Thursday, February 24, 2011

NAMSHUKURU MUNGU

Nazidi kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake katika maisha yangu amenipa nguvu na tumaini katika siku zote za maisha yangu. Hakuniacha kamwe amekuwa nami siku zote katika mapito yoyote niliyopitia alikuwa nami hakuniacha hadi siku hii ya leo natimiza miaka kadhaa hakuwahi kuaniacha bali alinikumbatia na kunishika mkono na kunipa penzi lake la kweli na kunitia moyo akinihakikishia maisha ya amani na furaha yenye baraka. Nami nazidi kushuhudia sasa kuwa nimeuona mkono wake ulivyo mkuu na uweza wake wa ajabu umetenda mengi mema na uwepo wake umenifunika mimi na familia yangu kwa jinsi ya kipekee kwa kweli nina kila sababu ya Kumshukuru na kutangaza fadhili zake; nazidi kumtukuza kwa maana anastahili sana sana.

Asante Mungu wangu kwa kunipenda, uhimidiwe Bwana wangu.