kwako uweze kuvishinda vyote na kutawala kama Bwana Mungu alivyokusudia kwa kukuumba kwako ewe mwanadamu. Tafuta uso wake kwa bidii kwa kusoma Neno kwani Neno ndiye Mungu mwenyewe ukisoma Yohana 1:1 bibilia inasema kuwa...... Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu. Hivyo Neno la Mungu ni Mungu mwenyewe kwa hivyo unaposoma hili Neno la Mungu unakuwa umemwingiza Mungu ndani ya maisha yako na yeye basi kwa upendo wake na kwa Neema yake anaanza kutenda kazi ndani ya maisha yako yale yote yaliyokuwa magumu hapo awali kwako yanakuwa mepesi kwa vile unaye Mungu ndani yako na kama nilivyosema hapo juu ni kuwa kwa kuwa Mungu alikuumba punde kidogo chini yake na amekupa mamlaka ya kutawala viumbe vyote na vyote vilivyomo humu duniani basi ni dhahiri vile vyote uvitakavyo utavipata bila wasiwasi. Ukisoma Zaburi 1:2-3 utakuwa na mafanikio katika kila ulitendalo kwa kusoma Neno lake tu na kutumia mamlaka aliyokupa.
Mimi nimejikubali, nimemkubali Yesu kuwa ni Bwana na mwokozi ndani ya maisha yangu na mamlaka naitumia na nimeona jinsi anavyotenda mambo makuu na ya ajabu katika familia yangu. Karibu nawe uweze kutumia mamlaka hiyo.
Ubarikiwe na Bwana.

Thursday, February 24, 2011

NAMSHUKURU MUNGU

Nazidi kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake katika maisha yangu amenipa nguvu na tumaini katika siku zote za maisha yangu. Hakuniacha kamwe amekuwa nami siku zote katika mapito yoyote niliyopitia alikuwa nami hakuniacha hadi siku hii ya leo natimiza miaka kadhaa hakuwahi kuaniacha bali alinikumbatia na kunishika mkono na kunipa penzi lake la kweli na kunitia moyo akinihakikishia maisha ya amani na furaha yenye baraka. Nami nazidi kushuhudia sasa kuwa nimeuona mkono wake ulivyo mkuu na uweza wake wa ajabu umetenda mengi mema na uwepo wake umenifunika mimi na familia yangu kwa jinsi ya kipekee kwa kweli nina kila sababu ya Kumshukuru na kutangaza fadhili zake; nazidi kumtukuza kwa maana anastahili sana sana.

Asante Mungu wangu kwa kunipenda, uhimidiwe Bwana wangu.

Sunday, February 13, 2011

UHIMIDIWE BWANA

Nitayasimulia matendo yake ya ajabu maana anastahili yeye ni mwaminifu na tena ni mwema sana utukufu na heshima ni kwake. Yeye ni mkuu sana yeye ni wa pekee anatenda maajabu ndani ya maisha yetu kila iitwapo leo. Mkono wake ni mkuu sana nao hutuongoza kila tuendapo, katika kila kona ya maisha yetu uko pamoja nasi na yeye hutuwazia yaliyo mema kila siku anatupenda upeo; upendo wa Agape anatupa tumaini siku zote za maisha yetu. Tuzidi kumpa sifa na utukufu na shukrani kwa maana anastahili.

Unastahili kuabudiwa Bwana wangu, unastahili kutukuzwa, unastahili kupewa sifa, utukufu na heshima ni kwako wewe, uhimidiwe, uinuliwe, ninakusujudia Bwana wangu nainua mikono yangu kwako kwa ishara ya kusarenda kwamba bila wewe mimi siwezi, bila wewe mimi si kitu ni wewe tu ndio kimbilio langu, ngome yangu na msaada wangu. Hakuna aliye mkuu kama wewe hakuna Mungu kama wewe hakuna mfalme kama wewe ni wewe peke yako unayestahili uabudiwa na kutukuzwa Mungu Mkuu Bwana wangu.
Naliinua jina la mwana wako wa pekee Yesu Kristo, jina lililo kuu, jina lipitalo majina yote lenye uweza wote, lenye neema litetalo uzima kwa jina hilo tumepata kukombolewa nakushukuru sana sana Bwana wangu. Nakurudishia sifa na utukufu maana unastahili. Haleluya Bwana; Haleluya Mungu wangu uhimidiwe Bwana asante sana na nashukuru kwa kila jambo ndani ya maisha yangu nakushukuru Bwana sana.

Friday, February 11, 2011

NI NANI ATAKAYEKUTENGA NA UPENDO WA MUNGU?

WARUMI 8:35-39

NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO? JE NI DHIKI, AU SHIDA, AU ADHA, AU NJAA,  AU UCHI, AU HATARI, AU UPANGA?

BIBLIA INATUNAAMBIA KUWA KATIKA MAMBO HAYO YOTEEE .................
LAKINI KATIKA MAMBO HAYO YOTE TUNASHINDA, NA ZAIDI YA KUSHINDA, KWA YEYE ALIYETUPENDA.
KWA MAANA NIMEKWISHA KUJUA HAKIKA YA KWAMBA, WALA MAUTI, WALA UZIMA, WALA MALAIKA, WALA WENYE MAMLAKA , WALA YALIYOPO, WALA YATAKAYOKUWEPO, WALA WENYE UWEZO, WALA YALIYO JUU, WALA YALIYO CHINI, WALA KIUMBE KINGINECHO CHOTE HAKITAWEZA KUTUTENGA NA UPENDO WA MUNGU ULIO KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU.

SIFA NI KWA BWANA

NALIINUA JINA LAKO BWANA WANGU NAKUPA SIFA SANA MAANA UNASTAHILI, UNASTAHILI KUABUDIWA UNASTAHILI KUTUKUZWA WEWE NI MUNGU MKUU, WEWE NI MFALME WA WAFALME, BWANA NI MWEMA SANA MUNGU MWENYE KUSIFIWA MUNGU MWENYE UPENDO. UPENDO WAKO NI WA PEKEE NALIINUA JINA LAKO, POKEA SIFA BWANA, NAKUTUKUZA BWANA WANGU UWEZA WAKO NI WA AJABU, UHESHIMIWE, UNASTAHIL!I UNASTAHILI! KUTUKUZWA.

MATENDO YAKO NI YA AJABU, MKONO WAKO NI MKUU SANA ASANTE KUNIPENDA BWANA, ASANTE KUNIUMBA, ASANTE KUNIPA NEEMA YAKO, ASANTE KUNILINDA ASANTE KWA KUWA UMEKUWA MWAMINIFU NDANI YA MAISHA YANGU UTUKUFU NA HESHIMA NI KWAKO BWANA, UAMINIFU WAKO NI WA PEKEE NAKUPENDA SANA BWANA, POKEA SIFA NA HESHIMA UABUDIWE! UABUDIWE! BWANA WANGU.

HALELUYAH!   HALELUYAH!

Friday, February 4, 2011

NYAKATI ZA MWISHO ZIMEKARIBIA

MAMBO YANAYOENDELEA HUKO MISRI NI UTABIRI WA NABII ISAYA ALIYO TABIRI JUU YA MISRI UKISOMA KATIKA ISAYA 19: 1 ..... UTAONA JINSI NABII ISAYA ALIVYOTABIRI JUU YA MISRI. HABARI YENYEWE INAJITOSHELEZA UKISOMA KWA MAKINI UTAELEWA.

SASA JE WEWE UKO TAYARI? UMESHAANDA MOYO WAKO? KWANI ISHARA ZOTE SASA ZINATIMIA ZILIZONENWA NA MANABII KATIKA KITABU KITAKATIFU CHA MUNGU. UNASUBIRI NINI ANZA SASA FANYA HIMA KUMTAFUTA BWANA AWE MWOKOZI WA MAISHA YAKO ILI UWEZE KUUNGANA NA YESU KATIKA UFALME WAKE KWA MAANA ANASEMA BILA YEYE HAUWEZI KAMWE KUINGIA KATIKA UFALME WAKE ACHA MAMBO YA DUNIA HII , ACHA NJIA ZAKO MBAYA MKUBALI BWANA YESU AMBAYE NDIE NJIA 

YESU ANASEMA HIVII MIMI NDIMI NJIA KWELI NA UZIMA MTU HAJI KWA BABA ILA KWA NJIA YA MIMI. 

