Thursday, February 24, 2011

NAMSHUKURU MUNGU

Nazidi kumshukuru Mungu kwa wema na fadhili zake katika maisha yangu amenipa nguvu na tumaini katika siku zote za maisha yangu. Hakuniacha kamwe amekuwa nami siku zote katika mapito yoyote niliyopitia alikuwa nami hakuniacha hadi siku hii ya leo natimiza miaka kadhaa hakuwahi kuaniacha bali alinikumbatia na kunishika mkono na kunipa penzi lake la kweli na kunitia moyo akinihakikishia maisha ya amani na furaha yenye baraka. Nami nazidi kushuhudia sasa kuwa nimeuona mkono wake ulivyo mkuu na uweza wake wa ajabu umetenda mengi mema na uwepo wake umenifunika mimi na familia yangu kwa jinsi ya kipekee kwa kweli nina kila sababu ya Kumshukuru na kutangaza fadhili zake; nazidi kumtukuza kwa maana anastahili sana sana.

Asante Mungu wangu kwa kunipenda, uhimidiwe Bwana wangu.

Sunday, February 13, 2011

UHIMIDIWE BWANA

Nitayasimulia matendo yake ya ajabu maana anastahili yeye ni mwaminifu na tena ni mwema sana utukufu na heshima ni kwake. Yeye ni mkuu sana yeye ni wa pekee anatenda maajabu ndani ya maisha yetu kila iitwapo leo. Mkono wake ni mkuu sana nao hutuongoza kila tuendapo, katika kila kona ya maisha yetu uko pamoja nasi na yeye hutuwazia yaliyo mema kila siku anatupenda upeo; upendo wa Agape anatupa tumaini siku zote za maisha yetu. Tuzidi kumpa sifa na utukufu na shukrani kwa maana anastahili.

Unastahili kuabudiwa Bwana wangu, unastahili kutukuzwa, unastahili kupewa sifa, utukufu na heshima ni kwako wewe, uhimidiwe, uinuliwe, ninakusujudia Bwana wangu nainua mikono yangu kwako kwa ishara ya kusarenda kwamba bila wewe mimi siwezi, bila wewe mimi si kitu ni wewe tu ndio kimbilio langu, ngome yangu na msaada wangu. Hakuna aliye mkuu kama wewe hakuna Mungu kama wewe hakuna mfalme kama wewe ni wewe peke yako unayestahili uabudiwa na kutukuzwa Mungu Mkuu Bwana wangu.
Naliinua jina la mwana wako wa pekee Yesu Kristo, jina lililo kuu, jina lipitalo majina yote lenye uweza wote, lenye neema litetalo uzima kwa jina hilo tumepata kukombolewa nakushukuru sana sana Bwana wangu. Nakurudishia sifa na utukufu maana unastahili. Haleluya Bwana; Haleluya Mungu wangu uhimidiwe Bwana asante sana na nashukuru kwa kila jambo ndani ya maisha yangu nakushukuru Bwana sana.

Friday, February 11, 2011

NI NANI ATAKAYEKUTENGA NA UPENDO WA MUNGU?

WARUMI 8:35-39

NI NANI ATAKAYETUTENGA NA UPENDO WA KRISTO? JE NI DHIKI, AU SHIDA, AU ADHA, AU NJAA,  AU UCHI, AU HATARI, AU UPANGA?

BIBLIA INATUNAAMBIA KUWA KATIKA MAMBO HAYO YOTEEE .................
LAKINI KATIKA MAMBO HAYO YOTE TUNASHINDA, NA ZAIDI YA KUSHINDA, KWA YEYE ALIYETUPENDA.
KWA MAANA NIMEKWISHA KUJUA HAKIKA YA KWAMBA, WALA MAUTI, WALA UZIMA, WALA MALAIKA, WALA WENYE MAMLAKA , WALA YALIYOPO, WALA YATAKAYOKUWEPO, WALA WENYE UWEZO, WALA YALIYO JUU, WALA YALIYO CHINI, WALA KIUMBE KINGINECHO CHOTE HAKITAWEZA KUTUTENGA NA UPENDO WA MUNGU ULIO KATIKA KRISTO YESU BWANA WETU.

SIFA NI KWA BWANA

NALIINUA JINA LAKO BWANA WANGU NAKUPA SIFA SANA MAANA UNASTAHILI, UNASTAHILI KUABUDIWA UNASTAHILI KUTUKUZWA WEWE NI MUNGU MKUU, WEWE NI MFALME WA WAFALME, BWANA NI MWEMA SANA MUNGU MWENYE KUSIFIWA MUNGU MWENYE UPENDO. UPENDO WAKO NI WA PEKEE NALIINUA JINA LAKO, POKEA SIFA BWANA, NAKUTUKUZA BWANA WANGU UWEZA WAKO NI WA AJABU, UHESHIMIWE, UNASTAHIL!I UNASTAHILI! KUTUKUZWA.

MATENDO YAKO NI YA AJABU, MKONO WAKO NI MKUU SANA ASANTE KUNIPENDA BWANA, ASANTE KUNIUMBA, ASANTE KUNIPA NEEMA YAKO, ASANTE KUNILINDA ASANTE KWA KUWA UMEKUWA MWAMINIFU NDANI YA MAISHA YANGU UTUKUFU NA HESHIMA NI KWAKO BWANA, UAMINIFU WAKO NI WA PEKEE NAKUPENDA SANA BWANA, POKEA SIFA NA HESHIMA UABUDIWE! UABUDIWE! BWANA WANGU.

HALELUYAH!   HALELUYAH!

Friday, February 4, 2011

NYAKATI ZA MWISHO ZIMEKARIBIA

MAMBO YANAYOENDELEA HUKO MISRI NI UTABIRI WA NABII ISAYA ALIYO TABIRI JUU YA MISRI UKISOMA KATIKA ISAYA 19: 1 ..... UTAONA JINSI NABII ISAYA ALIVYOTABIRI JUU YA MISRI. HABARI YENYEWE INAJITOSHELEZA UKISOMA KWA MAKINI UTAELEWA.

SASA JE WEWE UKO TAYARI? UMESHAANDA MOYO WAKO? KWANI ISHARA ZOTE SASA ZINATIMIA ZILIZONENWA NA MANABII KATIKA KITABU KITAKATIFU CHA MUNGU. UNASUBIRI NINI ANZA SASA FANYA HIMA KUMTAFUTA BWANA AWE MWOKOZI WA MAISHA YAKO ILI UWEZE KUUNGANA NA YESU KATIKA UFALME WAKE KWA MAANA ANASEMA BILA YEYE HAUWEZI KAMWE KUINGIA KATIKA UFALME WAKE ACHA MAMBO YA DUNIA HII , ACHA NJIA ZAKO MBAYA MKUBALI BWANA YESU AMBAYE NDIE NJIA 

YESU ANASEMA HIVII MIMI NDIMI NJIA KWELI NA UZIMA MTU HAJI KWA BABA ILA KWA NJIA YA MIMI. 

Egypt's Protests Day of Anger Riots 25 Jan 2011 Demonstrations Rare Raw ...




UTABIRI WA NABII ISAYA 19:1 HEBU SOMA NA UANGALIE NA HII. KAA TAYARI USIFANYE MCHEZO NYAKATI ZA MWISHO ZIMEKARIBIA