Friday, September 24, 2010

TUELIMISHANE

Kusema kweli mimi wakati mwingine nashindwa kuelewa hapa naomba msaada wenu jamani kujua tofauti ya hawa wenye kazi hii na wale tunaokwenda kwa ajili ya mambo mengine mengine (wale tunaopenda kuvunja kazi zao na mipango yao katika jina la Yesu) yaani waganga wa kienyeji. Je hawa si wale wale jamani au ni sawa na hospitali kwa daktari unakwenda basi na hawa ndio jambo moja. Nina maswali mengi mno naamini na nyie ndugu mnayo tusaidiane kuelimishana pia tusisahau kuiombea nchi yetu tuwapo kwenye maombi jamani.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.Blandina Nyoni akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa tiba za asili Dkt. Ahmad Darusi kuhusu namna ya kutumia Dawa aliyoitengeneza yenye uwezo wa kuwasaidia wagonjwa wa UKIMWI wakati wa sherehe za uzinduzi wa Usajili wa waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.
Katibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Bi. Blandina Nyoni akituma fomu za usajili wa waganga wa tiba za asili na tiba mbadala kwa njia ya mtandao katika mikoa yote ya Tanzania leo jijini Dar es salaam fomu ambazo zitapatikana kwenye ofisi za Halimashauri kote nchini kwa ajili ya usajili. Wanaoshudia Kulia ni Mganga mkuu wa serikali Dkt. Deo Mutasiwa na Msajili wa Tiba za Asili na Tiba Mbadala Dkt. Paul Muhani (Kushoto).

 Baadhi ya wataalam wa Tiba za asili wakiwa na dawa mbalimbali za asili walizozitengeneza tayari kwa maonyesho leo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Usajili wa waganga wa Tiba za asili na Tiba mbadala katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.

(Hii ni kwa hisani ya blog ya Isaa Michuzi)

No comments: