Friday, September 3, 2010

MAOMBI YANGU KWAKO SIKU HII YA LEO

Bwana Mungu wetu Mfalme wa Amani, ninakutukuza ninakupa heshima na utukufu. Asante kwa kuwa mwema kwetu na uaminifu wako ndani ya maisha yetu.Asante kwa kutupa kibali katika siku hii nzuri na njema ya leo. Wabariki wana wako baba panda kitu kipya ndani ya maisha yao siku hii ya leo. Bariki kazi za mikono yao, wabariki kila waingiapo na watokapo, chochote watakachofanya au kugusa kwa siku hii ya leo kiwe kimebarikiwa. Waepushe na kila hila za yule mwovu na kazi zake, waondolee magonjwa, hofu, huzuni, kukosa amani, uchungu. Wape furaha ya kweli, amani itokayo kwako, tabasamu la kweli kutoka ndani ya mioyo yao, panda ujasiri wako ndani yao. Roho Mtakatifu wape hekima itokayo kwako, maarifa  na ufahamu wako. Linda familia, watoto na ndoa zao. Nashukuru baba kwa maana maombi haya yamepata kibali machoni pako katika jina la mwanao mpendwa Yesu Kristo. Amen, Amen, Amen.

No comments: