Tuesday, November 23, 2010

WAPENDA KOFIA ( ZA KANISANI) MAMA RWAKATARE STYLE

Haya wapendwa kwa wale wanaopenda kuvaa kofia mimi naita Mama Rwakatare style kwa sababu huyu Mtumishi wa Bwana anapenda sana kuvaa akiwa kanisani na baadhi ya waumini wake chagua yako uipendayo sasa.






 



barikiwa

VAZI LA KWENDEA KANISANI

Kwa wale wapenda makofia hizi picha zitawasaidia lakini si lazima kuvaa kofia kama haupendi vaa suit yako namna hii jimwaye kanisani.

Kofia si lazima kama inakusumbua achana nayo suit yatosha


Nadhani mnaona style ya nyuma ya hii suit si ya kwenye harusi au send off hili ni vazi la kwendea kanisani.

Hii suit kwa bongo Dar es salaam inafaa sana joto likizidi unatoa koti unaonekana namna hiyo kwenye picha ndogo. Kama hauoni tabu basi pendeza na koti lako msifu Bwana bila kuchoka.
Nimeipenda hii lakini mimi si mtu wa kofia hivyo naweza vaa bila kofia na nikatoka safiii kabisa jaribu uone.

Hizi si sare za harusi jamani ni vazi la kwendea kanisani la heshima kabisaa na sio nzito kwa TZ yawezekana kuvalika.
Watakao lalamika joto Dar jamani sasa sidhani kama hapo una la kusema


Ukipenda suruali haya, skirt twende, joto kali vua koti uonekane namna hiyo hapo.
nimeipenda
Wapenda suruali kama mimi hatukubaki nyuma ndio kama hivi tena na kanisani tunaingia kumsifu na kumshangilia Bwana tukiimwaga mioyo yetu.
Binti naye aweza kuvaa hivii.


picha zaidi zaja wakaka na wababa sijawasahau nao natoa zao karibuni.
mabinti kaeni sawa zenu zaja.
african style nayo yaja
enjoy