Wednesday, November 10, 2010

JE WAJUA KUWA UNAMWIBIA MUNGU?

BWANA MUNGU ANASEMA HIVII,

Tokea siku za Baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema Bwana wa Majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?
JE MWANADAMU ATAMWIBIA MUNGU? LAKINI NINYI MNANIIBIA MIMI, MWASEMA TUMEIBA KWA NAMNA GANI? MMENIIBIA DHAKA NA DHABIHU. NINYI MMELAANIWA KWA LAANA, MAANA MNANIIBIA MIMI, NAAM TAIFA HILI LOTE.
LETENI ZAKA KAMILI GHALANI, ILI KIWEMO CHAKULA KATIKA NYUMBA YANGU, MKANIJARIBU KWA NJIA HIYO, ASEMA BWANA WA MAJESHI MJUE KAMA SITAWAFUNGULIA MADIRISHA YA MBINGUNI NA KUWAMWAGIENI BARAKA, HATA ISIWEPO NAFASI YA KUTOSHA AU LA. NAMI KWA AJILI YENU NITAMKEMEA YEYE ALAYE, WALA HATAHARIBU MAZAO YA ARDHI YENU, WALA MZABIBU WENU HAUTAPUKUTISHA MATUNDA YAKE KABLA YA WAKATI WAKE KATIKA MASHAMBA ASEMA BWANA WA MAJESHI. NA MATAIFA YOTE YATAWAITENI HERI, MAANA MTAKUWA NCHI YA KUPENDEZA SANA, ASEMA BWANA WA MAJESHI. Soma Malaki 3:7-12

Mpendwa katika Bwana Je wewe umeshaona jinsi gani ambavyo unamwibia Mungu? Umeshaona ni kwa jinsi gani basi neno la Nabii Hagai 1:5:7 linavyotenda kazi ndani ya maisha yako? Kwani Nabii Hagai anakwambia hivii zitafakarini njia zenu, Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo, mnakula lakini hamshibi............ na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka toboka.
Unaona sasa ni kwa jinsi gani unavyokuwa haufanikiwi? Jibu ni kwamba umemwibia Mungu hivyo na yeye hakuweza kumkemea yule adui alae mshahara wako, mazao yako, kazi yako ya mikono inakuwa haisongi mbele kwa sababu umemwibia Mungu. Tubadilike wapendwa tuanza kutoa zaka zilizo kamili ili Bwana Mungu wetu atufungulie madirisha ya mbinguni tupate baraka na pia amkemee yule adui alae asiguse kazi zetu za mikono.
Naamini kwa somo hili japo nimefafanua kidogo litakujenga na kukufanya ubadilike na kuanza kutoa zaka na dhabihu kwa Mungu ili mshahara wako usiingie ktk mfuko uliotoboka toboka. Japo shetani naye hajalala usingizi anasubiri mlangoni ili akuzuie usipate baraka kutoka kwa Mungu uzidi kumtumikia kwani ukianza kujiandaa tu kutoa zaka na yeye yuko anakupa mipango mingi ya matumizi ya kipato chako( anakupangia budget ya mwezi mzima pamoja na ile zaka uliyokuwa utoe hivyo unabaki mtupu) au kama ni vitu anakwambia kuwa hiki utakihitaji tena baadae au ni kizuri sana huwezi kukitoa hivyo unamtolea Bwana vile vilivyo dhoofu. Tunahitaji maombi ili kuweza kuvuka katika hili eneo hili  kwani limewakalia watu wengi na wengi wetu tupo kwenye vifungo katika hili swala. Bwana Mungu atuhurumie na atuwezeshe tuwe na moyo wa utoaji wa zaka na dhabihu kwa moyo mkunjufu.
MAOMBI YA KUMAANISHA NDIO YATAKAYOWEZA KUTUWEZESHA KULISHINDA HILI JARIBU.

No comments: