Monday, September 3, 2012

NAMSHUKURU MUNGU

Namshukuru Mungu sana kwa wema na fadhili zake anazonitendea kila iitwapo leo nimeuona wema wake katika maisha yangu hakuna siku aliyeniacha mpweke bali siku zote alikuwa nami akinitia moyo akinitetea na kunipa muongozo sahihi wa maisha yangu. Kwa kweli namshukuru Mungu sana na kwa upendo wake mkuu.Uinuliwe baba, uhimidiwe, upewe sifa kwa maana wastahili hakuna mwingine kama wewe na hatakuwepo wa kulinganishwa na wewe wewe ni baba wewe ni Bwana wangu , wewe ni Mungu wangu sina Mungu mwingine ila ni wewe asante kwa kunipenda asante kwa kunikumbatia asante kwa kunifunika kwa wema wako, jina lako ni kuu sana na jina lako libarikiwe. Ameni

No comments: