Tuesday, November 30, 2010

IMANI YAKO ITAKUPONYA, MWAMINI BWANA YESU LEO

Kila mwaka tarehe 1 / 12 ni siku ya kuadhimisha janga la UKIMWI kwa kuwa na ujumbe mbalimbali jinsi ya kutokomeza na kuelemisha watu jinsi ya kujikinga na kuzuia maambukizo mapya ya virusi vya UKIMWI na vile vile kuishi kwa matumaini kuhusiana na ugonjwa huu. Japo kuna baadhi ya maeneo elimu bado sijui niseme ni changa au haijawafikia walengwa vizuri, na  la kushangaza yakiwemo baadhi ya maeneo ya mijini yakiongoza kwa asilimia kubwa ya kuwa na maongezeko mapya ya mambukizi ya virusi vya UKIMWI. Swali la kujiuliza ni kuwa watu hawataki kuelewa au ni elimu imezoeleka kiasi kwamba watu wanaona hakuna jipya au maisha ndio yanawalazimisha kutokuzingatia yanayosemwa. Au je waelemishaji nao pia hawana elimu ya kutosha ya kuwaelimisha watu / watoaji elimu ni wachache kuliko walengwa / walioathirika? au wamekosa imani na Asasi / NGO zinazotoa huduma hii? Ukiangalia kwa mtazamo wa kawaida tu kuna Asasi/NGO mbalimbali zimeazishwa kwa ajili ya kusaidia na kuelimisha waathirika wa UKIMWI / na ambao bado hawajapata maambukizi pamoja na watoto yatima na wajane. Je wanatoa elimu sahihi na yakutosha? kama ndio kwa nini kuna ongezeko kubwa la watoto yatima na maabukizi mapya yanaibuka siku hadi siku? au waanzilishi  wa hizi Asasi / NGO wanatafuta maslahi yao wenyewe kwa kupitia mgongo wa walioathirika badala ya kutoa elimu ya sahihi na ya kutosha? Japo kwenye takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania imeshuka kwenye kiwango cha maambukizi ya UKIMWI ukilinganisha na nchi nyingine za Africa. Je hili nalo ni kweli yanaweza kuwa ongezeko la maambukizi mapya limepungua wakati bado tunashuhudia watoto yatima wakiongezeka kutokana na hili janga? (Tutafakari hili) Mimi sina jibu ila haya yote ni mtazamo wa kibinadamu tu. Hebu tungalie Biblia inatuambia nini kwa habari ya magonjwa? Je kuna ambalo linashindikana kwa Bwana? Kama yeye alitufinyanga kwa mikono yake si anajua kila sehemu ya viungo vyetu hivyo ni rahisi yeye kuturekebisha pale penye madhaifu na kupatia uzima. Hebu tuone Biblia inasema nini basi kwa habari ya uponyaji....

Ukisoma kwenye Biblia zetu utaona kwamba UKOMA ndio uliokuwa ugonjwa mbaya sana na ulikuwa unatishia watu enzi hizo za kale pia ulikuwa ni ugonjwa usioponyeka lakini watumishi wa Mungu walikuwa wanauwezo wa kuwaponya watu kutokana na ugonjwa huu kilichokuwa kinahitajika ni Imani na kutii tu, kwa Mfano Naaman aliyekuwa unaukoma lakini alipokea uponyaji. Soma 2Wafalme 5: 8-19 na pia Soma Mathayo 8:1-4 Yesu anaponya ukoma.

Japo kwa jambo la kushangaza na la kuhuzunisha ni kuwa huu ugonjwa hadi sasa upo toka enzi za akina Musa hadi leo lakini je ni kwamba dawa za kuuponya huu ugonjwa haijapatikana? imepatikana na ipo sema watu hawatilii maanani. Wako wapakwa mafuta wa Bwana ambao wamepewa karama ya kuponya wanaponyesha huu ugonjwa, kadhalika na UKIWMI pia wako watumishi wapakwa mafuta wa Bwana waliopewe karama ya uponyaji wako kukusaidia leo. Kama huu UKOMA ambao ulikuepo toka enzi hizo za akina Musa unawezekana kuponyeka kwanini watu wasiamini kuwa hata UKIMWI waweza kupona? Ukimwamini Mungu na kuyashika maagizo yake na kutii hakika utapona.

Mfano wa mwanamke aliyetoka damu kwa miaka kumi na miwili biblia inatuambia kuwa yule mwanamke aliazimia kuwa akiweza kushika tu upindo wa vazi aliyovaa Yesu hakika atapona na kweli alivyofanya hivyo kwa Imani yake kuu aliyokuwa nayo alipokea uponyaji muda ule ule Soma Mathayo 9 : 20 - 22; pia kwenye Marko 5: 25-34; sasa je wewe wawezaje kukata tamaa na kushindwa kumwammini Yesu kuwa kwa jina lake tu magonjwa yanatoweka hayatakuwa na nafasi tena ndani ya maisha yako utapona na utakuwa na nguvu na mwenye afya tele.  

Kama bado haujaambukizwa acha njia zako mbaya mtafute YESU shika maagizo yake na kuyatenda hakika atakuponya na hili janga wewe na familia yako na watu wa nyumbani mwako. Ingawa unaweza kuwa mwaminifu, waweza kuwa unatenda yaliyo mema kwa mtazamo wa kibinadamu lakini bado ukaupata huu ugonjwa kwa njia nyingine kwa mfano katika ajali kama ya gari, pikipiki au njia yoyote ile nk. (unajua kuwa maambukizi waweza pata kwa njia nyingi si kwa kuzini tu japo kuzini ndio njia kubwa ya maambukizi haya ya virusi vya UKIMWI). Lakini ukimtegemea Mungu na kukubali kuwa Yesu alikufa msalabani kwa ajili yako  na kuyatenda yote aliyokuamuru, hali hii haitakupata wewe na familia yako kwa ujumla na hata hutaacha wanao yatima bali utaishi hadi miaka mia na ishirini na utakufa ungali ukiwa na nguvu zako.

Yesu alifanya miujiza mingi ya uponyaji na hata sasa bado anafanya kwani anawatumia watumishi mbalimbali kufanya kazi aliyoianzisha kinachoturudisha nyuma ni kutokutilia maanani na imani kuwa haba kama nilivosema hapo juu. Watu tumekuwa na kiburi tukidhani kuwa wanayofanya watumishi wa Mungu ni ya uongo lakini mimi nakusihi leo hebu mwamini Yesu halafu utaona matunda yake na hakika hautajuta. Soma mistarii hii ikusaidie kwa habari ya imani katika uponyaji Mathayo 8 : 5-13; Mathayo 8 : 14-17;
Mathayo 9 : 27 - 31 n.k.

Mwamini yeye leo mtumainie Bwana peleka haja zako kwake naye atatenda, atakushindia na pia atakuponya, usikate tamaa usihangaike ikuze imani yako kwa kusikiliza na kusoma neno la Mungu mara kwa mara kwani Biblia inasema hivi "Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo"
Warumi 10 : 17 kisha mweleze shida yako peleka haja zako kwake naye atafanya. Pia Yesu anasema hivi, hata ukiwa na Imani kiasi cha punje ya haradali ukisema mlima huu ung'oke mahali hapa uende kule, nao utang'oka. Hivyo basi na uponyaji wako unahitaji imani yako kidogo tu kama punje ya haradali kwa Yesu kuwa anaweza kukuponya nawe utapokea uponyaji. Tumwamini yeye tuuone mkono wa Bwana ukitenda ndani ya maisha yetu.

Sasa basi watoto waliojaa matumaini wanakwambia nini kutokana na siku hii ya UKIMWI



Pia siku hii wanawasha mishumaa

Kunakuwepo pia na maigizo

Mishumaa kwa ajili ya ishara ya amani, upendo na mshikamano kuhusiana na siku hii haikosemani.

Mashairi yenye ujumbe wa siku hii ya kuhamasisha na kuelimisha hayakosekani kutoka kwa watoto wetu wapendwa.

Tuungane pamoja kuwaombea watoto yatima, wajane na pia kuwasaidia pale kwenye uhitaji kwani wanahitaji msaada wako wewe na mimi pia si kwa mali na fedha tu hata kwa maombi yako na kuonyesha upendo wako kwao utabarikiwa na Bwana ukisoma kwenye Mithali 19 :17 Neno la Mungu linasema hivi, "amhurumiaye masikini humkopesha Bwana, naye atamlipa kwa tendo lake jema". Hebu mkopeshe Mungu leo uone jinsi atakavyorudisha deni lake kwa haraka na tena ataweka na faida juu. Zaidi pia Bwana Mungu anasema kuwa yeye ni Baba wa Yatima na mume wa Wajane, unajua kuwa baba hawezi kumwacha mwanae afe kwa njaa lazima atahangaika huku na huko ili awatafutie riziki watoto wake ndivyo hivyo na Mungu wetu alivyo kwa watoto yatima, hebu fanya jambo leo ufanyike kuwa baraka kwa watoto hawa na Mungu atakubariki.

Monday, November 29, 2010

POKEA BARAKA ZA BWANA

BWANA AKUBARIKI NA KUKULINDA, BWANA AKUANGAZIE NURU ZA USO WAKE NA KUKUFADHILI BWANA AKUINULIE USO WAKE NA KUKUPA AMANI
BWANA AKUBARIKI UINGIAPO NA UTOKAPO TANGU SASA NA HATA MILELE

Thursday, November 25, 2010

SIKUKUU NJEMA WAPENDWA

NAWATAKIA WOOOTE SIKUKUU NJEMA YENYE BARAKA TELE NA AMANI YA KRISTO ITAWALE MIOYONI MWENU.

MSILE SANA MKAVIMBIWA JAMANI KWANI KUVIMBIWA NAYO NI DHAMBI.



HAPPY THANKS GIVING!!!!!!!!!
MBARIKIWE

USE YOUR DOUBLE PORTION OF SPEAKING POWER

1 Peter 2:9
But you are a chosen generation, a royal priesthood, a holy nation, His own special people...


God calls us “a royal priesthood”. This means that we are kings as well as priests under the king-priesthood of Jesus Christ. This has never happened before in the history of God’s people. In the Old Testament, kings and priests were two distinct groups of people. You were either a king or priest, but not both at the same time.

Today, because we are in Christ, we are king-priests — a royal priesthood. This means that we have a double portion of speaking power because as kings, “Where the word of a king is, there is power” (Ecclesiastes 8:4), and as priests, “by their word every controversy and every assault shall be settled”. (Deuteronomy 21:5)

So if you are a Christian businessman, you will have an edge over worldly businessmen. What you say about your business deals will come to pass. And if you are falsely accused, know that by your very word, every controversy and every assault will be settled!

And as a king-priest parent, when you bless your children, your words have the power to set in motion supernatural events which will bring them into God’s prosperous abundance and superabounding grace. And there will be such a courage and resilience about them that it will empower them to win the fights of life!

When the devil comes to you and says that you will die young because your father and grandfather died young, or that you will never be successful because you are not well-educated, you must remember that the devil is neither a king nor a priest. There is no power in his words. But there is power in yours because you are a king-priest in Christ!

So instead of agreeing with him, believe and declare, “I will not die young. With long life He will satisfy me and show me His salvation!” Say, “The Lord will make my way prosperous and give me good success!” Use your double portion of speaking power and see these blessings come to pass!

Wednesday, November 24, 2010

VAZI LA BINTI LA KWENDEA KANISANI


Linen ni vazi zuri tu la kwendea kanisani waweza kuvaa suruali kama hivi au skirt na ukapendeza tu.



Skirt na blouse ya Linen


nimependa mshono wa hii suit na ni nzuri kwa binti wa kileo mpasuo si mkuuubwa na wale wasiopenda kuvaa mburuzo basi hii angalau itakutoa chicha.

hii nayo boma kwa binti wa kileo kwani kitambaa chepesi kimeongezekea chini ili kutoonyesha umini mkubwa kwa sababu bila hicho kitambaa chepesi inaonekana ni kimini cha ukweli sema kitambaa hicho chepesi kinafanya nguo isionekane ni mini skirt. Angalia rangi nyingine chini na jinsi inavyovutia.





Wapenda suruali haya kikoti waweza vua kama joto limechachamaa
Hata binti anaweza kutupia kofia kama hivi.




Kwa baadhi ya makanisa wasiopenda waumini wanawake wavae suruali hii ya juu na chini ni bomba sana sana






MWALIKO! MWALIKO! MWALIKO!

DON'T MISS

Worship with us Sunday 28/11/2010 at 3PM with special gospel music by the Brooklyn Tabernacle Singers and a truth that transforms – Talking to Yourself!!!

See you there,
Pastor Jim Cymbala

Tuesday, November 23, 2010

WAPENDA KOFIA ( ZA KANISANI) MAMA RWAKATARE STYLE

Haya wapendwa kwa wale wanaopenda kuvaa kofia mimi naita Mama Rwakatare style kwa sababu huyu Mtumishi wa Bwana anapenda sana kuvaa akiwa kanisani na baadhi ya waumini wake chagua yako uipendayo sasa.






 



barikiwa

VAZI LA KWENDEA KANISANI

Kwa wale wapenda makofia hizi picha zitawasaidia lakini si lazima kuvaa kofia kama haupendi vaa suit yako namna hii jimwaye kanisani.

Kofia si lazima kama inakusumbua achana nayo suit yatosha


Nadhani mnaona style ya nyuma ya hii suit si ya kwenye harusi au send off hili ni vazi la kwendea kanisani.

Hii suit kwa bongo Dar es salaam inafaa sana joto likizidi unatoa koti unaonekana namna hiyo kwenye picha ndogo. Kama hauoni tabu basi pendeza na koti lako msifu Bwana bila kuchoka.
Nimeipenda hii lakini mimi si mtu wa kofia hivyo naweza vaa bila kofia na nikatoka safiii kabisa jaribu uone.

Hizi si sare za harusi jamani ni vazi la kwendea kanisani la heshima kabisaa na sio nzito kwa TZ yawezekana kuvalika.
Watakao lalamika joto Dar jamani sasa sidhani kama hapo una la kusema


Ukipenda suruali haya, skirt twende, joto kali vua koti uonekane namna hiyo hapo.
nimeipenda
Wapenda suruali kama mimi hatukubaki nyuma ndio kama hivi tena na kanisani tunaingia kumsifu na kumshangilia Bwana tukiimwaga mioyo yetu.
Binti naye aweza kuvaa hivii.


picha zaidi zaja wakaka na wababa sijawasahau nao natoa zao karibuni.
mabinti kaeni sawa zenu zaja.
african style nayo yaja
enjoy

Monday, November 22, 2010

TUKIWA NA YESU TUNAYAWEZA YOTE

Bwana wetu Yesu Kristo anatuambia hivii,

Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa baba ila kwa njia ya mimi.

Pia Yesu anaendelea kusema hivii,

Amin, amin nawaambieni, Yeye aniaminie mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya, naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa baba. Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili baba atukuzwe ndani ya mwana.

Tutafakari mistari hii je Bwana Yesu alikuwa na maana gani alivyokuwa anasema maneno haya? Je unaamini kuwa bila Yesu hautaweza kuuona ufalme wa Mungu? Basi sasa kama bado haujampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi ndani ya maisha yako tafakari kwa makini kuhusu mstari huu. Mpokee leo naye atabadili hali ya maisha unayoishi sasa na utapata burudiko la moyo na furaha ya kweli kwani yeye ndiye njia pekee ya wewe kuweza kumwona Bwana.

Je unajua kuwa ukimwamini Yesu na kazi alizozifanya angali hapa duniani na wewe waweza kufanya kama yeye na kubwa kuliko alizozifanya Yesu?  Cha msingi ni wewe tu kumwamini na kuamini kuwa Yesu ni Bwana, na ya kuwa miujiza aliyoitenda na wewe waweza kuifanya. Kwa maana aliyeko ndani yako baada ya kumpokee na kumwamini ana nguvu na ni mkubwa kuliko hayo mapepo, magonjwa nk. Yesu aliweza kumfufua Lazaro aliyekaa kaburini siku nne basi hakika na wewe waweza kufufua. Yesu aliponya vipofu, viziwi na wewe utaweza kuwaponya watu pia anasema na mengine makubwa zaidi yake utaweza kufanya, unachotakiwa ni kumwamini tuuuu.
Anaongeza kusema pia ukiomba lolote kwa jina lake atafanya? haijalishi ni kitu gani unachoomba mradi uombe kwa jina lake Yesu hakika atakutendea, iwe ni amani, furaha, ndoa, watoto, kazi, fedha, na mengineyo mengi atakupa bila hiyana. Tumwamini yeye na tuyashike maagizo yake basi naye atatutendea na pia kwa nguvu ya uweza wake tutafanya mambo makubwa hata yale ambayo kwa akili zetu za kibinadamu yasingewezekana kutendeka na kwa sababu ameahidi na hakika atatenda.

Roho Mtakatifu atuwezesha na atufafanulie kwa hekima yake maneno haya ya Bwana wetu Yesu Kristo na pia yawe ni chachu na nguzo ya kutusogeza karibu na baba na kutuwezesha kuamini.
Barikiwa mpendwa.

BLESSED TO BE A BLESSING

Dear Friend,
As our loving heavenly Father, it is God's utmost wish for us to prosper and be blessed in all areas of our lives. (3 John 1:2, KJV) Today, I want you to know that God wants to abundantly supply every need in your life and bless you out of the largeness of His heart. He wants you to experience His abundance far above anything you could ask or imagine!
Jesus came to give us a new life — a life worth living — one in which we are blessed as His children for a divine purpose. I want to encourage you to start looking at His blessings on your life in a whole new way: seeing that you are blessed to be a blessing!
Deuteronomy 8:18 says, "And you shall remember the LORD your God, for it is He who gives you power to get wealth, that He may establish His covenant. . ." It is God who gives us the power to prosper, and just like Abraham, we are blessed to be a blessing. (Genesis 12:2)
When we are abundantly blessed by God, we will have enough to give to those in need. Also, people will see His awesome goodness in our lives and turn to Him.
Are you ready to dive in and experience it for yourself?
Now, you may be thinking, "I would love to give to others and be a blessing, but I just don't have anything to offer. How can I overcome lack so that I can bless others?" I understand that in difficult times, especially times of economic stress, it's natural for many people to look at what they have and say, "I'm not blessed! I have nothing to offer!"
But listen, beloved, God's Word says that you can enjoy His abundance in your life and be a powerful blessing to others. Your situation may seem impossible in the natural, but God can supernaturally work in your life and your finances. You are immensely favored and greatly loved by your heavenly Father, who has provided everything you could possibly need through the complete work of Jesus.
Beloved, I want to encourage you to make a decision today to receive God's supply and abundance in your life. If you want true prosperity that covers every area of your life, let me show you God's way according to His Word. Listen to the word of grace, read the word of grace, share the word of grace, but above all, walk in the truth of the word of grace and watch your soul prosper. Then, get ready because God will do incredible things through you to bless the lives of others!
Blessed to be a blessing,

ASK IN JESUS NAME AND RECEIVE



John 16:23
23“… Most assuredly, I say to you, whatever you ask the Father in My name He will give you.

Do you always end your prayers with “in Jesus’ name”? Maybe your Sunday school teacher taught you to do this, or maybe you have heard church leaders and other believers utter it at the end of their prayers.

I used to say “in Jesus’ name” very quickly as if those were magic words that would get my prayers answered. Then, one day, I heard the Lord asking me why I was doing that.

The Lord wanted me to realize that whenever I pray and say “in Jesus’ name”, I am putting my entire faith for my prayer to be answered not in who I am or what I have done, but in the person and name of our Lord and Savior Jesus Christ, and what He has done at the cross!

Whenever we ask God for anything in Jesus’ name, Jesus says to us, “Most assuredly, I say to you, whatever you ask the Father in My name, He will give you.” This means that in your prayer for healing, when you say “in Jesus’ name”, healing comes over your sick body because it is by His stripes that you are healed. (1 Peter 2:24) In your prayer for protection, when you say “in Jesus’ name”, you are kept safe because the blood of Jesus protects and delivers you from evil. (Exodus 12:13)

Beloved, the good name of your family cannot save you. Your pastor’s name cannot save you. Even the name of the latest medical breakthrough cannot save you. Only one name under heaven can save you — Jesus! And the good news is that His name in Hebrew, Yeshua, means salvation — healing, preservation, wholeness, wellness, provision, prosperity, safety and deliverance for you and your family!

So these days, whenever I pray, I slow down at the end of my prayer and say, “Father, I ask all this not based on what I have or have not done, but based on Jesus and His finished work at the cross. I ask all this in Jesus’ name. Amen!”

Saturday, November 20, 2010

REAL THANKSGIVING, DO SOMETHING, BRING SOMEONE

Food for your soul!
Food for your stomach!

Don’t miss the 3:00 PM service this Sunday and the handing out of 500 turkeys with all the trimming. This is for folks needing extra help. This might be you or someone you can bring to make next Thursday a day of real thanksgiving to God.

Hope to see you then!

Sincerely,
Pastor Jim Cymbala
Brooklyn Tabernacle Church

Thursday, November 18, 2010

NENO LA BWANA



neno la uzima
Nahumu 1:2-9
Bwana ni Mungu mwenye Wivu, naye hujilipiza kisasi. Bwana hujilipiza kisasi naye ni mwingi wa hasira; Bwana hujilipiza kisasi juu ya adui zake, huwawekea adui zake akiba ya Hasira.
Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi wala hatamwesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe, Bwana ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake. Yeye huikemea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote.
Mstari 5 unasema hivi, Milima hutetemeka mbele zake, navyo vilima huyeyuka, nayo dunia huinuka mbele ya uso wake, naam, dunia na wote wakaao ndani yake. Ni nani awezeye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake?  Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye. Bwana ni mwema ni ngome siku ya taabu, naye huwajua hao wamkimbiliao. Lakini kwa gharika ifurikayo atapakomesha kabisa mahali pake, na kuwafuatilia adui zake hata gizani.
Mnawaza nini juu ya Bwana? Yeye atakomesha kabisa mateso hayatainuka mara ya pili.

The God of More Than Enough




Luke 5:9
For he and all who were with him were astonished at the catch of fish which they had taken;

As a young Christian, I grew up hearing preachers say that God only supplies our needs, not our wants. Yet, in the Bible, God clearly shows us that He wants to meet not just our needs, but also our wants.

For example, the famous “shepherd psalm” begins with “The Lord is my shepherd; I shall not want”. (Psalm 23:1) Another psalm says, “Oh, fear the Lord, you His saints! There is no want to those who fear Him. The young lions lack and suffer hunger; but those who seek the Lord shall not lack any good thing.” (Psalm 34:9–10)

One of the names of our God is Jehovah Jireh, which means “the all-providing One”. He provides more than enough. The God of more-than-enough came in the flesh and walked among His people. And as He walked by the Sea of Galilee, He did not give His disciples small blessings. That is why He said to Peter, “Launch out into the deep and let down your nets [plural] for a catch,” (Luke 5:4) and not “let down your net [singular]”. And what a catch it turned out to be — a boat-sinking, net-breaking catch! It was such a big and unexpected blessing that Peter and all who were with him were “astonished at the catch of fish which they had taken”.

Beloved, see God’s heart for you today. He wants to prosper you greatly. Don’t settle for anything less, thinking that He only supplies your needs and not your wants. If you need a job, know that He wants you to pray not just for a job, but for a position. When you have a position, you have influence and you are able to impact lives. Maybe what you need is a pay increment. Then, pray not just for that, but also to be in a position to give increments!

You may start out poor when you follow God. But you cannot remain poor when you follow the God of more-than-enough. In fact, like Peter, you too will be astonished that God supplies more than what you need and beyond what you have asked!

Wednesday, November 17, 2010

SIKU YA WAMAMA LIVING WATER CENTER KAWE NO. 2

Madhabahuni siku hiyo palionekana hivi.

Mtumishi wa Mungu Mama Lilian Ndegi akiwa na msaidizi wake Anna wakifanya maombi kabla ya kupanda jukwaani kutoa Neno.

