Biblia yangu inaniambia hivii:
"KWA HIYO AJIDHANIAYE AMESIMAMA NA AANGALIE ASIANGUKE"
Nadhani hii ni mithali ya kiswahili pia sasa jamani huu ni udhihirisho tosha kuwa Biblia ina kila kitu haikuaacha hata chembe ni sisi tu wavivu wa kuisoma. Haya si maneno yangu ila ni maneno anayosema Mtume Paulo akiwaambia kanisa la Korintho. Kwa hiyo ndugu tuwe makini tusijidhanie kuwa tuko imara tumesimama tuangalie sana sana tusije tukaanguka kwani mshtaki wetu yuko mlangoni anasubiria tu tujikwae ajichomeke ndani. Hivyo basi tukaze sana kusoma neno la Mungu na kutii kwani ndio njia pekee ya kumshinda adui yetu. Tufishe ile roho ya kiburi inayojinyanyua ndani ya maisha yetu kwani ndio inayotufanya wakati mwingine kujiona tuko sawa na kudharau mambo kumbe loo tunaanza kuanguka. Navunja na kuikataa roho ya kiburi ktk jina la Yesu.
Neno, Neno, Neno la Mungu ndio nguzo yetu. Uwe na wakati mzuri.
No comments:
Post a Comment