Nitayasimulia matendo yake ya ajabu maana anastahili yeye ni mwaminifu na tena ni mwema sana utukufu na heshima ni kwake. Yeye ni mkuu sana yeye ni wa pekee anatenda maajabu ndani ya maisha yetu kila iitwapo leo. Mkono wake ni mkuu sana nao hutuongoza kila tuendapo, katika kila kona ya maisha yetu uko pamoja nasi na yeye hutuwazia yaliyo mema kila siku anatupenda upeo; upendo wa Agape anatupa tumaini siku zote za maisha yetu. Tuzidi kumpa sifa na utukufu na shukrani kwa maana anastahili.
Unastahili kuabudiwa Bwana wangu, unastahili kutukuzwa, unastahili kupewa sifa, utukufu na heshima ni kwako wewe, uhimidiwe, uinuliwe, ninakusujudia Bwana wangu nainua mikono yangu kwako kwa ishara ya kusarenda kwamba bila wewe mimi siwezi, bila wewe mimi si kitu ni wewe tu ndio kimbilio langu, ngome yangu na msaada wangu. Hakuna aliye mkuu kama wewe hakuna Mungu kama wewe hakuna mfalme kama wewe ni wewe peke yako unayestahili uabudiwa na kutukuzwa Mungu Mkuu Bwana wangu.
Naliinua jina la mwana wako wa pekee Yesu Kristo, jina lililo kuu, jina lipitalo majina yote lenye uweza wote, lenye neema litetalo uzima kwa jina hilo tumepata kukombolewa nakushukuru sana sana Bwana wangu. Nakurudishia sifa na utukufu maana unastahili. Haleluya Bwana; Haleluya Mungu wangu uhimidiwe Bwana asante sana na nashukuru kwa kila jambo ndani ya maisha yangu nakushukuru Bwana sana.