Baba Ninakushukuru kwa wema na fadhili zako nasema asante kwa kunipenda kwa pendo la kipekee pendo la agape, uhimidiwe maana unastahili, utukuzwe kwa maana unastahili upewe sifa kwa maana unastahili unastahili! unastahili! unastahili! Bwana wangu. Nakupenda sana sana Bwana asante kunipenda asante kwa kunibariki asante kwa kila kilicho katika maisha yangu. Bila wewe mimi siwezi ni kwa uweza wako na nguvu zako mimi niko hivi nilivyo leo hii asante sana Bwana wangu. Mkono wako ni mkuu sana umenitangulia katika kila jambo ndani ya maisha yangu asante sana Bwana nakupenda sana Mungu wangu. Sina Mungu mwingine ila ni wewe sina Bwana mwingine ila ni wewe na sina kiongozi mwingine katika maisha yangu ila ni wewe tu Bwana ni wewe tu Mungu wangu ni wewe peke yako ndio tegemeo langu ngome yangu na uzima. Uhimidiwe Mungu wangu uhimidiwe Mfalme wangu uhimidiwe ewe uliye kimbilio langu, utukufu na heshima ni kwako Bwana wangu na Mungu wangu. Amen Amen Amen