Egypt's Protests Day of Anger Riots 25 Jan 2011 Demonstrations Rare Raw ...




UTABIRI WA NABII ISAYA 19:1 HEBU SOMA NA UANGALIE NA HII. KAA TAYARI USIFANYE MCHEZO NYAKATI ZA MWISHO ZIMEKARIBIA

Sunday, January 30, 2011

USHUHUDA

Namshukuru Mungu sana kwa kunipa mafunuo ya kuanzisha hii Blog kwani toka nianzishe nimeona jinsi Mungu anavyotenda ndani ya maisha yangu na pia kunipa kibali mbele za watu kwani nimefanikiwa kukutana na watu kupitia blog hii ambao hapo kabla nilikuwa siwafahamu na kujua kuwa bado kuna watu wana kiu ya kumjua Mungu sana na wengi wako kwenye vifungo.
Nimepata email kadha wa kadha za watu kuomba maombi nami nimefanya hivyo kwa uweza wa Roho mtakatifu na usaidizi wake. Lakini hivi karibuni nimepata maombi ya kipekee kutoka katika nchi moja huko Africa. Huyu ni mtumishi wa Mungu ambaye analo kanisa lake lenye watu thelathini, yeye badala ya kuomba maombi aliomba asaidiwe Biblia kwa ajili yake yenye Maandishi makubwa ili aweze kuwafundisha vizuri waumini wake, kwani anasema kutokana na umri alio nao kwa maana ni mtu mzima macho yake hayaoni vizuri. Nami kwa msaada wa Mungu naamini ni kwa kibali chake kumwelekeza huyu mtumishi kwangu hivyo imenipasa kufanya  hivyo na zaidi. Namshukuru Mungu kwa hili kwani siku zote nilikuwa namwomba Mungu anitumie mimi kama chombo chake sasa naamini kuwa nimefanyika chombo kwa Bwana kwa watu kupata neno lake ambalo ni muhimu katika maisha yetu sisi sote na naamini litawafungua wengi katika vifungo.

Namshukuru Mungu kwa ajili ya hili kwani naamini hizi Biblia zitawaokoa wengi ambao watalisikia neno akiwahubiria huyu mtumishi nami nitakuwa nimeishi andiko katika Yohana 15:1-2

Bwana Yesu Apewe Sifa sana sana sana. Tuzidi kupendana na Amani ya Kristo itawale mioyoni mwetu. Amen amen.

RAHA YA UWOKOVU

Ukiwa ndani ya Yesu kuna raha  mpendwa asikwambie mtu, yote yanawezekana kwa Bwana hata yale ambayo kwa akili za kibinadamu ni magumu kuwezekana ili maradi tu umwamini. "Biblia inasema hivi, yote yawezekana kwake yeye aminie". Nami na mwamini Mungu nimeuona mkono wake ndani ya maisha yangu, amani niliyonayo leo na furaha vyote nimevipata kutoka kwake yeye. Ananishindia siku hadi siku kila kitu kwangu ni shwari kwani najua ninaye mwenye uweza wote aliye mbele yangu, anayenipenda aliyenishika mkono anayeijua kesho yangu tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu Bwana Mungu Yesu Kristo pamoja na Roho wake Mtakatifu naamini hata niacha kamwe, ananikumbatia na kunitia nguvu. Furaha, amani, utulivu, nguvu, na uweza ninavyo leo kwa sababu siku moja niliamua kuwa nataka kuwa na mshauri, mpenzi, mwalimu, kiongozi, baba Yesu Kristo ndani ya maisha yangu naye bila hiyana akanikubali akanivuta karibu nae akaniambia mwanangu karibu nyumbani hapa umefika yale uliyopitia na kuyaona hapo kabla hayatakupata tena kamwe na wala hautayaona. Kama alivyowaambia wana wake wa Israel kuwa hao Wamisri mnaowaona leo hamtawaona tena kamwe na mimi akaniambia kuwa  Wamisri waliokuwa katika maisha yangu sitawaona tena kamwe nami nina amini hivyo na zaidi. 