Ilikuwa ni siku njema sana watu walizama kabisa kwenye maombi

Maombezi yalifanyika siku hiyo watu wengi walifunguliwa kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Wamama wakiwa wamezama kwenye maombi siku hiyo.
Mpakwa mafuta wa Bwana akiwa kwenye maombi.
Mlangoni pa kuingilia palionekana hivi siku hiyo.

Tuesday, November 16, 2010

MAOMBI YANGU KWAKO SIKU HII YA LEO

BABA KATIKA JINA LA YESU KRISTO NALITUKUZA JINA LAKO NA NINAKUSHUKURU KWA WEMA NA FADHILI ZAKO UNAZONITENDEA NDANI YA MAISHA YANGU SIKU HADI SIKU. ASANTE KWA UPENDO WAKO, ASANTE KWA REHEMA ZAKO, ASANTE KWA KUNIPA TUMAINI SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU, ASANTE KWA ULINZI WAKO NA BARAKA ZAKO UNAZONIPA SIKU HADI SIKU. LIHIMIDIWE JINA LAKO.

NAKUSHUKURU MUNGU WANGU KWA AJILI YA BABA HUYU, MAMA HUYU, KIJANA HUYU, BINTI HUYU NA WALE WOTE WATAKAOFUNGUA MAOMBI HAYA KWA MAANA MUNGU UMEZIDI KUWAPENDA KWA JINSI YA TOFAUTI. ENDELEA BWANA KUONYESHA UWEZA WAKO NA PENZI LAKO NDANI YA MAISHA YAO. WASAMEHE MAKOSA YAO BWANA NA UWAREHEMU NA KUWAHURUMIA, DAMU YA YESU KRISTO ULIYOMWAGIKA PALE MSALABANI KWA AJILI YA ONDOLEO LA DHAMBI IWATAKASE DHAMBI ZAO NA KUWASAFISHA NA KUWAWEKA HURU. USIWAACHE MFALME WANGU WA AMANI BALI WAZINGIRE KWA WIGO WAKO NA UTUKUFU WAKO UWAFUNIKE. ROHO MTAKATIFU  WAFUNIKE KWA WIGO WA MOTO WAKO UTAWALE NYUMBA ZAO, FAMILIA ZAO, WATOTO WAO, NDOA ZAO NA HATA KAZI ZA MIKONO YAO. USIWANYIME BARAKA ZAKO KILA IITWAPO LEO BWANA WANGU TEMBEA NAO KATIKA MAISHA YAO YA KILA SIKU KILA WAINGIAPO NA WATOKAPO WAKAPATE KIBALI MACHONI PAKO NA KWA WANADAMU PIA EE MWOKOZI WANGU. WAPE ILE HAJA YA MIOYO YAO BWANA KWANI WANAKUTUMAINIA WEWE TU KWA MAANA WEWE NDIWE NGAO YAO, NGOME YAO NA MSAADA KATIKA MAISHA YAO NA BILA WEWE BWANA HAWEZI KUFANYA JAMBO LOLOTE KWANI WEWE NDIO TEGEMEO LAO KUU.
WAKINGE NA KILA NGUVU ZA GIZA NA MAJARIBU YALETWAYO NA YULE MWOVU. WAOKOE KATIKA VISHAWISHI, KILA ROHO ZITAKAZOINUKA JUU YAO SIKU HII YA LEO NA ZISHINDWE KATIKA JINA LA YESU, NAKATAA ROHO YA HOFU NDANI YA MAISHA YAO KATIKA JINA LA YESU, NAKATAA MAGONJWA, NAKATAA ROHO YA UCHUNGU, HASIRA, CHUKI , KUKATA TAMAA KATIKA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARET ALIYE HAI. KIFUNGO KIWAYO CHOTE WALICHOFUNGWA NDANI YA MAISHA YAO NINAKIFUNGUA SASA KATIKA JINA LA YESU, NINAWAKOMBOA KATIKA ULIMWENGU WA KIROHO NA KUWARUDISHA POPOTE WALIPOFUNGWA KATIKA JINA LA YESU. SHETANI HANA MAMLAKA NAO, NGUVU ZA GIZA HAZINA MAMLAKA NAO, WACHAWI HAWANA MAMLAKA NAO, MAJINI HAYANA MAMLAKA NAO KUANZIA SASA, KUANZIA LEO KATIKA JINA LA YESU KRISTO WA NAZARETI.
NAWAPA AMANI YA KRISTO, UPENDO, FURAHA, TUMAINI, AFYA NJEMA NA KILA HALI YA UWEZA WA MUNGU KATIKA MAISHA YAO YA KILA SIKU KUANZIA SASA. UWEPO WAKO BWANA USIWAPUNGUKIE BALI UZIDI KUWAFUNIKA NA KUWAONGOZA KILA WAKANYAGAPO WAPAMILIKI MUNGU WANGU. ROHO YA UNYENYEKEVU IUMBIKE NDANI YA MAISHA YAO, TUNDA LA ROHO MTAKATIFU LIUMBIKE NDANI YAO BWANA. ROHO MTAKATIFU TAWALA MAISHA YAO, ONEKANIKA BWANA NDANI YA MAISHA YAO. USIWAACHE JEHOVA BALI UZIDI KUWATUMIA KAMA CHOMBO CHAKO KITEULE. FANYA JAMBO JIPYA NDANI YA MAISHA YAO SASA BWANA, ANZA NAO KWA UPYA LEO TENA BWANA.
NAKUSHUKURU MUNGU WANGU, NASEMA ASANTE ROHO MTAKATIFU KWA MAANA MAOMBI HAYA YAMEKUBALIKA MBELE ZAKO NA YAMEKUWA MANUKATO KATIKA KITI CHAKO CHA ENZI EE MUNGU WANGU.
KATIKA JINA LA MWANAO MPENDWA YESU KRISTO NINAOMBA NA KUSHUKURU.

