Sunday, January 30, 2011

RAHA YA UWOKOVU

Ukiwa ndani ya Yesu kuna raha  mpendwa asikwambie mtu, yote yanawezekana kwa Bwana hata yale ambayo kwa akili za kibinadamu ni magumu kuwezekana ili maradi tu umwamini. "Biblia inasema hivi, yote yawezekana kwake yeye aminie". Nami na mwamini Mungu nimeuona mkono wake ndani ya maisha yangu, amani niliyonayo leo na furaha vyote nimevipata kutoka kwake yeye. Ananishindia siku hadi siku kila kitu kwangu ni shwari kwani najua ninaye mwenye uweza wote aliye mbele yangu, anayenipenda aliyenishika mkono anayeijua kesho yangu tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu Bwana Mungu Yesu Kristo pamoja na Roho wake Mtakatifu naamini hata niacha kamwe, ananikumbatia na kunitia nguvu. Furaha, amani, utulivu, nguvu, na uweza ninavyo leo kwa sababu siku moja niliamua kuwa nataka kuwa na mshauri, mpenzi, mwalimu, kiongozi, baba Yesu Kristo ndani ya maisha yangu naye bila hiyana akanikubali akanivuta karibu nae akaniambia mwanangu karibu nyumbani hapa umefika yale uliyopitia na kuyaona hapo kabla hayatakupata tena kamwe na wala hautayaona. Kama alivyowaambia wana wake wa Israel kuwa hao Wamisri mnaowaona leo hamtawaona tena kamwe na mimi akaniambia kuwa  Wamisri waliokuwa katika maisha yangu sitawaona tena kamwe nami nina amini hivyo na zaidi. 

Wewe je unataka kuonja furaha na amani hii niliyo nayo mimi leoo?Njoo kwa Yesu leo ndugu yangu mkubali awe Bwana na Mwokozi katika maisha yako nawe utapata penzi la kweli lisilo na mawaa. Yale yote yaliomwiba kwako yatakwisha na hautayapata wala kuyaona tena.

Nampenda Yesu sana na Yeye anakupenda pia karibu upate furaha ya kweli na tufurahi pamoja.

No comments: