BWANA APEWE SIFA SANA,
NAZIDI KUMTUKUZA MUNGU KWA WEMA NA FADHILI ZAKE ANAZONITENDEA SIKU HADI SIKU KATIKA MAISHA YANGU. KATIKA POST ZANGU ZA NYUMA NILIAHIDI KUWA NITAENDELEA NA SOMO LA UPENDO WA KWELI NA HATA (WASWAHILI WANASEMA AHADI NI DENI) NA KWA VILE NILIAHIDI LAZIMA NITIMIZE AHADI ILI DHAMIRI YANGU IWE NJEMA NA SAFI.
TUENDELEE KUMSIFU MUNGU NA KUMTUKUZA KWA UKUU WAKE NA UAMINIFU WAKE NDANI YA MAISHA YETU KWANI BILA YEYE SISI HATUWEZI LOLOTE. TUNAHITAJI KUONGOZWA NA YEYE ILI TUWEZE KUSHINDA VIKWAZO NA MAJARIBU YALETWAYO NA YULE MSHITAKI WETU IBILISI.
TUWE MAJASIRI NA WENYE KUJIKINGA TUSIDHURIWE MIOYO YETU KWANI KWENYE MOYO NDIKO KWENYE CHIMBUKO LA UCHUNGU, MAWAZO MABAYA, CHUKI, FITINA, HOFU n.k CHANZO CHA KUZALIWA DHAMBI.
TUWE WASOMAJI WA NENO LA MUNGU KILA WAKATI TUNAPOWIWA KUFANYA HIVYO NA TUKABIDHI MAISHA YETU KWA ROHO MTAKATIFU YEYE AWE NDIYE KIONGOZI KATIKA KILA NYANJA YA MAISHA YETU.
HIVYO KAA MKAO WA KULA CHAKULA CHA UZIMA KWA HABARI YA UPENDO WA KWELI
MZIDI KUBARIKIWA NA BWANA
No comments:
Post a Comment