AMENI!  AMENI!  AMENI!

NENO LA UZIMA (KUBALI KUJARIBIWA)

Zekaria 13:9

Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha katika moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; WATALIITA JINA LANGU, NAMI NITAWASIKIA; mimi nitasema, WATU hawa ndio wangu; nao watasema BWANA NDIYE MUNGU WETU.

Haya si maneno yangu bali ni maneno ya Bwana Mungu akituambia sisi wana wake wa leo. Mpendwa kubali kupitishwa katika moto kwa maana lipo kusudi la Mungu kufanya hivyo. Ukiona vita vimekuwa vikali ndani ya maisha yako basi usimlau shetani wala usimnung'unikie Mungu kwa kudhania ya kuwa amekuacha ila ujue kuwa Mungu anakupitisha katika moto ili usafishwe kama fedha isafishwavyo utolewa kila aina ya uchafu, visiki hata vile vilivyoweka mizizi yake kwenda chini sana, (kwa maana ya udhaifu wako fulani ambao umekuwa ni vigumu kuuacha ambapo unakupelekea kutenda dhambi) hivi vyote anataka aving'oe ndani ya maisha yako, ili uwe safi. Kisha anakupitisha katika majaribu kwa maana ya kuwa anamwachia shetani akujaribu ili aone kweli umetakata unafaa kuwa chombo chake kiteule.
Majaribu ni mtaji mpendwa wa kukupeleka hatua nyingine katika ufalme wa kiroho, kusudi la Mungu kukupitisha katika moto na pia kuacha ujaribiwe ni kukusafisha na kukufanya uwe safi kama yeye alivyo kwani Mungu wetu hakai mahali palipo pachafu kwa sababu yeye ni Mtakatifu. Na ili wewe uwe Mtakatifu kama yeye alivyo ni kwa kusafishwa ndio maana anasema katika maandiko yake kuwa iweni watakatifu kama mimi nilivyo Mtakatifu. Sasa je wawezaje kuwa Mtakatifu kama bado unao uchafu ndani yako? Na hakuna awezaye kuuona uchafu uliokuwa nao isipokuwa yeye pekee ndiye aonaye hata ndani ya mioyo yetu na yeye ndiye anayeweza kukutoa yale ambayo kwa macho ya  nyama ya kibinadamu hatuwezi kuyaona ambayo yamekuwa changamoto kubwa katika maisha yako na kufanya usiweze kutumiwa na Bwana au yamekuwa kizuizi kikubwa cha wewe kufanikiwa. Kutokuwa msafi pia ndipo kunakopelekea hata maombi yako yanakuwa hayapokelewi kwa maana ukimwita Mungu anakuwa hakusikii maana anasema akishakusafisha na kukujaribu na kukuona safi ndipo utakapomwita jila lake naye atasikia.
Ukisoma katika 1Wakoritho 10:12 utaona ya kuwa Mungu ni mwaminifu hata akiaacha ujaribiwe anafanya pia na mlango wa kutokea katika hilo jaribu. Hivyo basi Mungu haruhusu majaribu yakupate kama hana kusudi jema nawe anachotaka ni wewe kumtumainia na kuamini kuwa anaweza kufanya yasiyowezekana yakawezekana cha msingi ni kuzidi kulitukuza jina lake, kumsifu na kushika maagizo yake na kutenda hasa hasa pale unapokuwa umepitishwa kwenye moto.
Faida ya kukubali kupitishwa kwenye moto na kujaribiwa ni kuwa utakapoita jina lakeanasikia tena kwa haraka sana anasema kuwa hakika utasema Bwana ndiye Mungu wako kwani atakutendea mpaka yale ambayo uliyokuwa hukuyaomba. Atafungua madirisha ya mbinguni na baraka zake zikushukie atakubariki uingiapo na utokapo, atabariki watoto wako, ndoa yako na hata familia yako kwa ujumla. Hata sahau kazi ya mikono yako kwani nayo pia itabarikiwa, atabariki mifugo yako na mazao yako shambani. Ukisoma katika Isaya 65:20-25 utaona ahadi nyingine za baraka kutoka kwa Mungu na ni jinsi gani utakavyoweza kufanikiwa katika maisha yako ukikubali kusafishwa.
Mungu wetu analokusudi jema nawe mpendwa kwani anakuwazia yaliyo mema siku zote. Hivyo basi kubali kupitishwa katika moto usafishwe uwe safi nawe uuone mkono wa Bwana ndani ya maisha yako.

