Sunday, January 30, 2011

USHUHUDA

Namshukuru Mungu sana kwa kunipa mafunuo ya kuanzisha hii Blog kwani toka nianzishe nimeona jinsi Mungu anavyotenda ndani ya maisha yangu na pia kunipa kibali mbele za watu kwani nimefanikiwa kukutana na watu kupitia blog hii ambao hapo kabla nilikuwa siwafahamu na kujua kuwa bado kuna watu wana kiu ya kumjua Mungu sana na wengi wako kwenye vifungo.
Nimepata email kadha wa kadha za watu kuomba maombi nami nimefanya hivyo kwa uweza wa Roho mtakatifu na usaidizi wake. Lakini hivi karibuni nimepata maombi ya kipekee kutoka katika nchi moja huko Africa. Huyu ni mtumishi wa Mungu ambaye analo kanisa lake lenye watu thelathini, yeye badala ya kuomba maombi aliomba asaidiwe Biblia kwa ajili yake yenye Maandishi makubwa ili aweze kuwafundisha vizuri waumini wake, kwani anasema kutokana na umri alio nao kwa maana ni mtu mzima macho yake hayaoni vizuri. Nami kwa msaada wa Mungu naamini ni kwa kibali chake kumwelekeza huyu mtumishi kwangu hivyo imenipasa kufanya  hivyo na zaidi. Namshukuru Mungu kwa hili kwani siku zote nilikuwa namwomba Mungu anitumie mimi kama chombo chake sasa naamini kuwa nimefanyika chombo kwa Bwana kwa watu kupata neno lake ambalo ni muhimu katika maisha yetu sisi sote na naamini litawafungua wengi katika vifungo.

Namshukuru Mungu kwa ajili ya hili kwani naamini hizi Biblia zitawaokoa wengi ambao watalisikia neno akiwahubiria huyu mtumishi nami nitakuwa nimeishi andiko katika Yohana 15:1-2

Bwana Yesu Apewe Sifa sana sana sana. Tuzidi kupendana na Amani ya Kristo itawale mioyoni mwetu. Amen amen.

RAHA YA UWOKOVU

Ukiwa ndani ya Yesu kuna raha  mpendwa asikwambie mtu, yote yanawezekana kwa Bwana hata yale ambayo kwa akili za kibinadamu ni magumu kuwezekana ili maradi tu umwamini. "Biblia inasema hivi, yote yawezekana kwake yeye aminie". Nami na mwamini Mungu nimeuona mkono wake ndani ya maisha yangu, amani niliyonayo leo na furaha vyote nimevipata kutoka kwake yeye. Ananishindia siku hadi siku kila kitu kwangu ni shwari kwani najua ninaye mwenye uweza wote aliye mbele yangu, anayenipenda aliyenishika mkono anayeijua kesho yangu tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu Bwana Mungu Yesu Kristo pamoja na Roho wake Mtakatifu naamini hata niacha kamwe, ananikumbatia na kunitia nguvu. Furaha, amani, utulivu, nguvu, na uweza ninavyo leo kwa sababu siku moja niliamua kuwa nataka kuwa na mshauri, mpenzi, mwalimu, kiongozi, baba Yesu Kristo ndani ya maisha yangu naye bila hiyana akanikubali akanivuta karibu nae akaniambia mwanangu karibu nyumbani hapa umefika yale uliyopitia na kuyaona hapo kabla hayatakupata tena kamwe na wala hautayaona. Kama alivyowaambia wana wake wa Israel kuwa hao Wamisri mnaowaona leo hamtawaona tena kamwe na mimi akaniambia kuwa  Wamisri waliokuwa katika maisha yangu sitawaona tena kamwe nami nina amini hivyo na zaidi. 

Wewe je unataka kuonja furaha na amani hii niliyo nayo mimi leoo?Njoo kwa Yesu leo ndugu yangu mkubali awe Bwana na Mwokozi katika maisha yako nawe utapata penzi la kweli lisilo na mawaa. Yale yote yaliomwiba kwako yatakwisha na hautayapata wala kuyaona tena.

Nampenda Yesu sana na Yeye anakupenda pia karibu upate furaha ya kweli na tufurahi pamoja.

Wednesday, January 26, 2011

BARIKIWA KWA KUMWOMBEA MWENZAKO (WAMAMA)

Jeremiah 29:11 "for I know the plans I have for YOU, declares the LORD
"Never give the devil a ride, he will want to take over the driving."

Dear Woman of God
Be still for a while and praise God for His favor, His grace and His awesomeness, God is able to do the impossible and is always near
He loves us unconditionally.

Dear God:
this is my friend, whom I love and this is my prayer for her
Help her live her life to the fullest, Please promote her and cause her to excel above her expectations. Help her to shine in the darkest places where it is impossible to love. Protect her at all times,
lift her up when she needs you the most, and let her know when
she walks with you, She will always be safe.

Love you Girl

asante dada Brenda D kwa kunitumia

Monday, January 24, 2011

The Principle of Evaluation: Assess Your Situation

“Do not think of your self more highly than you ought, but rather think of yourself with sober judgment in accordance with the measure of faith God has given you.” Romans 12:3 (NIV)
"Do you believe you can change? Do you believe things can be different in your life?"
You can’t get to where you need to be until you first know where you are. That’s why, if you want to change anything in your life, Romans 12 says you need to humbly assess or evaluate your current state.
Now the reason I say humbly is because we don’t want to admit what’s not working in our lives. We don’t want to admit we’re in a hole or things aren’t working out. We don’t like to admit we need to change. We want to pretend we have it all together. That’s the barrier of pride.
Humility is the ingredient for change that will counter our pride. We have to start by admitting we don’t have it all together.
What are you pretending is not a problem in your life? Is it a problem in your marriage? An addiction? A problem with your body? Whatever it is, you need to start with an honest evaluation of yourself.
Change also takes faith. Do you believe you can change? Do you believe things can be different in your life? Ask yourself how much faith you will need in order to make the changes you want in your life. Is it more than you have right now? That’s evaluating the measure of your faith.
I want you to grow in your faith because without faith it is impossible to please God. I want you to grow in the measure of your faith, and I want you to set goals that are so big they force you to grow in faith.
Where will you get this faith to grow? Romans 10:13 says, “Faith comes from hearing the Word of God” (NIV). In other words, if you read the Bible more, then your faith will grow, then your trust in God will deepen, and then you will change.

PRAYER (MAOMBI)

Father, in the Name of Jesus, bless me even while I'm reading this prayer and bless the one that sent this to me in a special way. Open doors in our lives today, Save and set free!
Give us a double portion of your Spirit as we take back everything that the devil has stolen:
****Emotional Health
****Physical Health
****Finances
****Relationships
****Children
**** Jobs
****Homes
****Marriages
I cancel every plot, plan and scheme the enemy has devised against us in the NAME OF JESUS.
And I declare:
NO WEAPON FORMED AGAINST US WILL PROSPER.
I speak LIFE into every dead situation. And, I thank You that nothing is over until YOU say it's over! Speak prophetically into our lives and to our situations:
****our households are blessed;
**** our health is blessed;
**** our marriages are blessed;
**** our finances are blessed;
**** our relationships are blessed;
**** our businesses are blessed;
**** our jobs are blessed;
**** our children are blessed;
**** our grandchildren are blessed;
**** our parents are blessed;
**** our siblings are blessed;
**** our ministries are blessed;
**** our decisions are blessed;
**** our friends are blessed.
**** Mortgages are paid and debts canceled; our hearts' desires are on the way;


According to YOUR perfect will and plan for our lives.
YOU SAID YOU'D NEVER FORSAKE US! IN JESUS' NAME!
AMEN!

asante sasa dada Brenda kwa kunitumia zidi kubarikiwa
 

Friday, January 21, 2011

KUBALI KUWA MLAWI

The Brooklyn Tabernacle Choir is currently accepting applications for membership. If you are interested, and are a member or in the process of becoming one, please apply online at:www.brooklyntabernacle.org/choirapp


The Brooklyn Tabernacle Music Staff

Haya kwa wale wenye karama ya kuimba au kama unajijua unayo sauti kama chiriku au hata ya kumtoa nyoka pangoni jiunge basi kuwa member wa Brooklyn Tabernacle Choir ukamwimbie Bwana maana kwenye sifa Mungu huwapo kwani yeye anapenda nyimbo za sifa na shukrani kuliko kitu kiwayo chote naye hushuka nakuja kuweka makao hivyo hima jiandikishe tumwimbie Bwana Sifa (kubali kuwa Mlawi) Soma 2 M/ Nyakati 5: 11-14

BWANA YESU ANAKUMBIA NINI LEO HII

Mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha. Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwone haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.

Tuesday, January 18, 2011

PATA PUMZIKO LA KWELI KATIKA MWAKA HUU

BWANA YESU ASIFIWE SANA SANA NIMERUDI KWA UPYA NA MAMBO MAPYA, MWAKA MPYA NA KARNE MPYA.

Neno la Mungu linasema hivii ....................
"NJOONI KWANGU NINYI NYOTE MSUMBUKAO NA WENYE KULEMEWA NA MIZIGO  NAMI NITAWAPUMZISHA"

MWAKA huu ni mwaka wa urejesho wa amani, furaha, na nguvu mpya ya kushinda majaribu, vikwazo, vifungo mbalimbali viletwavyo na nguvu za giza za yule mwovu shetani. Hivyo basi mpendwa hakuna haja ya kubeba mizigo ya dhambi, kutokusamehe, uchungu n.k. tujifunze kusamehe na kutokuweka vinyongo songa mbele acha kuwabeba watu wakati huo umekwisha samehe na usonge mbele uuone wema na mkono wa Bwana katika maisha yako kwa mwaka huu wote na hata milele. Usikubali kujaribiwa na yule mwovu bibilia inatuambia hivii mshitaki wetu yule mwovu shetani ni kama simba angurumaye akizunguka huku na huko akitafuta mtu wa kummeza hivyo basi tujiepushe naye tumshinde kwa kujifunza kusamehe, kutolipiza  visasi, acha hasira zisizo na mpango, kataa chuki, na mambo mengine kama hayo tusome NENO LA MUNGU KWA BIDII KILA SIKU ambalo litafanya Roho Mtakatifu aweke makao katika mioyo yetu.

Acha kusumbuka na kuteseka njoo kwa Yesu tua mzigo wako kwake upate furaha na amani ya kweli katika maisha yako. Maana kwenye amani Roho Mtakatifu huwepo na unajua palipo Roho wa Bwana yote yanawezekana hata yale ambayo kwa akili za kibinadamu yalikuwa hayawezekani kwake yanawezekana. Yesu anatuambia kuwa tumpatie mizigo yetu iliyo mizito atupe wa kwake ambao ni mwepesi sasa kwa nini mpendwa ujibebeshe mizigo ambayo hakusaidii wala haikupi faida yoyote sana sana ni hasara na maumivu tele tele njoo kwa Yesu upate pumziko la milele.

Pia Yesu anasema tusivunje mioyo kwani kwa kupitia yeye tunayashinda yote, aliushinda ulimwengu na sisi tutaushinda. Hakuna kurudi nyuma wala kulegea viungo tuuvae ujasiri tusimame imara katika mwaka huu tuone penzi la kweli, uweza na nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na jinsi mkono wake ulivyo Mkuu.

Nawapenda wote na amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu.
Uwe na wakati mzuri. Amen

Godly Goals Require Faith

Without faith it is impossible to please God …. Hebrews 11:6 (NIV)
"We must set goals that are bigger than ones we can reach on your own."
Godly goals are set through faith. The Bible says, “Without faith, it is impossible to please God.” In order to please God, we must set goals that require faith.
What does this mean? It means we must set goals that are bigger than ones we can reach on your own.
For instance, I want you to set a health goal for this year. As I’ve said, if you don't have a health goal, then your goal is to stay the same or get worse. To move forward – to get healthier -- you must set a health goal.
Let’s say you need to take off some weight. If you say, ‘My goal is to lose one pound’ – well … you know you can do better than that. Set a goal based on what God tells you to do and I have no doubt that will be a goal that will require you to remain dependent upon Jesus.
You haven't believed God until you've attempted to do something that can't be done unless his power is at work in your life.

Tuesday, January 11, 2011

MAOMBI YA MWAKA MPYA

BABA NINALITUKUZA JINA LAKO NASEMA ASANTE SANA BWANA KWA KUWEZA KUTULINDA NA KUTUPA AMANI, ASANTE KWA ULINZI WAKO, BARAKA ZAKO NA UPENDO USIO NA KIPIMO, ASANTE KWA KUTUPA TUMAINI NA FURAHA KWA MWAKA ULIOPITA NAKUSHUKURU BWANA KWA KUTUVUSHA SALAMA NA SISI KUWEZA KUUONA TENA MWAKA 2011 ANZA NASI TENA KWA UPYA BWANA KATIKA MWAKA HUU NA KARNE HII MPYA JEHOVA ENDELEA KUTUTIA NGUVU, TUPE AMANI, FURAHA, UTU WEMA, FADHILI ZAKO, BUBUJIKO LA ROHO WAKO MTAKATIFU, NA UPENDO WA KWELI UUMBIKE NDANI YA MAISHA YETU, TUNDA LA ROHO MTAKATIFU LIZIDI KUUMBIKA NDANI YETU, TUPE ROHO YA UNYENYEKEVU NA MOYO ULIOPONDEKA, NA UWEPO WAKO BWANA USITUONDOKEE, BARIKI KAZI ZA MIKONO YETU, BARIKI WATOTO WETU NDOA ZETU, FAMILIA ZETU, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA HATA MAJIRANI ZETU WOTE  KWA MWAKA HUU MPYA NA KARNE NYINGINE BWANA, BARIKI KUINGIA KWETU NA KUTOKA KWETU, TUNASIHI KIBALI MBELE YAKO BWANA NA KWA WANADAMU PIA, TUNAOMBA KIBALI CHAKO POPOTE TUINGIAPO NA TUNAPOKANYAGA BWANA ONEKANIKA WEWE BWANA KILA TUINGIAPO, MANENO YA VINYWA VYETU JEHOVA YATAWALIWE NA WEWE TUWE NI WATU WA KUBARIKI KWA MWAKA HUU NA SIO WA KULAANI TUWE NI WATU WA KUTIA MOYO NA KUWALETA WATU KWAKO EE BWANA, ROHO MTAKATIFU FANYA MAKAO KATIKA VILINDI VYA MIOYO YETU. TEMBEA NASI TUSHIKE MKONO UTUONGOZE WEWE KWA MWAKA HUU WOTE NA HATA MILELE NA MILELE NINAOMBA HAYA KUPITIA JINA LA MWANAO MPENDWA YESU KRISTO  ALIYE BWANA NA MWOKOZI KATIKA MAISHA YETU. AMEN AMEN AMEN

HERI YA MWAKA MPYA WENYE BARAKA TELE NA AMANI YA BWANA IWATAWALE KATIKA MAISHA YENU NA FAMILIA ZENU KWA UJUMLA
 MZIDISHIWE BARAKA NA BWANA YESU KRISTO ALIYE HAI

HAPPY NEW YEARRRRRRRRRRRR.