Wewe je unataka kuonja furaha na amani hii niliyo nayo mimi leoo?Njoo kwa Yesu leo ndugu yangu mkubali awe Bwana na Mwokozi katika maisha yako nawe utapata penzi la kweli lisilo na mawaa. Yale yote yaliomwiba kwako yatakwisha na hautayapata wala kuyaona tena.

Nampenda Yesu sana na Yeye anakupenda pia karibu upate furaha ya kweli na tufurahi pamoja.

Wednesday, January 26, 2011

BARIKIWA KWA KUMWOMBEA MWENZAKO (WAMAMA)

Jeremiah 29:11 "for I know the plans I have for YOU, declares the LORD
"Never give the devil a ride, he will want to take over the driving."

Dear Woman of God
Be still for a while and praise God for His favor, His grace and His awesomeness, God is able to do the impossible and is always near
He loves us unconditionally.

Dear God:
this is my friend, whom I love and this is my prayer for her
Help her live her life to the fullest, Please promote her and cause her to excel above her expectations. Help her to shine in the darkest places where it is impossible to love. Protect her at all times,
lift her up when she needs you the most, and let her know when
she walks with you, She will always be safe.

Love you Girl

asante dada Brenda D kwa kunitumia

Monday, January 24, 2011

The Principle of Evaluation: Assess Your Situation

“Do not think of your self more highly than you ought, but rather think of yourself with sober judgment in accordance with the measure of faith God has given you.” Romans 12:3 (NIV)
"Do you believe you can change? Do you believe things can be different in your life?"
You can’t get to where you need to be until you first know where you are. That’s why, if you want to change anything in your life, Romans 12 says you need to humbly assess or evaluate your current state.
Now the reason I say humbly is because we don’t want to admit what’s not working in our lives. We don’t want to admit we’re in a hole or things aren’t working out. We don’t like to admit we need to change. We want to pretend we have it all together. That’s the barrier of pride.
Humility is the ingredient for change that will counter our pride. We have to start by admitting we don’t have it all together.
What are you pretending is not a problem in your life? Is it a problem in your marriage? An addiction? A problem with your body? Whatever it is, you need to start with an honest evaluation of yourself.
Change also takes faith. Do you believe you can change? Do you believe things can be different in your life? Ask yourself how much faith you will need in order to make the changes you want in your life. Is it more than you have right now? That’s evaluating the measure of your faith.
I want you to grow in your faith because without faith it is impossible to please God. I want you to grow in the measure of your faith, and I want you to set goals that are so big they force you to grow in faith.
Where will you get this faith to grow? Romans 10:13 says, “Faith comes from hearing the Word of God” (NIV). In other words, if you read the Bible more, then your faith will grow, then your trust in God will deepen, and then you will change.

PRAYER (MAOMBI)

Father, in the Name of Jesus, bless me even while I'm reading this prayer and bless the one that sent this to me in a special way. Open doors in our lives today, Save and set free!
Give us a double portion of your Spirit as we take back everything that the devil has stolen:
****Emotional Health
****Physical Health
****Finances
****Relationships
****Children
**** Jobs
****Homes
****Marriages
I cancel every plot, plan and scheme the enemy has devised against us in the NAME OF JESUS.
And I declare:
NO WEAPON FORMED AGAINST US WILL PROSPER.
I speak LIFE into every dead situation. And, I thank You that nothing is over until YOU say it's over! Speak prophetically into our lives and to our situations:
****our households are blessed;
**** our health is blessed;
**** our marriages are blessed;
**** our finances are blessed;
**** our relationships are blessed;
**** our businesses are blessed;
**** our jobs are blessed;
**** our children are blessed;
**** our grandchildren are blessed;
**** our parents are blessed;
**** our siblings are blessed;
**** our ministries are blessed;
**** our decisions are blessed;
**** our friends are blessed.
**** Mortgages are paid and debts canceled; our hearts' desires are on the way;


According to YOUR perfect will and plan for our lives.
YOU SAID YOU'D NEVER FORSAKE US! IN JESUS' NAME!
AMEN!

asante sasa dada Brenda kwa kunitumia zidi kubarikiwa
 

Friday, January 21, 2011

KUBALI KUWA MLAWI

The Brooklyn Tabernacle Choir is currently accepting applications for membership. If you are interested, and are a member or in the process of becoming one, please apply online at:www.brooklyntabernacle.org/choirapp


The Brooklyn Tabernacle Music Staff

Haya kwa wale wenye karama ya kuimba au kama unajijua unayo sauti kama chiriku au hata ya kumtoa nyoka pangoni jiunge basi kuwa member wa Brooklyn Tabernacle Choir ukamwimbie Bwana maana kwenye sifa Mungu huwapo kwani yeye anapenda nyimbo za sifa na shukrani kuliko kitu kiwayo chote naye hushuka nakuja kuweka makao hivyo hima jiandikishe tumwimbie Bwana Sifa (kubali kuwa Mlawi) Soma 2 M/ Nyakati 5: 11-14

BWANA YESU ANAKUMBIA NINI LEO HII

Mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwone haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.

Tuesday, January 18, 2011

PATA PUMZIKO LA KWELI KATIKA MWAKA HUU

BWANA YESU ASIFIWE SANA SANA NIMERUDI KWA UPYA NA MAMBO MAPYA, MWAKA MPYA NA KARNE MPYA.

Neno la Mungu linasema hivii ....................
"NJOONI KWANGU NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KULEMEWA NA MIZIGO  NAMI NITAWAPUMZISHA"

MWAKA huu ni mwaka wa urejesho wa amani, furaha, na nguvu mpya ya kushinda majaribu, vikwazo, vifungo mbalimbali viletwavyo na nguvu za giza za yule mwovu shetani. Hivyo basi mpendwa hakuna haja ya kubeba mizigo ya dhambi, kutokusamehe, uchungu n.k. tujifunze kusamehe na kutokuweka vinyongo songa mbele acha kuwabeba watu wakati huo umekwisha samehe na usonge mbele uuone wema na mkono wa Bwana katika maisha yako kwa mwaka huu wote na hata milele. Usikubali kujaribiwa na yule mwovu bibilia inatuambia hivii mshitaki wetu yule mwovu shetani ni kama simba angurumaye akizunguka huku na huko akitafuta mtu wa kummeza hivyo basi tujiepushe naye tumshinde kwa kujifunza kusamehe, kutolipiza  visasi, acha hasira zisizo na mpango, kataa chuki, na mambo mengine kama hayo tusome NENO LA MUNGU KWA BIDII KILA SIKU ambalo litafanya Roho Mtakatifu aweke makao katika mioyo yetu.

Acha kusumbuka na kuteseka njoo kwa Yesu tua mzigo wako kwake upate furaha na amani ya kweli katika maisha yako. Maana kwenye amani Roho Mtakatifu huwepo na unajua palipo Roho wa Bwana yote yanawezekana hata yale ambayo kwa akili za kibinadamu yalikuwa hayawezekani kwake yanawezekana. Yesu anatuambia kuwa tumpatie mizigo yetu iliyo mizito atupe wa kwake ambao ni mwepesi sasa kwa nini mpendwa ujibebeshe mizigo ambayo hakusaidii wala haikupi faida yoyote sana sana ni hasara na maumivu tele tele njoo kwa Yesu upate pumziko la milele.

Pia Yesu anasema tusivunje mioyo kwani kwa kupitia yeye tunayashinda yote, aliushinda ulimwengu na sisi tutaushinda. Hakuna kurudi nyuma wala kulegea viungo tuuvae ujasiri tusimame imara katika mwaka huu tuone penzi la kweli, uweza na nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na jinsi mkono wake ulivyo Mkuu.

Nawapenda wote na amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu.
Uwe na wakati mzuri. Amen

Godly Goals Require Faith

Without faith it is impossible to please God …. Hebrews 11:6 (NIV)
"We must set goals that are bigger than ones we can reach on your own."
Godly goals are set through faith. The Bible says, “Without faith, it is impossible to please God.” In order to please God, we must set goals that require faith.
What does this mean? It means we must set goals that are bigger than ones we can reach on your own.
For instance, I want you to set a health goal for this year. As I’ve said, if you don't have a health goal, then your goal is to stay the same or get worse. To move forward – to get healthier -- you must set a health goal.
Let’s say you need to take off some weight. If you say, ‘My goal is to lose one pound’ – well … you know you can do better than that. Set a goal based on what God tells you to do and I have no doubt that will be a goal that will require you to remain dependent upon Jesus.
You haven't believed God until you've attempted to do something that can't be done unless his power is at work in your life.

Tuesday, January 11, 2011

MAOMBI YA MWAKA MPYA

BABA NINALITUKUZA JINA LAKO NASEMA ASANTE SANA BWANA KWA KUWEZA KUTULINDA NA KUTUPA AMANI, ASANTE KWA ULINZI WAKO, BARAKA ZAKO NA UPENDO USIO NA KIPIMO, ASANTE KWA KUTUPA TUMAINI NA FURAHA KWA MWAKA ULIOPITA NAKUSHUKURU BWANA KWA KUTUVUSHA SALAMA NA SISI KUWEZA KUUONA TENA MWAKA 2011 ANZA NASI TENA KWA UPYA BWANA KATIKA MWAKA HUU NA KARNE HII MPYA JEHOVA ENDELEA KUTUTIA NGUVU, TUPE AMANI, FURAHA, UTU WEMA, FADHILI ZAKO, BUBUJIKO LA ROHO WAKO MTAKATIFU, NA UPENDO WA KWELI UUMBIKE NDANI YA MAISHA YETU, TUNDA LA ROHO MTAKATIFU LIZIDI KUUMBIKA NDANI YETU, TUPE ROHO YA UNYENYEKEVU NA MOYO ULIOPONDEKA, NA UWEPO WAKO BWANA USITUONDOKEE, BARIKI KAZI ZA MIKONO YETU, BARIKI WATOTO WETU NDOA ZETU, FAMILIA ZETU, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA HATA MAJIRANI ZETU WOTE  KWA MWAKA HUU MPYA NA KARNE NYINGINE BWANA, BARIKI KUINGIA KWETU NA KUTOKA KWETU, TUNASIHI KIBALI MBELE YAKO BWANA NA KWA WANADAMU PIA, TUNAOMBA KIBALI CHAKO POPOTE TUINGIAPO NA TUNAPOKANYAGA BWANA ONEKANIKA WEWE BWANA KILA TUINGIAPO, MANENO YA VINYWA VYETU JEHOVA YATAWALIWE NA WEWE TUWE NI WATU WA KUBARIKI KWA MWAKA HUU NA SIO WA KULAANI TUWE NI WATU WA KUTIA MOYO NA KUWALETA WATU KWAKO EE BWANA, ROHO MTAKATIFU FANYA MAKAO KATIKA VILINDI VYA MIOYO YETU. TEMBEA NASI TUSHIKE MKONO UTUONGOZE WEWE KWA MWAKA HUU WOTE NA HATA MILELE NA MILELE NINAOMBA HAYA KUPITIA JINA LA MWANAO MPENDWA YESU KRISTO  ALIYE BWANA NA MWOKOZI KATIKA MAISHA YETU. AMEN AMEN AMEN

HERI YA MWAKA MPYA WENYE BARAKA TELE NA AMANI YA BWANA IWATAWALE KATIKA MAISHA YENU NA FAMILIA ZENU KWA UJUMLA
 MZIDISHIWE BARAKA NA BWANA YESU KRISTO ALIYE HAI

HAPPY NEW YEARRRRRRRRRRRR.