Kwa wale tunaowapa watoto wetu time out badala ya fimbo tunakoseaa?????
Biblia inasema kuwa "YEYE ASIYETUMIA FIMBO YAKE HUMCHUKIA MWANAE, BALI YEYE AMPENDAYE HUMRUDI MAPEMA" Mithali 13:24
Haya ndugu sisi tunaosema kuwa mtoto hachapwi tunampa time out kwenye kona tunakosea jambo hili ina maana wewe humpendi mwanao? na kila neno lilioandikwa kwenye Biblia ni amin na kweli halisemi uongo.
Mimi nasema ni kweli watoto bila fimbo kidogo hawasongi bwana ndio maana na watoto wa siku hizi heshima kwa wazazi wao hawana utakuta mtoto anamjibisha mzazi wake kama nini sijui hawawaheshimu wazazi kwa sababu ya nini hukuwahi kumrekebisha kwa fimbo. Kwani Mfalme Suleiman anasema hivi "UJINGA UMEFUNGWA NDANI YA MOYO WA MTOTO, LAKINI FIMBO YA ADHABU ITAUFUKUZIA MBALI. Mithali 22:15
Hivyo basi usipomchapa mwanao japo kidogo ujinga hautatoka kwake kamwe ndio maana basi wakati mwingine watoto wanatudharau, wanakuwa hawatuheshimu kwa sababu gani ya kukosa kuutoa ujinga ndani ya moyo wake. Lakini kumchapa mwanao kusiwe ni kwa kumchapa chapa tu kila mara bali pale anapokuwa amekosea na kosa lenyewe liwe linaonekana sio unahisi au una mahasira yako either kutoka kazini au mume /mke mmegombana basi hasira zote zinaishia kwa mtoto au hata mtoto akivunja glass basi unachukua fimbo unaanza kumnyuka. Bahati mbaya huwa zinakuwepo jamani kwani hata sisi wazazi wakati mwingine umeshika glass vibaya imekuponyoka ikaanguka basi lazima itapasuka wewe nani atakuchapa? kuna makosa mengine unaoona hii ni tabia ambayo ukiiacha itakuwa mbaya na itamwaribia mwanao mwelekeo wa maisha yake hapo baadaye hivyo fimbo inamrekebisha anaanza kuwa mtu safi.
Cha msingi ni kuwachapa watoto wetu pale wanapofanya makosa na kosa lenyewe la kuoneka na si la kuonea au kumalizia hasira. Na umweleze kosa lake ni nini ili ajue na siku nyingine hatarudia kwani pia asipojua kosa lake inakuwa ni yale yale baadaye anakuwa sugu na hata hiyo fimbo haiogopi na wewe pia hakuheshimu. Tuwe makini sana na TUSIWANYIME FIMBO!TUSIACHE KUWARUDI PALE WANAPOKOSEA NA ZAIDI SANA KUWAOMBEA.
Pia Baba yetu wa Mbinguni kwa vile anatupenda huwa anaturudi, Biblia inatuambia kuwa Bwana huwarudi wale awapendao hivyo wakati mwingine ukiona mambo ndivyo sivyo anza kujichunguza wapi ulipokosea si kwa kujihukumu bali kwa kutaka kutambua kosa na kujirekebisha na kutokurudia tena kwani wakati mwingine si shetani bali ni Bwana anaona akunyoroshe kidogo ili ukae katika mstari unaotakiwa kwa vile ANAKUPENDA HATAKI UPOTEE.
Barikiwa
Soma Mithali 3:11-12