Tuesday, January 18, 2011

PATA PUMZIKO LA KWELI KATIKA MWAKA HUU

BWANA YESU ASIFIWE SANA SANA NIMERUDI KWA UPYA NA MAMBO MAPYA, MWAKA MPYA NA KARNE MPYA.

Neno la Mungu linasema hivii ....................
"NJOONI KWANGU NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KULEMEWA NA MIZIGO  NAMI NITAWAPUMZISHA"

MWAKA huu ni mwaka wa urejesho wa amani, furaha, na nguvu mpya ya kushinda majaribu, vikwazo, vifungo mbalimbali viletwavyo na nguvu za giza za yule mwovu shetani. Hivyo basi mpendwa hakuna haja ya kubeba mizigo ya dhambi, kutokusamehe, uchungu n.k. tujifunze kusamehe na kutokuweka vinyongo songa mbele acha kuwabeba watu wakati huo umekwisha samehe na usonge mbele uuone wema na mkono wa Bwana katika maisha yako kwa mwaka huu wote na hata milele. Usikubali kujaribiwa na yule mwovu bibilia inatuambia hivii mshitaki wetu yule mwovu shetani ni kama simba angurumaye akizunguka huku na huko akitafuta mtu wa kummeza hivyo basi tujiepushe naye tumshinde kwa kujifunza kusamehe, kutolipiza  visasi, acha hasira zisizo na mpango, kataa chuki, na mambo mengine kama hayo tusome NENO LA MUNGU KWA BIDII KILA SIKU ambalo litafanya Roho Mtakatifu aweke makao katika mioyo yetu.

Acha kusumbuka na kuteseka njoo kwa Yesu tua mzigo wako kwake upate furaha na amani ya kweli katika maisha yako. Maana kwenye amani Roho Mtakatifu huwepo na unajua palipo Roho wa Bwana yote yanawezekana hata yale ambayo kwa akili za kibinadamu yalikuwa hayawezekani kwake yanawezekana. Yesu anatuambia kuwa tumpatie mizigo yetu iliyo mizito atupe wa kwake ambao ni mwepesi sasa kwa nini mpendwa ujibebeshe mizigo ambayo hakusaidii wala haikupi faida yoyote sana sana ni hasara na maumivu tele tele njoo kwa Yesu upate pumziko la milele.

Pia Yesu anasema tusivunje mioyo kwani kwa kupitia yeye tunayashinda yote, aliushinda ulimwengu na sisi tutaushinda. Hakuna kurudi nyuma wala kulegea viungo tuuvae ujasiri tusimame imara katika mwaka huu tuone penzi la kweli, uweza na nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na jinsi mkono wake ulivyo Mkuu.

Nawapenda wote na amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu.
Uwe na wakati mzuri. Amen

No comments: