Friday, September 3, 2010

VAZI LIPI LAFAA HASA KWENDEA KANISANI? TUELIMISHANE

Wapendwa jamani hili ni jambo ambalo linawasumbua sana watu wengi na wengine hata wanadiriki kutokwenda kanisani siku nyingine sababu kubwa sina nguo ya kuvaa. Naomba tusaidiane tuelimishana kuhusu hili kwa sababu mimi ninaamini kuwa Mungu wetu haangalii mavazi  umbo, utajiri wala chohote kiwayo chote ila yeye anaangalia MOYO wako. 1Samweli 16:7

Sasa je ni vyema kwa waumini kumnyooshea kidole mtu aliyevaa nguo fupi au suruali au jeans akaenda nayo kanisani? (naongelea kwa mwanamke) Mfano kama nimeokoka nikivaa jeans kanisani au nguo fupi na (kijana wa kiume) akavaa suruali chini ya makalio inamaanisha kuwa mimi sijaokoka? Unawezaje basi kutambua kuwa mimi nimeokoka au la kwa kuangalia mavazi yangu? Au kama hata sijaokoka mimi ni muumini wa kawaida napenda kwenda kanisani napenda kujifunza kuhusu neno la Mungu je utanitenga na kuanza kunisengenya kuniangalia jicho pembe kuwa mimi sifai kuingia kanisani kwa kungalia uvaaji wangu? Je Yesu alikuja kutafuta walio watakatifu tu au wenye dhambi? Si vyema mimi nije kama nilivyo ili niweze kupata badiliko la kweli? Je si Roho Mtakatifu pia aamuaye ndani ya mioyo yetu namna ya kuwa Mtakatifu nadhani akiwa ndani yako atakuonyesha jinsi ya kuvaa au mwasemaje wapendwa?
Naomba tusaidiane kuchangia hii mada ili tujifunze na tuelimishane kusudi tupate kupona. Pia kama unazo picha za kuonyesha vazi la kwendea kanisani tafadhali naomba unipostie ili tubadilike. Barikiwa na Bwana

2 comments:

Anonymous said...

Ni kweli kabisa, Moyo wako ndio muhimu. Moyo wa ukunjufu na upendo. Hata ukivaa manguo yanameremeta kama dhahabu lakini kama moyo wako haumfurahishi Mungu, unajisumbua tu. Kama unataka kumfurahisha Mungu moyo wako uwe sawa. Be the Best of what he created you for. Dont Complimaze your Character for anyone or any thing, maana ukifanya hivyo sasa ndio sasa unamuuzia Shetani moyo wako, na Mungu hata sikumoja hataki tuwe hivyo.

Helen Matechi - Tabasamu said...

Nimeipenda comment yako tubadilike jamani Mungu anaangaliza zaidi MOYO. Asante mpendwa na Mungu azidi kukubariki