Friday, September 24, 2010

KUHUSU VAZI LA KWENDEA KANISANI

KUMBE LIPO JAMBO KATIKA VAZI LA KANISANI
Nimekutana na mtumishi mmoja wa Bwana dada mtanashati ambaye aliwahi kushiriki Miss Tanzania miaka ya nyuma na kwa sasa ameokoka na Bwana anamtumia tukawa tunazungumza kuhusiana na VAZI LA KWENDEA KANISANI (hii ni kutokana na post zangu za nyuma) akasema yeye ameipata hii kutoka kwa mtumishi wa Mungu mmoja ambaye alimwambia kuwa si kwamba makanisa wanakataza uvaaji wa mabinti au wamama kuvaa vimini kanisani (na makanisa mengine hata suruali kwa wanawake wanakataza) tatizo linakuwa ni kwa hao Baba zetu na kaka zetu ambao tamaa ya mwili bado kufishwa kwani wakiona wadada wamevaa namna hiyo na akiwa ibadani basi mambo ya ibada yanaishia hapo hapo inakuwa tena umempeleka sehemu nyingine kabisa na hata neno kusikiliza inakuwa ngumu. Kwa hiyo inakuwa uwepo wake ibadani siku hiyo ni ya bure hapokei kitu kabisa.
Na huyo mtumishi wa Bwana pia akatoa mfano wa akina mama/dada wengine wanaokaa viti vya mbele kabisa wengine wanajisahau sana unakuta anakaa vibaya hivyo pia inampa wakati mgumu mtumishi wa Bwana wakati yuko mbele anatoa Neno la Mungu kwani kukwambia kaa vizuri anashindwa na yeye ni mwanaume rijali basi inabidi aweke macho pembeni ili kuweza kutokuvutiwa na kuchungulia kwani anasema wao pia ni binadamu na shetani anatafuta kila njia ya kuweza kuwaangusha. "Kumwingiza mtumishi wa Mungu majaribuni ni laana kubwa tena kubwa sana."
Hivyo basi cha msingi wanachoona kinafaa kufanya ni kuwaambia wamama na wadada wavae nguo ndefu na magauni mapana au wasivae suruali kama sheria ya kanisa ili kuepusha kuwapoteza au kuwakwaza au hata kuwaingiza majaribuni baadhi ya wababa na wakaka na hata baadhi ya watumishi wawapo kwenye uwepo wa Mungu (kanisani)

Nadhani nitakuwa nimeleweka kama sivyo, namsihi Roho Mtakatifu aliye mwalimu mkuu akueleweshe.
Vazi la kanisani linatakiwa kuwa hivi wapendwa. (Haswa kwa wale wakaaji wa mbele kabisa)

Helen & Mama miezi kadhaa iliyopita Brooklyn Tabernacle tukitoka kanisani.

Mtoto wa Kifai (Matechi's la familia)
yeye hutoka hivi kwenda kanisani.

No comments: