Baadhi ya watu husemaaa"Kuokoka ni ushamba, ukiokoka ina maana unayo matatizo, umefulia hauna jipya" je hii ni kweli?
Laiti watu wa namna hii wangemjua Mungu wangejua furaha na uzuri wa kuokoka wasingesema hivyo. Bibilia inasema Dunia na vyote vijazavyo ni mali ya Bwana Dhahabu fedha nk ni mali yake Baba yetu sasa je iweje mtuite tuliofulia? sisi walokole tumejaa amani, tuna furaka ya kweli kutoka ndani ya moyo. Maisha yetu yana msimamo na mafanikio yetu yanaanzia ndani kwenda nje, tumebarikiwa ktk kila nyaja. Sisi ni watoto wa mfalme tangu lini prince au princess akawa amepauka / amefulia? jamani lazima alivyonavyo baba na sisi pia tunavyo na chochote tukitakacho twakipata tukimwomba baba anatupa bila hiyana na vingine hata tusipoomba anatupatia yeye mwenyewe kadri apendavyo. Njoo uonje uzuri wa kuokoka hakika hautajuta.
No comments:
Post a Comment