Friday, February 11, 2011

NI NANI ATAKAYEKUTENGA NA UPENDO WA MUNGU?

WARUMI 8:35-39

NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO? JE NI DHIKI, AU SHIDA, AU ADHA, AU NJAA,  AU UCHI, AU HATARI, AU UPANGA?

BIBLIA INATUNAAMBIA KUWA KATIKA MAMBO HAYO YOTEEE .................
LAKINI KATIKA MAMBO HAYO YOTE TUNASHINDA, NA ZAIDI YA KUSHINDA, KWA YEYE ALIYETUPENDA.
KWA MAANA NIMEKWISHA KUJUA HAKIKA YA KWAMBA, WALA MAUTI, WALA UZIMA, WALA MALAIKA, WALA WENYE MAMLAKA , WALA YALIYOPO, WALA YATAKAYOKUWEPO, WALA WENYE UWEZO, WALA YALIYO JUU, WALA YALIYO CHINI, WALA KIUMBE KINGINECHO CHOTE HAKITAWEZA KUTUTENGA NA UPENDO WA MUNGU ULIO KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU.

SIFA NI KWA BWANA

NALIINUA JINA LAKO BWANA WANGU NAKUPA SIFA SANA MAANA UNASTAHILI, UNASTAHILI KUABUDIWA UNASTAHILI KUTUKUZWA WEWE NI MUNGU MKUU, WEWE NI MFALME WA WAFALME, BWANA NI MWEMA SANA MUNGU MWENYE KUSIFIWA MUNGU MWENYE UPENDO. UPENDO WAKO NI WA PEKEE NALIINUA JINA LAKO, POKEA SIFA BWANA, NAKUTUKUZA BWANA WANGU UWEZA WAKO NI WA AJABU, UHESHIMIWE, UNASTAHIL!I UNASTAHILI! KUTUKUZWA.

MATENDO YAKO NI YA AJABU, MKONO WAKO NI MKUU SANA ASANTE KUNIPENDA BWANA, ASANTE KUNIUMBA, ASANTE KUNIPA NEEMA YAKO, ASANTE KUNILINDA ASANTE KWA KUWA UMEKUWA MWAMINIFU NDANI YA MAISHA YANGU UTUKUFU NA HESHIMA NI KWAKO BWANA, UAMINIFU WAKO NI WA PEKEE NAKUPENDA SANA BWANA, POKEA SIFA NA HESHIMA UABUDIWE! UABUDIWE! BWANA WANGU.

HALELUYAH!   HALELUYAH!