NENO LA MUNGU LIGONGELEZEWE KATIKA VIBAO VYA MIOYO YETU.

Monday, November 15, 2010

GOD IS RAINING BLESSINGS ON YOU

Deuteronomy 28:12
The Lord will open to you His good treasure, the heavens, to give the rain to your land in its season, and to bless all the work of your hand. You shall lend to many nations, but you shall not borrow.


In the Bible, rain usually speaks of blessings. Even today, Israelis thank God when it rains because they know that when He gives them rain, their blessings will be plentiful. Their cattle will feed in large green pastures and eat cured, winnowed fodder. And when they see rivers and streams of water flowing from their mountains and hills (Isaiah 30:23–25), they know that times of refreshing have come.

Likewise, you can expect God to rain His blessings on you and bless the work of your hands. Then, you will come to a place where you will “lend to many nations, but you shall not borrow”. In fact, Jesus wants you to know that this is a blessing which He died to give you because when He died, He did not even have a tomb of His own. He was laid in a borrowed tomb, so that you can have the power to lend.

Indeed, our church bears testimony to this blessing. When I first joined the church full-time, it was very small — about 100-odd members. The Lord has, however, rained His blessings on us and blessed the work of our hands. Today, we have a congregation of more than 19,000 members and we are still growing. In fact, our church is lending its support to many ministries, both locally and overseas. We continue to see God pouring His blessings of prosperity and increase on us, and we thank Him for all the good things that are happening to us.

My friend, there is nothing you can do about the rain but to let it fall. So just expect God to rain His blessings on you! Let them fall! And you will be blessed with more than enough, so that with your needs and your family’s needs more than met, you can be a blessing to others too!

Saturday, November 13, 2010

You Will Have Whatever You Say

Mark 11:23
For assuredly, I say to you, whoever says to this mountain, ‘Be removed and be cast into the sea,’ and does not doubt in his heart, but believes that those things he says will be done, he will have whatever he says.

God says that we will have whatever we say. So whatever we want to have, we can say it and have it. Unfortunately, we often say what we don’t want to have.

For example, we say, “I don’t know why I go through my money so fast every month. Even when my boss gives me an increment, there never seems to be enough money.” And true enough, we see a lack of money at the end of every month.

You see, you will have whatever you say, good or bad. So why not change what you have been saying to, “From now on, I will have more than enough because Jesus became poor at the cross, so that I might become rich — 2 Corinthians 8:9. So poverty, be gone in Jesus’ name!”

Whatever mountain of difficulty you have, be it a mountain of debt or serious health condition, Jesus says, “For assuredly, I say to you, whoever says to this mountain, ‘Be removed and be cast into the sea,’ and does not doubt in his heart, but believes that those things he says will be done, he will have whatever he says.”

Jesus highlights the importance of saying by mentioning the word “say” thrice, but the word “believe” only once. Our problem today is that there is more preaching on believing than saying. So the reason people find it hard to walk in faith is that they are not saying enough of the Word.

But if we would focus more on saying God’s Word, faith will come. That is how God quickened Abraham’s faith. He changed Abraham’s saying when He changed his name from Abram to Abraham, which means “father of many nations”. (Genesis 17:5) From then on, whenever Abraham introduced himself, he would say, “Hi, my name is Father Of Many Nations."

Beloved, declare your abundance, saying, “The Lord is my shepherd, I shall not want.” (Psalm 23:1) Speak forth your healing, saying, “By Jesus’ stripes I am healed!” (Isaiah 53:5) And you will have whatever you say!

Friday, November 12, 2010

WATOTO WENYE AMANI NA MATUMAINI WANAKUAMBIA HIVII

Hapa nadhani ujumbe unajitosheleza. Lakini ukiwa na Yesu hili kwako halipo kabisa na wala halitakugusa. Kama tayari ugonjwa huu umeshakutembelea usiwe na wasiwasi  kwani yeye anao uwezo wa kuponya kama aliweza kushinda kifo na mauti magonjwa ni jambo dogo sana kwake kinachohitajika hapa ni Imani yako tu umwamini kuwa anaweza naye atatenda. Ukisoma katika Biblia kazi kubwa aliyoifanya Yesu alipokuwa hapa duniani ni uponyaji kwa hiyo mpokee leo kuwa Bwana na Mwokozi ndani ya maisha yako naye atakushindia vita hivi vya magonjwa.